KUZIMU ni mahali pa namna gani, Je! huko wanaishi watu wakifa na kwenda kupata mateso au ni vinginevyo?

KUZIMU ni mahali pa namna gani, Je! huko wanaishi watu wakifa na kwenda kupata mateso au ni vinginevyo?

JIBU: Kuzimu ipo, na ni sehemu iliyo halisi kabisa biblia inaelezea katika (Luka 16:19-31)… Mtu anapokufa katika dhambi (yaani haujaoshwa dhambi zake kwa damu ya YESU KRISTO)..mtu anaenda moja kwa moja kuzimu/jehanum, huko kuna mateso mengi sana, mtu huyo atakaa huko akingojea ufufuo wa wafu, ambao utakuja baada ya ule utawala wa YESU KRISTO wa miaka 1000 kuisha ambapo wafu wote watafufuliwa na kuhukumiwa mbele ya kile kiti cheupe cha Hukumu..  

Ufunuo 20:12 “Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.

13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.

14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto.

15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto”.  

Ukisoma pia Yohana 5:28 BWANA YESU aliyasema maneno hayo..

“Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. 29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.”  

Unaona wale wanaotenda mabaya wote watafufuliwa kwa ufufuo wa hukumu, hivyo baada ya kuhukumiwa kulingana na matendo yao ndipo watakapotupwa kwenye lile ZIWA LA MOTO atakapokuwepo shetani na malaika zake, lenye mateso mengi kuliko jehanum. ni kama tu vile mtu anapokamatwa na hatia anawekwa kwanza mahabusu kwa muda fulani akisubiria kupandishwa mahakamani, sasa akishahukumiwa mahakamani kulingana na makosa yake ndipo anapopelekwa magereza kutumikia makosa yake. na ndivyo itakavyokuwa kwa waovu wote walioikataa neema ya msalaba wa Bwana YESU KRISTO watakapokufa sasa hivi wataenda kuzimu kwenye vifungo na mateso, wakingojea hukumu ya mwanakondoo kisha baadaye watatupwa kwenye lile ziwa la moto.

Lakini wanaokufa sasa katika haki, wanapelekwa mahali panapoitwa “Paradiso” . Paradiso ni mahali panapofanana na mbinguni,lakini sio mbinguni, ni mahali pa raha, wanawekwa humo kwa muda fulani wakingojea ufufuo wa wenye haki, atakapokuja Bwana mawinguni, watafufuliwa na kuvaa miili ya utukufu na kuungana na watakatifu walio hai na kwa pamoja kwenda na Bwana mbinguni kwenye karamu ya mwana kondoo.   Paradiso kwa jina lingine ni Peponi.

1 Wathesalonike 4: 15 “Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti.

16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.

17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.”  

Hivyo ndugu fahamu kuwa kuzimu ipo. Ni sehemu halisi kabisa.

Ubarikiwe sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

NI UTHIBITISHO UPI UNAOONYESHA KUWA KUNA MBINGUNI NA KUZIMU?

JE! NI KWELI KUNA VIUMBE VINAVYOISHI SAYARI NYINGINE (ALIENS)?

BWANA ALIMAANISHA NINI KUSEMA “WAACHE WAFU WAZIKE WAFU WAO.(MATHAYO 8:21)?

MTI UANGUKAPO, PAPO HAPO UTALALA.

MTI WA UZIMA NA MTI WA MAARIFA.


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Nelson bujenja
Nelson bujenja
2 years ago

Amen nmebarikiwa sana

Rowland asante Robert
Rowland asante Robert
3 years ago

Shalom…naomba kuuliza Biblia inaposema kuwa makabuli yatawatoa wafu, vivyo hivyo bahari, je hawa watakao toka/fufuliwa makabulini ni watu gani ikiwa mtu akifa anaenda mbinguni au jehanam?