MTI WA UZIMA NA MTI WA MAARIFA.

MTI WA UZIMA NA MTI WA MAARIFA.

Mwanzo 2:8-9 “Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya.

Bwana Mungu akachipusha katika ardhi kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa; na mti wa uzima katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya”.

Tukisoma katika mistari hii hapa juu, tunaona kabisa mwanzoni Mungu alipopanda bustani mashariki mwa Edeni Mungu aliiweka miti ya aina tatu bustanini nayo ni:

  • Kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa.
  • Mti wa uzima katikati ya bustani,
  • Na mti wa ujuzi wa mema na mabaya.

Hapa usichanganye hii ni miti aina tatu tofauti yenye tabia tatu tofauti tofauti, tukianzana na mti wa kwanza, 

  1. Kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa

Sasa mti wa aina hii unaozungumziwa hapa biblia inasema Mungu alichepusha katika ardhi ”KILA” mti unaofaa kwa chakula, tunaona hili neno “KILA” linamaanisha ni miti mingi na sio mti mmoja, mfano wa miti hii ni  mapeasi, matofaa, maembe,mananasi, ndizi, mapasheni,mapapai n.k. hii ni miti aina ya kwanza ya mti ambayo Mungu aliichepusha katika ardhi kwa ajili ya chakula cha mwanadamu kumfaa kwa ajili ya mwili wake na mahitaji yake akiwa bustanini, yeye pamoja na wanyama wake wote Bwana aliompa. Adamu hakupewa masharti juu ya miti hii alikuwa na uhuru wa kula jinsi apendavyo na jinsi atakavyo kama biblia inavyosema. 

      2. Mti wa uzima katikati ya bustani. 

Huu ni mti aina ya pili ambao Bwana aliuweka bustanini, tunaona kuwa mti wa pili na watatu imebeba tabia, na hii miti miwili ya mwisho ipo mmoja, mmoja tu. sio mingi kama ile aina ya kwanza ya mti, sasa huu mti wa uzima. Huu mti ulikuwa hauonekani kwa macho, kama miti mingine, na ulikuwa ni mti ambao ukila matunda yake (sio kula kwa mdomo) unapata uzima ambao umebeba ule uzima wa milele. Kwahiyo huu mti Mungu aliuweka kama hazina kwa Adamu endapo ikitokea wameupoteza ule uzima, waende kula matunda yake wapate uzima tena, Mungu kwa kujua kuwa mwanadamu baadaye atapoteza uzima aliuumba huu mti kuwa kama akiba ya tiba baadaye. Na huu mti Adamu hakuwa na matumizi nao kwasababu tayari alikuwa na uzima wa milele ndani yake.

Lakini tunaona baadaye Adamu alipodondoka kwenye dhambi na kupoteza uzima ndani yake alitamani kwenda kula matunda ya mti wa uzima lakini njia yake ilikuwa imeshafungwa ikilindwa mpaka wakati ulioamuriwa wa hiyo njia kufunguliwa ufike.kwahiyo ilipasa mwanadamu aijue hiyo njia ni ipi. soma mwanzo 3:24.  kuanzia hapo wanadamu ndipo walipoanza kufa na kuanza kutafuta suluhisho la kuishi milele tena, na ndipo hapo wanadamu walipoanza kuliitia jina la BWANA, mwanzo 4:26

  Lakini sasa sisi tunaoishi wakati huu wa neema tunajua NJIA ni ipi?… na huo MTI WA UZIMA  ni nani?… na MATUNDA yake ni nini?..na tunajua sio mwingine zaidi ya BWANA wetu YESU KRISTO mwokozi wetu Haleluya!! .Kwa ufafanuzi mfupi wa jambo hili tusome maandiko yafuatayo…

  Yohana 14:6″ Yesu akamwambia, Mimi ndimi NJIA, na KWELI, na UZIMA; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.” Unaona hapo!?? hakuna njia yoyote sisi tunaweza kumfikia Baba kama ilivyokuwa hapo mwanzo kabla ya Adamu kuasi isipokuwa kwa njia ya YESU tu!    na pia tena ukisoma

 Yohana 6:47-51″ Amin, amin, nawaambia, Yeye aaminiye yuna UZIMA WA MILELE.

48 Mimi ndimi chakula cha uzima.

49 Baba zenu waliila mana jangwani; wakafa.

50 Hiki ni chakula kishukacho kutoka mbinguni, kwamba mtu akile wala asife.

51 Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki, ATAISHI MILELE. Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.”

  Maandiko hayo hapo juu  yanaonyesha wazi kabisa kuwa hakuna uzima wa milele mahali pengine popote nje ya BWANA YESU KRISTO, matunda ya porini siku zote hayajawahi kumpa mtu uzima wa milele, kwahiyo mtazamo wa kuwa matunda ya mti wa uzima ni matunda yafananayo na ya mwituni sio sahihi,(ni kukosa tu Roho ya mafunuo) kwasababu matunda ya kawaida hayawezi kutupa sisi uzima wa milele, biblia inasema hakuna wokovu wowote nje ya Yesu Kristo, Hivyo basi maana ya kula matunda ya mti wa uzima ni kulitafakari na kuliamini NENO la Bwana Yesu tu, na kusafishwa kwa damu yake ambaye yeye ndiye huo mti wa uzima. Na hili NENO la Mungu ndilo liletalo Utii,Upendo,Amani,Uvumilivu,Fadhili,Kiasi,Utakatifu,Utu wema,Hekima,Haki n.k. 

Wagalitia 5:22″ Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria”.

   3.Mti wa ujuzi wa mema na mabaya.

Kama tulivyouona mti wa pili, haukuwa mti wa kawaida kama ule wa kwanza, ndivyo ulivyo na huu pia, mti huu nao upo mmoja na umebeba tabia ya kipekee kwamba ukila matunda yake, utapata maarifa ya ujuzi wa mema na mabaya na ndio mti pekee Mungu aliomkataza mwanadamu asiule, alimwambia kabisa siku atakapokula tu matunda ya mti ule atakufa hakika. Lakini mwanadamu alikaidi  akala na ikapelekea hata sisi wote tukaingia katika hali ya laana ambayo tunayo mpaka sasa, lakini ashukuriwe Mungu njia ya mti wa uzima (YESU KRISTO) imeshafunguliwa tunao ukombozi wetu.

Huu mti asili yake ni mauti, na mauti inaletwa na shetani, kama vile uzima unavyoletwa na Yesu Kristo vivyo hivyo mauti inaletwa na shetani. Kwahiyo huu mti alikuwa ni “shetani” mwenyewe, na matunda yake ni “kwenda kinyume na NENO la Mungu” ndio huko unazaliwa uongo,uasherati,uuaji,ulevi,wizi,ulafi,sanamu,ufisadi,wivu, usengenyaji, n.k. ambayo mwisho wake ni mauti.

sasa kilichotendeka Edeni. shetani ambaye ndio ule mti wa ujuzi wa mema na mabaya, alimwingia nyoka. na nyoka akaenda kumdanganya Hawa kwa mafundisho yake ya uongo aliyoyatoa kwa baba yake shetani. kumbuka Mungu alimwonya mwanadamu adumu katika maagizo yake, asitafute maarifa mengine nje na Neno lake, lakini kwa kuwa shetani alijua mwanadamu anapenda maarifa ambayo Mungu alimkataza mwanadamu asiyatafute, na shetani siku zote ni mpingamizi wa Mungu hivyo alimjaribu katika hayo hayo, ndipo alipomwingia nyoka, na kumshawishi Hawa kutokumtii Mungu. na njia shetani aliyotumia ni ushawishi wa kufanya uasherati, kwa maana nyoka alimwambia ukila matunda haya utafanana na Mungu ukijua mema na mabaya. kumbuka kuwa nyoka hakuwa mnyama “reptilia” kama tunavyomwona leo, bali alikuwa ni mnyama anayekaribiana sana na mwanadamu, alikuwa na uwezo wa kuongea, kutafakari, alikuwa anatembea kwa miguu miwili, kwa ufupi alikuwa kama mtumwa wa mwanadamu.Baada ya kulaaniwa ndipo alipotembea kwa matumbo, na kula mavumbi.

nyoka alikuwa mnyama aliyekuwa anakaribiana sana na mwanadamu, mbali na wanyama wengine, katika wanyama wanaokaribiana na mwanadamu, alikuwa akitoka nyani anafuata nyoka kisha mwanadamu. tazama picha juu.

Kwahiyo baada ya nyoka kuingiwa na shetani na kwenda kufanya uzinzi na Hawa, Hawa naye akaenda kumpa tunda (kuzini) na mumewe, ikapelekea Hawa kubeba mimba ya mapacha wawili wasiofanana, akamzaa Habili na Kaini kila mmoja akiwa na baba yake. Baba yake Habili alikuwa ni Adamu na baba yake Kaini alikuwa ni nyoka. kumbuka nyoka hakuwa kama nyoka tunayemwona leo.(kwa ufafanuzi mrefu fuatilia somo langu liitwalo UZAO WA NYOKA.)

Tujue kuwa kitendo cha kula matunda ya porini kama peasi, embe au papai, hakuwezi kumfanya mtu ajione kuwa uchi, na kama walikula matunda yale kwa midomo hiyo midomo ndiyo ingetakiwa ilaaniwe na sio viungo vya uzazi, tunaona kabisa baada ya kula tunda (kuzini) walikimbilia kwenda kujifunika sehemu zao za siri, kiashirio kuwa hizo sehemu zao ndizo zilizohusika katika tendo lile.

Ni dhahiri kabisa kuwa mwanadamu ni vigumu kushawishika kwa matunda ya porini, kwa sababu alikuwa na matunda mengine mengi kwanini sasa aende kula lile la katikati ya bustani ya Edeni? Jibu ni dhahiri kuwa ni dhambi ile ile ya asili ambayo shetani alifahamu atampata nayo mwanadamu kirahisi na ndiyo hiyo hiyo anayowapata nayo wanadamu hata leo na hii sio nyingine bali ni dhambi ya uasherati.

Mungu ni yeye yule jana, na leo na hata milele, alichokichukia Edeni ndio hicho hicho anakichukia hata leo. Kama ilikuwa kula tunda kama tunda la kawaida ni makosa angeendelea kukichukia na kukikemea hicho kitu mpaka leo. lakini ni dhambi ya uasherati Mungu anayoichukia hata leo na ndiyo inayowaangusha watu wengi, kwa wanaojiita wakristo na wasio wakristo. kwahiyo hili tunda la kutokuliamini neno la Mungu (ambalo kwa mara ya kwanza shetani alilitangaza kwa kivuli cha uzinzi) hadi leo watu wanalila hili tunda. kama vile tu watu wa Mungu wanavyoendelea kula matunda ya mti wa uzima (kama tulivyosema ni kuliamini na kuliishi Neno la Mungu)  ili wapate uzima wa milele vivyo hivyo hadi leo watu wanaendelea kula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya kama uasherati, n.k. kwa ajili ya mauti yao wenyewe. Akipandacho mtu ndicho atakachovuna.

Kwahiyo ndugu jambo lile lile lililotendeka Edeni linaendelea kutendeka hadi leo, je! unakula matunda ya ule mti wa ujuzi wa mema na mabaya huku ukijua kabisa Mungu amekataza usiyale ambayo tunayajua matunda yake ndiyo haya, uasherati, na mengine ni uongo, ulevi,ufisadi, usengenyaji, ushoga, ulafi, anasa, kuupenda ulimwengu, wizi, rushwa, tamaa mbaya, chuki, wivu, n.k. unafahamu kabisa mwisho wa haya ni mauti kama Mungu alivyosema pale Edeni, siku utakapokula matunda hayo utakufa hakika. Apple haliwezi likakufanya ufe! na biblia inasema mshahara wa dhambi ni mauti. Kimbilia kwa Yesu sasa ukale matunda ya Mti wa uzima, upate uzima wa milele, Bwana Yesu alisema itakufaidia nini uupate ulimwengu mzima na kupata hasara ya nafsi yako au utatoa nini badala ya nafsi yako. Kuzimu ipo, tazama miti miwili ipo mbele yako, chagua moja MTI WA UZIMA au MTI WA MAUTI. 

Warumi 6:16 Hamjui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake katika kumtii, mmekuwa watumwa wake yule mnayemtii, kwamba ni utumishi wa dhambi uletao mauti, au kwamba ni utumishi wa utii uletao haki.

 Chaguo lipo kwako. Wakati umekwenda sana na mlango wa neema unakaribia kufungwa, je! umejiweka tayari.?? Umejazwa Roho Mtakatifu,??

Neema ya Mungu iwe pamoja nawe.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

UZAO WA NYOKA.

JE! NYWELE ZAKO ZINAOTA AU ZIMESIMAMA?

UNAFANYA NINI HAPO?


Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
13 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Minister Nehemiah
Minister Nehemiah
1 year ago

Mungu akuhurumie maana unajaribu kufundisha mafundisho yako na sio biblia ila hata km nia yako Ni njema basi jitahidi kumsikiliza Roho wa Mungu maana hadi natetemeka kwa mafundisho yako potofu Mungu akurehem
Kwanza unatakiwaujue kuwa biblia haijawahi kukosea ilipo taja uzinzi haikusema ugali,hivyo basi nilazima uelewe kuwa tunda sio uzinzi
Kumbuka usiongeze wala kupunguza neno ktk mafundisho yako Ufunuo22:18,19
Lazima ujue hawa alipo danganywa kula tunda hakula pamoja na Nyoka alikula yeye na akampa Adam ale ila Nyoka hakula Soma biblia yako vzr mwanzo3:5,6,
Kulingana na uongo wa Nyoka hawa akala kwakutamani kufanana na Mungu Kama alivyo danganywa na shetani kwakujua mema na mabaya sio uzinzi
Pili Mungu ali mli wabarikia Adam na hawa akisema zaeni mkaongezeke hata kabla ya kula tunda Soma biblia yako vzr mwanzo1:28. pia ndoa Ni mpango wa Mungu na sio mpango wa shetani hilo utambue Soma mwanzo2:23,24 hivyo basi nikuulize mtu aweza kuzini na mkewe? Mungu akusaidie Sana.
Ndugu usipotoshe maandiko kwa hadisi za kizee zisizo kuwa za dini
1timo4:7,2timo2:14-19 Nakukumbusha tu…
Dunia imebeba mafundisho mengi kwani hata shuleni tulijifunza kuwa binadamu wa kwanza alikuwa nyani na ikawa ukisema ni Adamu unawekewa kosa ukitazama nikama kweli lkn ni elimu tu za dunia so usiipokee Kila elimu mtumishi utapotea hta paulo anasema aliwauwa walio wa njia hii akizani anamfanyia bwana ibada.
Je niwangapi wametoka na mafundisho yako wakiamini kuwa kweli lakini kumbe ni hadithi za kizee Bwana akuhurumie kwakweli.

MICHAEL NZUNGU
MICHAEL NZUNGU
1 year ago

Fanya utafiti wako mzuri hapana ku kurupuka na kupayukapayuka, kama ADAMU Na EVA wangelifanya uzinzi ao EVA Angelizini na nyoka biblia ingeandika wazi, kwaiyo unapotosha ilo andiko mpendwa !

Anonymous
Anonymous
1 year ago
Reply to  MICHAEL NZUNGU

Kweli kwa hiyo baba umetupiga kitu kizito kichwani,Bibliya haina haja ya kusema tunda ikiwa niuzinzi umefanyika,ndugu taka sana kufundishwa na Roho wa Mungu usije ukafiri unawaokowa watu kumbe unawapotosha na kuwa weka mbele za hukumu

Gloire luther
Gloire luther
1 year ago
Reply to  MICHAEL NZUNGU

Kweli kwa hiyo baba umetupiga kitu kizito kichwani,Bibliya haina haja ya kusema tunda ikiwa niuzinzi umefanyika,ndugu taka sana kufundishwa na Roho wa Mungu usije ukafiri unawaokowa watu kumbe unawapotosha na kuwa weka mbele za hukumu

Muriithi Gitonga
Muriithi Gitonga
2 years ago

Nina swali hapa, Ikea Hawa kafanya ngono na adamu, na mungu alikuwa kawambia wazaane, wangezaana she pasipo kuingiliana?

Emmanuel Kitengule
Emmanuel Kitengule
2 years ago

Asante sana na barikiwa sana mwalimu.Maarifa haya ni ya viwango.

Anonymous
Anonymous
2 years ago

Naona kama post ipo sensational sana na mengi uliyoandika ni mawazo yako na tafsiri zako mwenyewe badala ya hasa kinachoelezwa na biblia.

unataka kunambia Mwandishi wa Mwanzo alishindwa kusema Mungu alimuweka Shetani Eden na kwamba Adam na hawa wasimsikilize? Kwamba mwandishi alishindwa kusema Mungu aliwakataza Adam na hawa kujuana??

Rowland asante Robert
Rowland asante Robert
3 years ago

Nashukuru kwa marifa haya, ubarikiwe na BWANA!

Nimefatilia somo hili kwa ukaribu na baadhi ya maswali yakajengeka kichwani Mwangu.
1.kwa maelezo hayo Inaonekana Adamu alikuwa anajua kilicho tokea kabla ya yeye kula tunda; maana kama alikuwa hajui kilicho tokea, yeye kosa lake lilikuwa wapi maana aliye zini ni haw(Eva)a hiyo hatia inakuwaje kwake? Au walitakiwa kuishi kama kaka na dada? Kwamaana nyingine basi hawa(Eva) alitoka nje ya ndoa kwa kushawishiwa na nyoka aliyeingiwa na ibilisi wafanye uzinzi,na kwamaana hiyo adamu, baada ya tendo hilo nyoka na Hawa alitakiwa asikubali kula nae tunda?

2. Nmeona kunakifungu mtumishi umeeleza kuwa kama wangekula matunda ya kawaida wasingekimbilia kuficha sehemu zao za siri, swali langu naomba kujua je hapo awali walikuwa wanavaa nguo?

3. Kwenye Biblia imemtaja vizuri nyoka/Joka(Serpent) hasa ktk ufunuo kama ni ibilisi na shetani
Ufunuo wa Yohana 12:9
“[9]Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.” Na sifa kubwa ktk Biblia ya nyoka huyu alikuwa ni mwerevu. Hizi sifa nyingine mtumishi tunaweza kuzisoma wapi?

Naomba msaada mtumishi nipo kujifunza, nimetatizika kidogo!

Nashukuru kwa somo zuri, kazi yako ni njema utalipwa na BWANA.

Joseph
Joseph
1 year ago

Barikiwa sana mwalimu

Caroline athamas
Caroline athamas
3 years ago

Hakika ukiijua kweli ya Neno LA Mungu utakua huru kwelikweli Bwana atusaidie tuzidi kuwekwa huru kweli Kwa Neno lake LA uzima

Daudi reuben
Daudi reuben
4 years ago

Haya bhana soma biblia vizuri