Yeshuruni ni nani katika biblia?

Yeshuruni ni nani katika biblia?

SWALI: Huyu Yeshuruni  ni nani kwenye biblia?. Na kwanini alinenepa na kumdharau mwamba wa wokovu wake (Kumb.32:15)?.


JIBU: Yeshuruni ni jina lingine la Taifa la Israeli lililotumika katika biblia ya kiyahudi hususani katika mashahiri,..Neno hili linaonekana mara 4 katika biblia soma (Kumbukumbu 32:15, 33:26, 33:5 na Isaya 44:2).

Hivyo tukirudi pale kwenye Kumbukumbu 32:15

Inasema..

“Lakini Yeshuruni alinenepa, akapiga teke; Umenenepa, umekuwa mnene, umewanda; Ndipo akamwacha Mungu aliyemfanya, Akamdharau Mwamba wa wokovu wake

16 Wakamtia wivu kwa miungu migeni, Wakamkasirisha kwa machukizo.

17 Walitoa sadaka kwa pepo, si Mungu, Kwa miungu wasiyoijua, Kwa miungu mipya iliyotokea siku zilizo karibu, Ambayo baba zenu hawakuiogopa.

18 Humkumbuki Mwamba aliyekuzaa, Mungu aliyekuzaa umemsahau,”

Maneno hayo aliyazungumza Musa akiwa jangwani, kama unabii, kuonyesha jinsi Israeli watakavyokuja kumsahau Mungu wao huko mbeleni watakapofika katika nchi yenye maziwa na na asali, kwa kufanikiwa kwao, kwa nchi kuwazalia, kwa kutokuwa tena na jangwa, wala kula chakula cha aina moja, kwa kufanya biashara na kufanikiwa na kuwa matajiri, watamsahau Mungu wao aliyewatoa katika ile nchi ya Misri, watamsahau yule Mungu ambaye walikuwa wanamtumainia walipokuwa jangwani kwenye shida, watamdharau na kugeukia miungu mingine. Na unabii huo ulikuja kutimia vilevile kama Musa alivyotabiri katika shahiri lile walipofika nchi ya ahadi.

Hivyo ukikutana na Neno hilo Yeshuruni ni nani, basi ufahamu hilo ni jina lingine la Israeli.

Hata leo hii ni kawaida ya watu kumtafuta Mungu wakati wa shida, tu, lakini pale wanapofanikiwa, au pale ambapo hawana haja ya kitu chochote, wana afya, wana mali basi Mungu kwao si kimbilio tena,..wapo tayari hata kuutakana wokovu na kuona kama ni ushamba.Ndio maana Bwana Yesu alisema ni rahisi ngamia kupenya katika tundu la sindano kuliko Tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu..Utajiri wa aina yoyote ile ni ukweli usiopingika kuwa ni kikwako kikubwa sana katika ufalme wa mbinguni, kama vile umaskini uliopindukia ulivyo. Haimaanishi kuwa tusiwe matajiri lakini tunapaswa tutumie hekima katika kumwomba Mungu atupe kile ambacho ni sawasawa na uwezo wetu, tusije tukanenepa na kuwanda kama Yeshuruni na kumsahau Mungu, kama Aguri bin yake alivyotushauri katika Mithali 30:9.

Mithali 30:8“…………Usinipe umaskini wala utajiri; Unilishe chakula kilicho kadiri yangu.

9 Nisije nikashiba nikakukana, Nikasema, Bwana ni nani? Wala nisiwe maskini sana nikaiba, Na kulitaja bure jina la Mungu wangu.”

Ubarikiwe,jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Nyinginezo:

SADAKA YA MALIMBUKO.

JE! UNAYO NAFASI MBINGUNI?

Ni sahihi kumuita Mariamu mama wa Mungu?

JISHUSHE ILI MUNGU AKUHUDUMIE.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments