Ubatizo wa moto ni upi?

Ubatizo wa moto ni upi?

JIBU: Ni kweli Yohana alibatiza kwa maji na alisema Bwana YESU atakapokuja atatubatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto..Sasa huu ubatizo wa moto ni upi?, kama tunavyofahamu moto hufanya kazi kuu tatu:

Ya kwanza: ni kuteketeza vitu dhaifu vyote visivyostahili. Kwamfano takataka..Vivyo hivyo Hatua hii ni ile Mungu anaichoma dhambi yote ndani ya mtu, hapo ndipo utakuta mtu tamaa ile ya kutenda dhambi aliyokuwa nayo kipindi cha nyuma inakufa yote, alikuwa anavuta sigara ghafla kiu ya sigara inakufa, alikuwa anakunywa pombe ghafla kiu ya pombe inakata, alikuwa ni mzinzi ghafla hata ile hamu ya kwenda kufanya uzinzi inakufa, alikuwa mtukanaji,ghafla anaanza kuona uzito tena kufungua kinywa chake na kutukana watu, alikuwa ni mwizi anajikuta hapendi tena uwizi, alikuwa msengenyaji ghafla dhamiri inamsuta akitaka kusengenya, alikuwa anatembea nusu uchi, ghafla anaanza kuona aibu hata kuzivaa hizo nguo n.k.

Ya pili: ni kuimarisha vitu vilivyo vigumu ili viwe vigumu na imara zaidi. kama vile dhahabu inapopitishwa kwenye moto.  

Hatua hii Roho Mtakatifu anapitisha mtu kwa lengo la kumuimarisha, Kama wafuaji wanavyofanya huwa wanayeyusha madini kwenye moto mkali ili baadaye yakishaganda yawe na mng’ao mzuri zaidi. , japo kwa nje yataonekana kama yanapitia dhiki ya hali ya juu kwa kuwekwa kwenye tanuru lakini yakishamalizwa kuchomwa matokeo yake yanaonekana kuwa bora zaidi kuliko yalipokuwa pale mwanzoni (Na ndio maana tunaona matofali ya udongo huwa yanachomwa kwanza, na ndipo yapelekwe kwa matumizi ya kujengea nyumba nzito,)..Hivyo kadhalika na kwa watoto wa Mungu..Tunapopokea Roho Mtakatifu..Mungu mwenyewe anaruhusu tupitie moto wa majaribu,ili kuihimarisha IMANI ZETU zisiwe dhaifu, hata tutakapopitia mambo magumu tusiweze kuanguka kirahisi.

Na ndio maana tunaona pale tu mtu anapoanza kuamini! mara anaanza kuona mambo ya nje yanabadilika, ghafla anakuchukiwa na ndugu au kutengwa, mwengine atapita misiba, mwingine magonjwa, mwingine vifungo, mwingine mapigo, mwingine anadorora kiuchumi, mwingine atatengwa n.k. mfano kama walivyopitia akina Ayubu, Yusufu n.k….Lakini Mungu kumpitisha mtu hivyo huwa sio kwa ajili ya kumwangamiza hapana bali ni kumuimarisha hivyo mtu kama huyo Bwana huwa anampa neema ya ziada kuyashinda hayo majaribu, kwasababu Mungu hawezi kuruhusu tujaribiwa kupita tuwezavyo

1Wakorintho 10:13 “Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili”.

  Na pia Ukisoma…  

1Petro 1: 6 Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali; 7 ili kwamba KUJARIBIWA KWA IMANI YENU, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo.”

  Hivyo huo ndio ubatizo wa Moto unaozungumziwa hapo..Kwahiyo mtoto yoyote wa Mungu ni lazima aupitie huo(Mitume walipitia, manabii walipitia na Bwana wetu Yesu Kristo alipitia kadhalika na sisi pia)..yaani ubatizo wa Maji pamoja na ubatizo wa Roho na wa moto .  

Na Hatua ya tatu: Ni kuchochea. Kwamfano moto ukiwashwa ndani ya bunduki, ile rasasi iliyo ndani yake ni lazima ifyatuke. Moto ukiwekwa chini ya sufuria yenye maji, yale maji ni lazima yatokote, Vivyo hivyo na moto wa Roho ukiachiliwa ndani ya mtu..Ni lazima atatoka na kwenda kuwahubiria injili wengine, hawezi kutulia..Na hicho ndicho kilichotokea ile siku ya Pentekoste mitume walipopokea ubatizo huu, muda huo huo walianza kuhubiri kwa kasi sana.

Ubarikiwe sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

JE, KAMA HAUNA UBATIZO SAHIHI HAUWEZI KUWA NA ROHO MTAKATIFU?

JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?

JE! UNAWEZA KUBATIZWA NA USIPOKEE ROHO MTAKATIFU?. NA JE! UNAWEZA KUPOKEA ROHO MTAKATIFU KWA KUWEKEWA MIKONO?

MELKIZEDEKI NI NANI?

SEHEMU YA MAANDIKO ILIYOFICHWA.


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
5 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Enock
Enock
1 year ago

Tuombeane

Elisha Mkumbwa
Elisha Mkumbwa
2 years ago

God bless you for the message

Anonymous
Anonymous
1 year ago
Reply to  Admin

Nataka kujuwa bibiliya kubatizwa maratatu