Maana yake nini “Wajapochimba waingie katika kuzimu, mkono wangu utawatoa huko”

Maana yake nini “Wajapochimba waingie katika kuzimu, mkono wangu utawatoa huko”

SWALI: Huu mstari una maana gani? Amos 9:2 “Wajapochimba waingie katika kuzimu, mkono wangu utawatoa huko; nao wajapopanda hata mbinguni, nitawatelemsha toka huko”


JIBU: Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe, Ni muhimu kufahamu sio kila mahali panapozungumzia Neno mbinguni katika biblia panamaanisha “mbinguni kule Malaika watakatifu walipo” Hususani katika agano la kale. Neno mbinguni pia linaweza kutumika na wapagani kumaanisha mbingu yao, kadhalika mbinguni kunaweza kumaanisha “sehemu iliyo inuka sana”.

Mtu aliyejiinua sana moyo wake katika roho anaonekana amepanda mpaka mbinguni.

Hali kadhalika sio kila mahali panalipoandikwa neno “kuzimu” katika biblia hususani agano la kale, kuna maanisha kule kuzimu, roho za viumbe walioasi zilipo!..hapana! sehemu nyingine panapotajwa neno kuzimu panamaanisha mahali pa chini sana. Kwamfano mtu aliye katika vifungo vingi vilivyomfanya awe chini sana, katika roho ni kama yupo kuzimu. (Yona na Mariamu na Hana).

Kwamfano tunaweza kusoma mistari ifuatayo ili tupate kuelewa vizuri.

Yona 2:1 “Ndipo Yona akamwomba Bwana, Mungu wake, katika tumbo la yule samaki,

  2 Akasema, Nalimlilia Bwana kwa sababu ya shida yangu, Naye akaniitikia; KATİKA TUMBO LA KUZİMU NALİOMBA, Nawe ukasikia sauti yangu.

3 Maana ulinitupa vilindini, Ndani ya moyo wa bahari; Gharika ya maji ikanizunguka pande zote; Mawimbi yako yote na gharika zako zote zimepita juu yangu”

Sasa hapo Yona sio kwamba alishuka kuzimu, mahali pa wafu, hapana, bali katika mazingira ya lile tumbo la samaki alilokuwemo ndio akakufananisha na KUZIMU. Mahali pabaja mfano wa kuzimu. Na mtu anapokuwa katika mazingira hayo yanayofananishwa na kuzimu, anaweza kupandishwa juu na kutoka huko, kama Yona na Hana mama yake Samweli.

1Samweli 2:6 “Bwana huua, naye hufanya kuwa hai; Hushusha hata kuzimu, tena huleta juu.

7 Bwana hufukarisha mtu, naye hutajirisha; Hushusha chini, tena huinua juu”

Na andiko lingine ndio hilo la kwenye Amosi 9:2 “Wajapochimba waingie katika kuzimu, mkono wangu utawatoa huko; nao wajapopanda hata mbinguni, nitawatelemsha toka huko”

Lakini mtu anayeshuka katika ile kuzimu halisi ya sehemu ya wafu walioasi, biblia inasema hawezi kurudi tena wala hawezi kutoka huko.

Ayubu 7:9 “Kama vile wingu likomavyo na kutoweka, Ni vivyo huyo ashukaye kuzimuni hatazuka tena kabisa.  Hatarudi tena nyumbani kwake, Wala mahali pake hapatamjua tena”.

Kwahiyo unaweza ukawa unapitia hali fulani katika hii dunia, ambapo mahali ulipo ni kama kuzimu, kila kona unaona giza limekuzunguka na mashaka, huoni unafuu popote, nataka nikuambie lipo tumaini kwa Kristo, maadamu bado unaishi, Bwana anaweza kukunyanyua tena na kukutoa huko Kuzimu, ulipo na kukupandisha juu, Hivyo Mwamini, omba kwa bidii na mshukuru, siku isiyokuwa na jina utaona miujiza.

Vivyo hivyo unaweza kuwa katika mahali fulani, au ukawa katika nafasi fulani na moyo wako  ukainuka sana, pengine ukajiona ni mungu-mtu, kila mtu anakuogopa, kila mtu anakuhofu au wewe ukajiona ni bora sana kuliko wengine wote wanaokuzunguka, nataka nikuambia mbele za Mungu, umejiinua na kufika mbinguni, na biblia inasema wote wajikwezao watashushwa (Luka 14:11).

Kwa maelezo marefu kuhusu  mbungini fungua hapa  >> mbinguni  ni wapi?

Hivyo mstari huo katika Amosi hauzungumzii Mbingu halisi, Malaika watakatifu waliopo, bali wala hauzungumzii Kuzimu halisi, wafu waliokufa katika dhambi walipo… Bali inazungumzia hali fulani ya maisha ambayo mtu yupo chini sana mfano wa kuzimu, na hali fulani ya maisha ambayo mtu kajiinua sana juu mfano wa mbingu.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

FUNGUO ZA UZIMA, MAUTI NA KUZIMU.

ALIKUWAKO NAYE HAYUKO, NAYE YU TAYARI KUPANDA KUTOKA KUZIMU.

CHAPA YA MNYAMA

UJIO WA BWANA YESU.

MAMBO MANNE,YANAYODHOOFISHA UOMBAJI WAKO.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments