Ni sahihi kumuita Mariamu mama wa Mungu?

Ni sahihi kumuita Mariamu mama wa Mungu?

Kwa kuwa Bwana Yesu alipitia katika tumbo la Mariamu je! Ni sahihi kumuita Mariamu mama wa Mungu?

JIBU: Mariamu alimzaa BWANA kwa namna ya mwili, hivyo wakati Bwana alipokuwa duniani ndio Mariamu alijulikana kama mama wa Yesu, na sio mama wa Mungu. Bwana Yesu alipokuja hapa duniani alikuwa ni Mungu katika mwili lakini hakuja kutafuta kuabudiwa na ndio maana hakuna sehemu yoyote alijiita yeye ni Mungu, zaidi sana alikuwa anawarudisha watu wamuabudu Baba.   Kumbuka Mungu alipouvaa mwili ilimpasa afananishwe na mwanadamu kwa namna zote, azaliwe, ale chakula, asikie maumivu, alie, aone huruma, n.k. kama mwanadamu mwingine yeyote, si ajabu kumuona akiwa na Baba au bibi, au babu au mjomba, lakini haimaanishi kuwa yeye (YESU) yupo chini ya hao wote hapana..

Biblia inatueleza vizuri juu ya jambo hilo tukisoma katika..

Mathayo 22:41 Bwana Yesu alizungumza maneno haya;  

“41 Na Mafarisayo walipokusanyika, Yesu aliwauliza, akisema, Mwaonaje katika habari za Kristo?

42 Ni mwana wa nani? Wakamwambia, Ni wa Daudi.

43 Akawauliza, Imekuwaje basi Daudi katika Roho kumwita Bwana, akisema,

44 Bwana alimwambia Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwawekapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako?

45 Basi, Daudi akimwita Bwana, amekuwaje ni mwanawe?

46 Wala hakuweza mtu kumjibu neno; wala hakuthubutu mtu ye yote tangu siku ile kumwuliza neno tena”.

Unaona hapo? jibu litakuwa pia hivyo hivyo kwa Mariamu kwamba Yesu atakuwaje mwanawe na wakati bado ni Bwana wake? na yeye ni binti wa Mungu (Kwasababu kama Daudi alikuwa mkubwa kuliko Mariamu aliambiwa hivyo je! si zaidi yeye?).  

Hivyo sisi wote tunaomwamini YESU KRISTO mbele zake ni ndugu na dada, Na yeye akiwa kama Baba yetu. Kwahiyo ni muhimu tujue kutofautisha jinsi Mungu anavyotenda kazi katika ofisi zake tofauti, Mungu anapoonyesha unyenyekevu (kuzaliwa kibinadamu) haimaanishi kuwa mwanadamu yupo juu yake. Hapana anafanya hivyo kutuonyesha sisi njia bora kama watoto wake.  

Ubarikiwe sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

MARIAMU

JE! BIKIRA MARIA NI MALKIA WA MBINGUNI?

LILE TUMAINI LILILO NDANI YETU LINAPOULIZIWA.

UDHAIFU WA SADAKA!

SHUKURU KWA KILA JAMBO.

KWANINI YESU ALIMUITA BABA YAKE “ABA”?


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Boniface
Boniface
2 years ago

ndg jiepushe sana kutoa tafsiri ya neno la Mungu kwa yale usiyofahamu. unapotosha