ALIKUWAKO NAYE HAYUKO, NAYE YU TAYARI KUPANDA KUTOKA KUZIMU.

ALIKUWAKO NAYE HAYUKO, NAYE YU TAYARI KUPANDA KUTOKA KUZIMU.

Ni nani huyo “alikuwako naye hayuko, naye yu tayari kupanda kutoka kuzimu.?”

Shalom, Jina la Yesu Kristo Bwana wetu lizidi kubarikiwa daima Tunapaswa tukumbuke kuwa Kila tunapoiona siku mpya, basi ndivyo tunavyopiga hatua nyingine kuufikia ule mwisho..Zile dalili kuu za mwisho wa dunia zimeshatimia, hivyo wakati wowote tunaweza kulishuhudia tukio la unyakuo wa kanisa..Na kwa wale watakaobaki nao pia watazishuhudia kazi za mpinga-Kristo pamoja na mapigo yote ya Mungu aliyoyazungumzia katika Ufunuo 16

Hivyo tunapaswa tuwe macho vilevile tuwe na maarifa ya kutosha kuzijua njama za shetani,..Inasikitisha kuona kuwa watu wengi bado wanadhani mpinga-Kristo ni mtu ambaye atatoka sehemu isiyojulikana, na kwamba atakuwa ni mtu wa ajabu sana.. vilevile kazi zake zitaonekana ikishafika kipindi cha dhiki kuu, hatujui kuwa roho hii ilishaanza kutenda kazi tangu zamani, ikaleta uharibifu wake kwa sehemu, na ndiyo hiyo hiyo itakayoleta dhiki kuu wakati wa mwisho… kwa kutumia ufalme wake ule ule uliotumia mwanzoni.

Kama vile maandiko yanavyosema:

Mhubiri 1:9 “Yaliyokuwako ndiyo yatakayokuwako; na yaliyotendeka ndiyo yatakayotendeka; wala jambo jipya hakuna chini ya jua”

Ni kweli kuwa hata kazi za mpinga-Kristo hazitakuwa mpya, zilishakwisha kuanza tangu zamani, na alishawahi kuzifanya huko nyuma na ni kitu kile kile ambacho atakuja kukifanya tena huko mbeleni,.. Kama Bwana wetu Yesu Kristo tunavyomtazamia kuja kwake… Na tunafahamu kuwa atatoka mbinguni, yeye mpinga-Kristo ana kitu gani hasa cha ziada tusijue atokako?..Hivyo usitazamie mambo makubwa sana, wala usitazamie mambo mapya sana, ..wala usitazamie atotokea nje ya ufalme tofauti na ule ule aliotokea nao mwanzo kuleta uharibifu..

Sasa tukirudi katika kitabu cha Ufunuo sura ya 17, tunaona Yohana akionyeshwa yule mwanamke kahaba, aliyeketi juu ya mnyama mwekundu sana.

tusome..

Ufunuo 7:1 Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi;

2 ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo ya uasherati wake.

3 Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.

4 Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake.

5 Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.

6 Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu ajabu kuu.

7 Na yule malaika akaniambia, Kwani kustaajabu? Nitakuambia siri ya mwanamke huyu, na ya mnyama huyu amchukuaye, mwenye vile vichwa saba na zile pembe kumi.

8 Yule mnyama uliyemwona alikuwako, naye hayuko, naye yu tayari kupanda kutoka kuzimu na kwenda kwenye uharibifu. Na hao wakaao juu ya nchi, wasioandikwa majina yao katika kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, watastaajabu wamwonapo yule mnyama, ya kwamba alikuwako, naye hayuko, naye atakuwako.

9 Hapo ndipo penye akili zenye hekima. Vile vichwa saba ni milima saba anayokalia mwanamke huyo.

10 Navyo ni wafalme saba. Watano wamekwisha kuanguka, na mmoja yupo, na mwingine hajaja bado. Naye atakapokuja imempasa kukaa muda mchache.

11 Na yule mnyama aliyekuwako naye hayuko, yeye ndiye wa nane, naye ni mmoja wa wale saba, naye aenenda kwenye uharibifu.

12 Na zile pembe kumi ulizoziona ni wafalme kumi, ambao hawajapokea ufalme bado, lakini wapokea mamlaka kama wafalme muda wa saa moja pamoja na yule mnyama.

13 Hawa wana shauri moja, nao wampa yule mnyama nguvu zao na mamlaka yao.

14 Hawa watafanya vita na Mwana-Kondoo, na Mwana Kondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio walioitwa, na wateule, na waaminifu.

mwonekano wake:

Kumbuka mwanamke huyu anaonekana amelewa kwa damu za watakatifu na damu ya mashahidi wa Yesu,..Unaweza kujiuliza amelewaje lewaje, amewezaje kuwachinja hao watu wote na kunywa damu yake, angali yeye ni mwanamke tu?… Utagundua kuwa ni kwasababu hakuwa peke yake,bali ni yule mnyama anayemwendesha chini yake ndiye anayemsaidia kufanya hizo kazi…

Na mnyama huyo biblia inasema alikuwepo naye hayupo naye yupo tayari kupanda katika uharibifu..Ili kufahamu kama alikuwepo lini,.. tunapaswa turudi kwenye historia kidogo, wakati Yohana anaonyeshwa maono hayo tayari utawala wa Rumi ulikuwa umeshawaua wayahudi wengi sana,.. na watakatifu wengi sana..Kuanzana na Kristo mwenyewe Bwana wetu, Ni warumi ndio waliomsulubishwa..baadaye tena AD 70 uliuwa wayahudi wengi, na kuliteketeza hekalu,.. jambo ambalo Bwana Yesu alishalitabiri katika Mathayo 24, juu ya kuhusuriwa kwa Yerusalemu, baadaye tena katika majira ya kanisa la Pili hadi wakati wa matengenezo ya Kanisa, Rumi hii ambayo baadaye ilikuja kuwa ya kidini chini ya Kanisa Katoliki ilihusika na mauaji ya watakatifu Zaidi ya milioni 68, wasiokuwa na hatia yoyote, waliuliwa kwasababu tu waliishika Imani yao, na kukataa mafundisho mengine ambayo hayakuwa mafundisho ya mitume..Kama Yohana 16:2 inavyosema “naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada.”

Maangamizi yake:

Historia inaonyesha hakuna ufalme wowote, au dini yoyote, wala utawala wowote uliowahi kuuwa wakristo kwa idadi kubwa ya watu namna hiyo,..zaidi ya utawala wa KiRumi.. sio tu kuifikia idadi hiyo , bali hata kukaribia idadi hiyo haijawahi kutokea..

Dini ya kikatoliki iliyokuwepo wakati ule si sawa na iliyopo sasahivi, wakati ule ilikuwa mtu yeyote ambaye anaonekana tu kwenda kinyume na Imani ile adhabu yake ilikuwa ni kifo,.. na ilikuwa imeenea kila mahali, ilikuwa ni dini ya kitaifa, unaaishi chini ya uongozi wa kidini (Ilikuwa ni serikali ya kidini), hakukuwa na mtu wa kawaida aliyeruhusiwa kusoma biblia kama ilivyo sasahivi, isipokuwa viongozi wa juu sana wa kanisa hilo..,

Si Chuki:

Tunapozungumza hivi sio kwamba tunatangaza chuki,.. au tunahukumu..au tunashambulia imani za wengine.. au tunaonyesha kwamba upande mmoja unajua zaidi ya mwingine.. au tunawachukia wakatoliki, au tunatangaza Imani mpya au dhehebu jipya. Hilo sio lengo hata kidogo,… lakini tunazungumza ukweli wa kimaandiko, ili kwamba anayetaka kuelewa aelewe na kila mtu asikie ukweli… UTAWALA WA RUMI, NA DINI YA RUMI NDIYO MAKAO MAKUU YA SHETANI NA MPINGA-KRISTO ATAKAYEKUJA!…Kwasababu huko nyuma alikuwepo alishatenda kazi hizo, naye yupo sasa hivi, isipokuwa amepoa kwa muda na ndiye atakayepanda na kwenda katika uharibifu siku za usoni.

Pembe Kumi:

Tukilifahamu hilo tunaweza kuona ni wakati gani huu tunaishi, kwamba ule mwisho umekaribia sana, na moja ya hizi siku utawala huu utapata nguvu tena, na safari hii hautaleta dhiki peke yake bali utatumia mataifa kusababisha dhiki, hizo ndio zile pembe 10 za Yule mnyama.

Mpinga-Kristo atakayetokea huko kwa kupitia kiti cha UPAPA.. atazitumia serikali zote za dunia nzima kuhimiza chapa..Na mtu yeyote atayeonekana hana chapa hiyo basi adhabu yake itakuwa ni mateso na kifo, kama wakati ule ule wa makanisa ya mwanzo..

Unaweza kuona tunaishi katika kipindi cha hatari kiasi gani?,..kumbuka “Alikuwako, naye hayuko, naye yu tayari kupanda kutoka kuzimu.

Kama wewe hujaokoka unasubiri nini?. Kila kiumbe kinafahamu wakati tuliobakiwa nao ni mchache hadi shetani mwenyewe anajua hilo na ndio maana anafanya kazi zake kwa kasi mno,.. kama tunavyoona wimbi zito la manabii wa uongo waliopo sasahivi..Tendo lililobaki ni kuTubu dhambi zako haraka kama hujatubu…kisha ukabatizwe kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako (Matendo 2:3), na Bwana mwenyewe atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu kukulinda na kukuongoza katika kuijua kweli yote. Mpaka ile siku ya Unyakuo.

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mafundisho mengine:

 

Ubarikiwe.

Maran atha!

Mada Nyinginezo:

CHAPA YA MNYAMA

MPINGA-KRISTO

MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

KWANINI DAUDI ALIKUWA NI MTU ALIYEUPENDEZA MOYO WA MUNGU?

 

NI KIPI MUNGU ANACHOKITAZAMA ZAIDI, MOYO AU MWILI?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments