JE! Kaini alimpatia mke wake wapi?

JE! Kaini alimpatia mke wake wapi?

SWALI: Kaini baada ya kumuua ndugu yake Abeli, alikimbilia katika nchi ya Nodi, Naomba kufahamu Je! Huko alipatia wapi mke na kuzaa naye watoto? (Mwanzo 4:16).

JIBU: Ukisoma Mwanzo 5:1-5 utaona inasema….

“1Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya;
2 mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa.
3 Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi.
4 Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, AKAZAA WANA, WAUME NA WAKE
5 Siku zote za Adamu alizoishi ni miaka mia kenda na the lathini, naye akafa.”

Sasa kwenye Mstari huo wa 4 utaona kuwa kumbe mbali ya Kaini na Abeli kuzaliwa na Adamu kulikuwa na wana wengine wa kike na wakiume waliokuja kuzaliwa kwenye familia yao pia, na ndio huko huko Kaini alipojitwalia mke.

SWALI: Kama KAINI alitwaa mke ambae alizaliwa na Adamu na Hawa ambao ni wazazi wake kwahiyo alimuoa dada yake je,kwahiyo nihalali kumuoa mwanamke ambae ni dada yangu wa damu?”.


JIBU: Kumbuka hata Adamu mwenyewe hakwenda kumtwaa mke kutoka kwenye familia nyingine, bali katika ubavu wake mwenyewe, hivyo kama ni undugu basi Adamu na hawa wana undugu mkubwa zaidi ya Dada na kaka…

Unaona? Mungu aliruhusu iwe hivyo mwanzoni kwa ajili ya uzazi, ili watu waongezeke, lakini baadaye Mungu alitoa maagizo kuwa ni makosa mtu kutwaa ndugu wake wa karibu na kumfanya kuwa mke wake..

Mambo ya walawi 18:6 “Mtu ye yote aliye wa kwenu asimkaribie mwenziwe aliye wa jamaa yake ya karibu ili kumfunua utupu; mimi ndimi Bwana”.

Na pia mstari wa 9 unasema…

9″ Utupu wa umbu lako, binti ya baba yako, au binti ya mama yako, kwamba alizaliwa nyumbani mwenu au kwamba alizaliwa kwengine, utupu wa hao usifunue”.

Kwahiyo ni machukizo kuoa ndugu yako yoyote yule wa karibu.

Ubarikiwe

   Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp


Mada Nyinginezo:

MTI WA UZIMA NA MTI WA MAARIFA.

UZAO WA NYOKA.

SIKUKUU 7 ZA KIYAHUDI ZINAFUNUA NINI KWETU?

IMANI NI KAMA MOTO.

SAUTI AU NGURUMO?

RUDIA, TENA NA TENA KUMWOMBA MUNGU USIKATE TAMAA.


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
8 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
1 year ago

jambo wa pendwa wa mungu nashukuru sana kwa mafundisho mnayo tufunza mimi ni mkongomani sijakua bado na phone ya watsapp lakini nitajitahidi ni nunue ili mniunge nanipate ku faidika zaidi asante sana

Emanuel lucas
Emanuel lucas
2 years ago

Shalom mpendwa naomba mniunge watsapp

Elizabeth kasichi
Elizabeth kasichi
2 years ago

Shalom! Biblia imeandikwa kwa mtiririko katika mwanzo 4 tunaona kuna kaini na habeli sura ya 5 Luna seth na wana wengine, sura ya 4;14 kaini anaogopa kwamba watu wengine wakimuona watamuua ni watu gani hao. Maana sura ya 4 inaelezea matukio yote ya kaini na habeli means duniani baada ya habeli kufa walibaki watatu tu!

BARAKA PAUL
BARAKA PAUL
2 years ago

Leave your message

Tadei Emmanuel chaula
Tadei Emmanuel chaula
2 years ago

Niunge

Gwankelahani Mwamakula
Gwankelahani Mwamakula
1 year ago
Reply to  Admin

Sasa mbona kwenye WhatsApp hamruhusu mtu kutuma wala kuchangia mada zaidi yenu maadmini tu? Naomba majibu WhatsApp