Kwanini MUNGU Anampa Nabii Hosea maagizo ya Kumuoa mwanamke kahaba? (Hosea 3)

Kwanini MUNGU Anampa Nabii Hosea maagizo ya Kumuoa mwanamke kahaba? (Hosea 3)

JIBU: Mungu alimpa maagizo nabii Hosea kuoa mke aliye kahaba, sio kwasababu Mungu, anahalalisha usherati, hapana! Kusudi la Mungu kufanya vile ni kutaka kuwaonyesha wana wa Israeli ni jinsi gani wao wanavyofanya uasherati katika roho zao mbele zake kwa kuyaacha maagizo yake.. Kwahiyo nabii Hosea alipooa mke wa uzinzi, ilikuwa kama ishara ya Bwana kutaka kuwaonyesha wana wa Israeli mambo wanayoyafanya mbele zake…

Sasa Bwana alitaka endapo watu watakapomwuliza Hosea kwanini ameoa mke ambaye ni mzinzi…ndipo Hosea awajibu, kama mimi ninavyoudhiwa na huyu mwanamke mzinzi ndivyo na ninyi (wana wa Israeli) mnavyomuudhi Bwana kwa kufanya uzinzi mbele zake kwa kulihalifu agano lake na kuabudu miungu migeni, ukisoma habari ile yote kwa urefu utaona jambo hilo. 

Sio mara ya kwanza Bwana kutoa ishara kupitia maisha ya watu, ukisoma biblia mahali pengine utaona Nabii ezekieli Bwana anamwagiza ale kinyesi, mahali pengine akate nywele zake kwa upanga azigawanye sehemu tatu….sehemu nyingine anaambiwa ahame nyumba yake kwa kutoboa ukuta, huku amejifunika macho kumwonyesha Mfalme wa Yuda Sedekia kwamba wakati majeshi ya wakaldayo yatakapouzingira mji kwa miaka miwili, yeye atatoroka kwa njia ya kutoboa ukuta wa mji, na hatimaye watamkamata na kumtoboa macho yake sawasawa na nabii Ezekieli alivyoonyesha… 

Ezekieli 12:1 Neno la Bwana likanijia tena, kusema,

2 Mwanadamu, wewe unakaa kati ya nyumba iliyoasi, watu ambao wana macho ya kuona, ila hawaoni, wana masikio ya kusikia, ila hawasikii; kwa maana ni nyumba iliyoasi.

3 Basi, mwanadamu, funga tayari vyombo kwa uhamisho, ukahame wakati wa mchana mbele ya macho yao; nawe utahama toka mahali pako hapa mpaka mahali pengine mbele ya macho yao; labda watafahamu, wajapokuwa ni nyumba iliyoasi.

4 Nawe utatoa vyombo vyako, wakati wa mchana, mbele ya macho yao, kana kwamba ni vyombo vya kuhamishwa; nawe mwenyewe utatoka, wakati wa jioni, mbele ya macho yao, kama watu watokavyo katika kuhamishwa.

5 Toboa mahali ukutani mbele ya macho yao, ukachukue vitu kwa kuvipitisha pale.

6 Mbele ya macho yao utajitwika begani pako, na kuvichukua nje gizani; utafunika uso wako, hata usiione nchi; kwa maana nimekuweka uwe ishara kwa nyumba ya Israeli.

7 Nikafanya vile vile kama nilivyoamriwa; nalitoa vyombo vyangu wakati wa mchana kana kwamba ni vyombo vya kuhamishwa, na wakati wa jioni nikautoboa ukuta kwa mkono wangu; nikavitoa gizani, nikavichukua begani, mbele ya macho yao.

8 Asubuhi neno la Bwana likanijia, kusema,

9 Mwanadamu, nyumba ya Israeli, je! Nyumba ile iliyoasi, hawakukuambia, Unafanya nini wewe?

10 Waambie, Bwana MUNGU asema hivi; Ufunuo huu wamhusu mkuu wa Yerusalemu, na nyumba yote ya Israeli walio kati yao.

11 Sema, Mimi ni ishara kwenu; kama mimi nilivyotenda, wao nao watatendwa vile vile; watahamishwa, watakwenda kufungwa.

12 Naye mkuu aliye kati yao atachukua begani katika giza; naye atatoka kwenda zake; watatoboa mahali ukutani, wapate kuvichukua vyombo vyao nje; atafunika uso wake, kwa sababu hataiona nchi kwa macho yake.

13 Tena wavu wangu nitautandika juu yake, naye atanaswa kwa mtego wangu; nami nitampeleka Babeli, mpaka nchi ya Wakaldayo; lakini hataiona, angawa atakufa huko.

14 Nami nitawatawanya kwa pepo zote wote wamzungukao ili wamsaidie, na vikosi vyake vyote; nami nitaufuta upanga nyuma yao.

15 Nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana; nitakapowatawanya kati ya mataifa, na kuwatupa-tupa katika nchi zote” 

Ukizidi kusoma utaona mahali pengine Nabii mmoja Bwana alimwagiza amwambie mtu ampige mpaka atoke majeraha.

 1 Wafalme 20: 35 “Basi, mtu mmoja wa wana wa manabii akamwambia mwenzake kwa neno la Bwana, Nipige, nakusihi. Akakataa yule kumpiga.

36 Akamwambia, Kwa sababu hukuisikiliza sauti ya Bwana, angalia, mara ukitoka kwangu simba atakuua. Na mara alipotoka kwake, simba alimwona, akamwua.

37 Ndipo akaona mtu mwingine, akasema, Nipige, nakusihi. Yule mtu akampiga, hata kumpiga na kumtia jeraha.”

 Sasa mambo haya yote ni ishara ya Bwana kutaka kuzungumza na wana wa Israeli kwa kupitia maisha ya watu, kwahiyo hiyo ndio sababu ya Mungu kumwambia Nabii Hosea akaoe mke wa kikahaba..na pia kumbuka Hosea mwenyewe hakuwa mzinzi ni yule mwanamke aliyeambiwa amwoe ndiye aliyekuwa ni kahaba. Kwa jinsi hiyo hiyo mambo hayo yanavyochukiza mbele za watu ndivyo hivyo hivyo yanavyochukiza mbele za Mungu, pale watu wanapoasi maagano yake. 

Ubarikiwe!


Mada zinazoendana:

RAHABU.

MPENDEZE MUNGU ZAIDI.

MADHARA YA DHAMBI YA UASHERATI.

MSHAHARA WA DHAMBI:

JE! ULEVI NI DHAMBI?

IELEWE SAUTI YA MUNGU.

VITA BADO VINAENDELEA.


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments