Jina la Yesu Kristo libarikiwe. Karibu katika mwendelezo wa mafunzo ya vitabu vya Biblia.
Tulishapitia vitabu 15 vya kwanza, kama hujavipitia nakushauri uvipitie kwanza ili tuende pamoja katika vitabu hivi vya mbele….Kitabu cha Mwisho kilikuwa ni kitabu cha Ezra..Ambaye tuliona Biblia inamtaja kama Mwandishi mwepesi…Ezra alitokea baada ya Wana wa Israeli kuingia Babeli.. kama tulivyojifunza huko nyuma kimtitiriko basi vile vitabu vya manabii kama vile Isaya, Yeremia,Ezekieli Danieli, na vinginevyo vingepaswa vitangulie kuorodheshwa kwenye kabla ya kitabu cha Ezra, lakini ameruhusu viwe katika mtiririko huo kwa mapenzi yake mwenyewe.
Na leo kwa Neema za Bwana tutaviangalia vitabu viwili vya Nabii mmoja, ambavyo matukio yake yalitangulia kabla ya wakati wa Ezra..Navyo ni vitabu vya YEREMIA pamoja na MAOMBOLEZO. Vitabu hivi viwili viwili vimeandikwa na mtu mmoja (Yeremia)…Tumeviruka vitabu vya hapo katikati vinavyofuata baada ya kitabu cha Ezra kama vile Nehemia, Esta, Ayubu, Zaburi, Mithali, na Ayubu, tutakuja kuvipitia hapo baadaye. Hivyo nakushauri baada ya kusoma somo hili, wewe mwenyewe chukua nafasi ya kuvipitia vitabu hivyo viwili, Na Bwana atakufunulia na mengi Zaidi ya haya, kwani hapa tunaandika kama summary tu.
Kama wengi wetu tunavyojua kuwa Yeremia Mungu alimwita tangu akiwa mdogo sana..na aliambiwa atakuwa Nabii wa Mataifa. Sasa kama ni mwanafunzi wa Biblia utagundua kuwa Huduma kubwa ya Yeremia ilikuwa ni kuwatabiria mataifa juu ya hukumu Mungu atakayoileta juu ya Mataifa yote ulimwenguni kutokana na maasi ya dunia. Ikiwemo na Taifa la Mungu (Israeli) humo humo.
Mungu alitaka kuiadhibu dunia kwa kupitia Babeli. Aliupa Ufalme wa Babeli nguvu, ambao aliutumia huo kuwa kama fimbo kwa mataifa yote duniani ikiwemo Israeli ndani yake. Babeli iliyalazimisha mataifa yote yalitumikie taifa hilo. Na Mungu aliruhusu hilo ili kuyakomesha mataifa ya dunia yanayofanya maasi..Sasa kumbuka sio kwamba Babeli lilikuwa ni Taifa takatifu hapana!.Ni Mungu tu alilichagua kama chombo chake kutimiza kusudi fulani tu!..Baada ya kumaliza kutimiza kusudi hilo, nalo pia Mungu aliliadhibu kwa maasi yake.
Hivyo Mungu akamtuma Yeremia kuyaambia mataifa hayo hatari iliyopo mbele yao..Wengi walimdharau Yeremia na kumwona Nabii wa uongo,..wengine walimwona ni kibaraka wa mfalme Nebkadneza wa Babeli…wengine walimwona kama ni kimtu tu kimejizukia kutabiri tabiri ujinga..n.k Lakini Yeremia alikuwa ni Nabii kweli wa Mungu.
Alizunguka kwenye mataifa yote mpaka Misri kwa Farao (Soma Yeremia 25:5-29)..kumwonya lakini hawakumsikia.. Na mwisho akamalizia kwa Taifa lake Teule kulionya kuwa litakwenda Utumwani miaka 70 lisipotaka kujinyenyekeza lakini nalo pia halikusikia..Ukisoma kitabu cha Yeremia na 2Wafalme wa pili utaona ni jinsi gani Yeremia alivyosumbuliwa na Sedekia Mfalme wa Israeli.
Kutokana na wana wa Israeli kutokutii, Unabii wa Yeremia ukatimia juu yao..Wakauawa na Nebukadneza mfalme wa Babeli na wengine wakachukuliwa mateka na kwenda kukaa huko kwa miaka 70.
Siku hiyo ya maangamizi ilipofika wana wa Israeli walichukuliwa mateka mpaka Babeli…Na Nabii Yeremia ndiye alikuwa ni nabii pekee aliyeyashuhudia maangamizi hayo na uteka huo.. siku hiyo ilikuwa ni siku ya uchungu sana, maana theluthi ya watu walikufa kwa Tauni na wengine kwa njaa kutokana na kukosekana chakula wakati huo, kwani mji huo ulikuwa umehusuriwa kwa muda mrefu sana, na majeshi ya Babeli hivyo, hata chakula ndani ya mji kilikuwa ni shida, kwasababu hakukuwa na kinachoingia wala kutoka, theluthi nyingine walikufa kwa kuuawa kikatili na jeshi la Nebkadneza, wanawake na Watoto walichinjwa chinjwa kama kuku na theluthi nyingine walichukuliwa Mateka huku wamefungwa mpaka Babeli Utumwani. Mapigo hayo manne ndiyo yaliyoipata Israeli yaani NJAA, TAUNI,UPANGA na KUCHUKULIWA MATEKA.
Ezekieli 5: 11 “Kwa sababu hiyo, kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, hakika kwa kuwa umepatia unajisi patakatifu pangu, kwa matendo yako yote niyachukiayo, na kwa machukizo yako yote, kwa sababu hiyo mimi nami nitakupunguza; wala jicho langu halitaachilia, wala sitaona huruma. 12 Theluthi yenu mtakufa kwa tauni, na kwa njaa watakomeshwa ndani yako; na theluthi yenu wataanguka kwa upanga pande zako zote; na theluthi yenu nitawatawanya kwa pepo zote, kisha nitafuta upanga nyuma yao. 13 Hivyo ndivyo ghadhabu yangu itakavyotimia, nami nitatosheleza hasira yangu juu yao, nami nitafarijika; nao watajua ya kuwa mimi, Bwana, nimenena kwa wivu wangu, nitakapokuwa nimeitimiza ghadhabu yangu juu yao”.
Ezekieli 5: 11 “Kwa sababu hiyo, kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, hakika kwa kuwa umepatia unajisi patakatifu pangu, kwa matendo yako yote niyachukiayo, na kwa machukizo yako yote, kwa sababu hiyo mimi nami nitakupunguza; wala jicho langu halitaachilia, wala sitaona huruma.
12 Theluthi yenu mtakufa kwa tauni, na kwa njaa watakomeshwa ndani yako; na theluthi yenu wataanguka kwa upanga pande zako zote; na theluthi yenu nitawatawanya kwa pepo zote, kisha nitafuta upanga nyuma yao.
13 Hivyo ndivyo ghadhabu yangu itakavyotimia, nami nitatosheleza hasira yangu juu yao, nami nitafarijika; nao watajua ya kuwa mimi, Bwana, nimenena kwa wivu wangu, nitakapokuwa nimeitimiza ghadhabu yangu juu yao”.
Na maneno hayo yalitimia kama yalivyo. Theluthi walikufa kwa njaa na tauni, theluthi nyingine kwa kuuawa kwa upanga, na theluthi nyingine kwenda Babeli. Israeli pakabakia kuwa tupu!..Na nabii Yeremia alikuwa anayashuhudia hayo.. Jambo hilo likamhuzunisha sana, maana aliwaonya sana waIsraeli wamgeukie Mungu lakini wakakataa, hivyo maangamizi hayo yalimchoma moyo sana kwani aliyashuhudia kwa macho yake yaliyokuwa yanatendeka…Ndipo kwa msukumo wa Roho akaandika kitabu cha MAOMBOLEZO. (Kitabu hichi killiandikwa na Yeremia mwenyewe)..Kuombolezea kilicholikumba Taifa teule la Mungu..
Taifa ambalo hapo kwanza lilikuwa linaogopwa!..lenye utisho wa ki-Mungu..Taifa ambalo Mfalme mkuu wa dunia Sulemani alitokea, taifa ambalo Mungu wake alisifika kwa kutokushindwa na lolote,..leo hii linakwenda utumwani!!…Taifa ambalo Mungu alilitoa Misri kwa mkono Hodari na kumwaibisha Farao leo hii linarudi tena utumwani kwa aibu kuu kama hiyo!!?..Hayo kweli ni maombolezo na uchungu mkali. Ndio maana ukisoma kitabu cha Maombolezo utaona jinsi Nabii Yeremia anavyoitaja Israeli kwa kulifananisha na “binti Sayuni au mwanamke mjane”
Maombolezo 1:1 “Jinsi mji huu ukaavyo ukiwa, Huo uliokuwa umejaa watu! Jinsi alivyokuwa kama mjane, Yeye aliyekuwa mkuu kati ya mataifa! Binti mfalme kati ya majimbo, Jinsi alivyoshikwa shokoa! (shokoa maana yake ni kibarua wa ngazi ya chini kabisa!) 2 Hulia sana wakati wa usiku, Na machozi yake yapo mashavuni; Miongoni mwa wote waliompenda Hakuna hata mmoja amfarijiye; Rafiki zake wote wamemtenda hila, Wamekuwa adui zake”…. 5 Watesi wake wamekuwa kichwa, Adui zake hufanikiwa; Kwa kuwa Bwana amemtesa Kwa sababu ya wingi wa makosa yake; Watoto wake wadogo wamechukuliwa mateka Mbele yake huyo mtesi. 6 Naye huyo binti Sayuni Enzi yake yote imemwacha; Wakuu wake wamekuwa kama ayala Wasioona malisho; Nao wamekwenda zao hawana nguvu Mbele yake anayewafuatia.”
Maombolezo 1:1 “Jinsi mji huu ukaavyo ukiwa, Huo uliokuwa umejaa watu! Jinsi alivyokuwa kama mjane, Yeye aliyekuwa mkuu kati ya mataifa! Binti mfalme kati ya majimbo, Jinsi alivyoshikwa shokoa! (shokoa maana yake ni kibarua wa ngazi ya chini kabisa!)
2 Hulia sana wakati wa usiku, Na machozi yake yapo mashavuni; Miongoni mwa wote waliompenda Hakuna hata mmoja amfarijiye; Rafiki zake wote wamemtenda hila, Wamekuwa adui zake”…. 5 Watesi wake wamekuwa kichwa, Adui zake hufanikiwa; Kwa kuwa Bwana amemtesa Kwa sababu ya wingi wa makosa yake; Watoto wake wadogo wamechukuliwa mateka Mbele yake huyo mtesi.
6 Naye huyo binti Sayuni Enzi yake yote imemwacha; Wakuu wake wamekuwa kama ayala Wasioona malisho; Nao wamekwenda zao hawana nguvu Mbele yake anayewafuatia.”
Maombolezo 1:16 “Mimi ninayalilia mambo hayo; Jicho langu, jicho langu linachuruzika maji; Kwa kuwa mfariji yu mbali nami, Ambaye ilimpasa kunihuisha nafsi; Watoto wangu wameachwa peke yao, Kwa sababu huyo adui ameshinda. 17 Sayuni huinyosha mikono yake; Hakuna hata mmoja wa kumfariji; Bwana ametoa amri juu ya Yakobo, Kwamba wamzungukao wawe watesi wake; Yerusalemu amekuwa kati yao Kama kitu kichafu. 18 Bwana ndiye mwenye haki; Maana nimeiasi amri yake; Sikieni, nawasihi, enyi watu wote, Mkayatazame majonzi yangu; Wasichana wangu na wavulana wangu Wamechukuliwa mateka”.
Maombolezo 1:16 “Mimi ninayalilia mambo hayo; Jicho langu, jicho langu linachuruzika maji; Kwa kuwa mfariji yu mbali nami, Ambaye ilimpasa kunihuisha nafsi; Watoto wangu wameachwa peke yao, Kwa sababu huyo adui ameshinda.
17 Sayuni huinyosha mikono yake; Hakuna hata mmoja wa kumfariji; Bwana ametoa amri juu ya Yakobo, Kwamba wamzungukao wawe watesi wake; Yerusalemu amekuwa kati yao Kama kitu kichafu.
18 Bwana ndiye mwenye haki; Maana nimeiasi amri yake; Sikieni, nawasihi, enyi watu wote, Mkayatazame majonzi yangu; Wasichana wangu na wavulana wangu Wamechukuliwa mateka”.
Maombolezo 2: 1 “Jinsi Bwana alivyomfunika binti Sayuni Kwa wingu katika hasira yake! Ameutupa toka mbinguni hata nchi Huo uzuri wa Israeli; Wala hakukikumbuka kiti cha miguu yake Katika siku ya hasira yake. 2 Bwana ameyameza makao yote ya Yakobo, Wala hakuona huruma; Ameziangusha ngome za binti Yuda Katika ghadhabu yake; Amezibomoa hata nchi Ameunajisi ufalme na wakuu wake. 3 Ameikata pembe yote ya Israeli Katika hasira yake kali; Ameurudisha nyuma mkono wake wa kuume Mbele ya hao adui, Naye amemteketeza Yakobo kama moto uwakao, Ulao pande zote”.
Maombolezo 2: 1 “Jinsi Bwana alivyomfunika binti Sayuni Kwa wingu katika hasira yake! Ameutupa toka mbinguni hata nchi Huo uzuri wa Israeli; Wala hakukikumbuka kiti cha miguu yake Katika siku ya hasira yake.
2 Bwana ameyameza makao yote ya Yakobo, Wala hakuona huruma; Ameziangusha ngome za binti Yuda Katika ghadhabu yake; Amezibomoa hata nchi Ameunajisi ufalme na wakuu wake.
3 Ameikata pembe yote ya Israeli Katika hasira yake kali; Ameurudisha nyuma mkono wake wa kuume Mbele ya hao adui, Naye amemteketeza Yakobo kama moto uwakao, Ulao pande zote”.
Ukiendelea kusoma mlango wa tatu pia ni maombolezo tu kwa kilichotokea juu ya Taifa la Mungu..
Maombolezo 3: 42 “Sisi tumekosa na kuasi; Wewe hukusamehe. 43 Umetufunika kwa hasira na kutufuatia; Umeua, wala hukuona huruma. 44 Umejifunika nafsi yako kwa wingu, Maombi yetu yasipite. 45 Umetufanya kuwa takataka, na vifusi Katikati ya mataifa. 46 Juu yetu adui zetu wote Wametupanulia vinywa vyao. 47 Hofu imetujilia na shimo, Ukiwa na uharibifu”.
Maombolezo 3: 42 “Sisi tumekosa na kuasi; Wewe hukusamehe.
43 Umetufunika kwa hasira na kutufuatia; Umeua, wala hukuona huruma.
44 Umejifunika nafsi yako kwa wingu, Maombi yetu yasipite.
45 Umetufanya kuwa takataka, na vifusi Katikati ya mataifa.
46 Juu yetu adui zetu wote Wametupanulia vinywa vyao.
47 Hofu imetujilia na shimo, Ukiwa na uharibifu”.
Na Baada ya maombolezo hayo, Yeremia kwakuwa ni nabii wa Mungu na Anamjua Mungu sana. Alijua kuwa mateso hayo ni ya muda tu!. Hayatadumu milele, ni ya kitambo tu!. Ni kweli wamemwasi Mungu na Mungu kawakasirikia hata kuwauza kwa maadui zao…lakini ni kwa muda tu. Kwasababu Mungu hawezi kumtupa mtu milele. Kwa kulijua hilo akaandika maneno yafuatayo..
Maombolezo 3: 31 “Kwa kuwa BWANA HATAMTUPA MTU HATA MILELE. 32 MAANA AJAPOMHUZUNISHA ATAMREHEMU, Kwa kadiri ya wingi wa huruma zake. 33 Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu. Wala kuwahuzunisha. 34 Kuwaseta chini kwa miguu Wafungwa wote wa duniani, 35 Kuipotosha hukumu ya mtu Mbele zake Aliye juu, 36 Na kumnyima mtu haki yake, Hayo Bwana hayaridhii kabisa”.
Maombolezo 3: 31 “Kwa kuwa BWANA HATAMTUPA MTU HATA MILELE.
32 MAANA AJAPOMHUZUNISHA ATAMREHEMU, Kwa kadiri ya wingi wa huruma zake.
33 Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu. Wala kuwahuzunisha.
34 Kuwaseta chini kwa miguu Wafungwa wote wa duniani,
35 Kuipotosha hukumu ya mtu Mbele zake Aliye juu,
36 Na kumnyima mtu haki yake, Hayo Bwana hayaridhii kabisa”.
Unaona ijapokuwa wameuzwa lakini Mungu anatoa maneno ya matumaini kuwa hatawatupa milele,.. ipo siku inakuja watafunguliwa kutoka katika utumwa wao..Na watarudi tena kuwa Taifa teule la Mungu endapo wakitubu huko walipo…
Kuudharau unabii ni kubaya sana. Hususani unabii unaokutabiria mwisho wa mambo yote. Wengi wanapenda kutabiriwa mambo mazuri tu! Lakini hawapendi kuambiwa kuwa mshahara wa dhambi ni mauti. Nabii Yeremia yeye mwenyewe hakupenda kuwatabiria watu kila siku habari za hukumu ijayo..Lakini ilimbidi afanye vile ili watu angalau wasalimike kwa maana ni kweli hukumu ilikuwa ipo karibu sana..sasa itamfaidia nini awafiche halafu aje kuona ndugu zake wanachinjika mbele ya macho yake. Ni heri awaambie wakatae wenyewe kama alivyofanya kuliko asingewaambia halafu awaone wanachinjika vile, ni heri aonekane anahukumu kuliko kutowajuza watu kinachokuja mbeleni…Nafikiri haya maombolezo aliyoyaandika hapo juu yangekuwa yenye uchungu mara elfu kama wakingekufa pasipo kujua chochote.
Huyo ni Nabii wa kweli ambaye anawaambia ukweli juu ya mwisho wao huku yeye mwenyewe akiomboleza..sio kwamba alikuwa anafurahia. Kadhalika Bwana Yesu anatuonya.. “kuna hukumu inakuja”..Hatuambii hivyo huku anafurahia..bali huku anatuombolezea kwa yatakayotukuta tusipotubu. Mshahara wa nguo fupi uvaazo na make-up uwekazo usoni ni jehanamu!! huo ndio ukweli usisikilize watu wanaokudanganya huko na huko wanaojiita ni watu wa Mungu..mshahara wa uzinzi na uasherati ni jehanamu, mshahara wa ufisadi, na kutokusamehe ni jehanamu. Mshahara wa kuishi nje ya Kristo vile vile ni jehanamu.
Kama hujampa Kristo Maisha yako. Haijalishi unatenda haki kiasi gani upo hatarini sana. Hivyo nakushauri ufanye uamuzi sahihi leo, kwasababu huijui Kesho.
Bwana akubariki sana.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho mengine:
Ikiwa utapenda kupitia uchambuzi wa vitabu vilivyotangulia bofya hapa >>> VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 6
Na kwa mwendelezo bofya hapa >> VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 8 (Kitabu cha Ezekieli)
Kwa maombezi/ Ushauri/ Ratiba za Ibada/Maswali/ Whatsapp/ Piga namba hizi: +255693036618/ +255789001312
Maran atha!
Mada Nyinginezo:
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1
Yeshuruni ni nani katika biblia?
KANUNI RAHISI YA KUFANIKIWA.
JINSI YA KUJIWEKA KARIBU NA MUNGU.
Rudi Nyumbani:
Print this post
Umenifundisha pakubwa sana Mungu wa mbinguni akubariki.
Amen uzidi kubarikiwa.