Je! shetani ni mwenye mwonekano mzuri au mapembe?

Je! shetani ni mwenye mwonekano mzuri au mapembe?

SWALI: Shetani kwa sasa ni mzuri wa umbo kama malaika watakatifu au ni mwenye mapembe na makwato na makucha marefu ya kutisha?


JIBU: Udanganyifu mkubwa uliopo duniani leo hii, ni pale watu wanapodhani kuwa shetani ni kiumbe chenye mapembe ya kutisha tu na kinakaa makaburini na kuzimu, hivyo wanadhani endapo mtu akikutana na kitu kama hicho kinachotisha sana ndio wamemuona shetani, Lakini hawajui kuwa yule alikuwa ni malaika kama wale wengine na alipoasi yeye na malaika zake, ndipo akawa shetani(Kumbuka maana ya neno shetani sio mapembe hapana bali ni MSHITAKI. 

Hivyo mara baada ya kuanguka ndipo akageuka na kuwa mshitaki wetu akitushitaki mbele za Mungu ..na biblia inaposema amelaaniwa haimaanishi kalaaniwa kimaumbile(ya nje) hapana, bali katika roho, na ndio maaana hata leo hii wanadamu wakilaaniwa na Mungu hawabadilili maumbile yao na kuwa vitu vya kutisha vyenye mapembe au viumbe visivyoeleweka, hapana bali roho zao ndio zinazobadilishwa. Kwahiyo shetani na malaika zake vivyo hivyo, wapo vilevile na ndio maana wanao uwezo wa kujigeuza jinsi wapendavyo hata kijifanya kama malaika wa Nuru wa Mungu, kadhalika pia hawajaondolewa ujuzi wao wote waliokuwa nao, isipokuwa hawana uwezo wowote wa kumshinda mtu aliye ndani ya Kristo.. Ukisoma;

2Wakorintho 11:3 “Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo.

14 Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.

15 Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao. 

Kwahiyo unaona hapo?..Hawa watu wote waasi pamoja na viumbe vilivyolaaniwa(malaika waovu), wapo tu kama walivyoumbwa, isipokuwa tabia za roho zao ndio zinazowatofautisha kwasababu hao tayari wameshalaaniwa wakiongejea mauti ya pili katika lile ziwa la moto..(Na tabia zao ndio zinazofananishwa na vitu vya kutisha). Kwahiyo ndugu kumbuka ni vita kubwa inayopigwa sasa hivi, haupigani na vibwengo, au majinamizi, n.k. bali unapigana na malaika na vita kubwa ni kukufanya wewe Uache Imani yako usiende mbinguni.Tujitahidi tufanye Imara wito wetu na uteule wetu, kwasababu shetani ni kama simba angurumaye.. 

1Petro 5:8 “Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.

9 Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kuwa mateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani.

 Ubarikiwe sana. Kwa mawasiliano/mafundisho zaidi kwa njia ya whatsapp, tutumie ujumbe kwenye
namba hizi: +255789001312/ +255693036618


Mada zinazoendana:

ANGUKO LA UFALME WA SHETANI:

KUZIMU NI MAHALI PA NAMNA GANI, JE! HUKO WANAISHI WATU WAKIFA NA KWENDA KUPATA MATESO AU NI VINGINEVYO?

JE! NI KWELI KUNA VIUMBE VINAVYOISHI SAYARI NYINGINE (ALIENS)?

TULICHUNGUZE UMBO LA YESU NA MWENENDO WAKE.

JE! MBINGUNI KUNA MALAIKA WA KIKE?. NA JE! TUKIFIKA MBINGUNI TUTAFANANA WOTE? 

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Leave a Reply