SWALI: Bwana akubariki ndugu yangu wa thamani . Naomba kujua kwa namna Bwana alivyokujalia kujua juu ya hawa viumbe kutoka katika sayari ya Mars kama sikosei wanaiotwa ALIENS je ni kweli wapo ?au ni elimu ya dunia (sayansi ) inayoidanganya ulimwengu?.
JIBU: Ubarikiwe sana kwa swali zuri ndugu, Ukweli ni kwamba hakuna viumbe vingine vinavyoishi katika ulimwengu (Universe) zaidi ya wanadamu, Biblia haijasema kama kuna viumbe wengine tofauti na wanadamu na wanyama. Hadithi ya huu ulimwengu inamuhusu Mwanadamu na Muumba wake basii!! Inahusu ni jinsi gani Mungu alivyomuumba Mwanadamu na kumpa mamlaka juu ya vitu vyote chini yake, vilivyopo ulimwenguni…
Kwahiyo hakuna kiumbe kingine chochote kilicho na akili zaidi ya mwadamu kinachoishi ulimwenguni wa mbali, kumbuka tunapozungumzia ulimwengu hatuzungumzii tu dunia tunayoishi peke yake hapana bali tunazungumzia sayari zote na magimba yote yaliyopo angani, na kila mahali ambapo upeo wa mwanadamu unaweza kufika kote huko ni ulimwenguni, na hakuna kiumbe kingine chochote kinachoishi katika ulimwengu chenye kumzidi mwanadamu akili…
Zaburi 8: 3 “Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, Mwezi na nyota ulizoziratibisha;4 Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie?5 Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima;6 Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.7 Kondoo, na ng’ombe wote pia; Naam, na wanyama wa kondeni;8 Ndege wa angani, na samaki wa baharini; Na kila kipitacho njia za baharini.9 Wewe, MUNGU, Bwana wetu, Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!”
Zaburi 8: 3 “Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, Mwezi na nyota ulizoziratibisha;
4 Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie?5 Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima;
6 Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.
7 Kondoo, na ng’ombe wote pia; Naam, na wanyama wa kondeni;
8 Ndege wa angani, na samaki wa baharini; Na kila kipitacho njia za baharini.
9 Wewe, MUNGU, Bwana wetu, Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!”
Sasa utauliza kama hakuna viumbe wengine wenye akili kuliko mwanadamu wanaoishi huko angani na kwenye masayari mengine…ni nini basi viumbe hivi wanasayansi wanavyoviona na kuvipiga picha huko angani vinavyofanana na watu?.
Ni ukweli usiopingika kwamba wana-sayansi kuna vitu wanaviona angani, na wakati mwingine wanafanikiwa kuvipiga picha, na wakati mwingine wanaona vinawapa ujumbe Fulani kwa ishara, na wakati mwingine vinatokea tu kwa mfano wa mwanga Fulani na kutoweka, na kuwabakisha katika maswali mengi. Na kwasababu Sayansi kwa sehemu kubwa haiamini kama kuna Mungu hivyo wana-sayansi hawa wanaishia kutafuta kujua ni nini hasa wanavyoviona au kuvipiga picha.
Sasa hivi viumbe (Ambavyo wana-sayansi wanaviiita ALIENS) ni wakina nani?..Jibu la swali hilo tunaweza kulipata katika mstari ufuatao.
Ufunuo 12: 7 “Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye”.
Ufunuo 12: 7 “Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;
8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye”.
Kwahiyo viumbe hawa wanasayansi wanaoviona huko angani ni shetani na majeshi yake (mapepo).Na kwasababu shetani naye ana akili, kama biblia inasema ana uwezo wa kujigeuza na kuwa mfano wa malaika wa Nuru, hivyo anachokifanya yeye na malaika wake walioasi (yaani mapepo) ni kujigeuza na kujifanya kuwa ni viumbe wengine wenye akili sana wanaotokea sayari za mbali, na wanawatokea baadhi ya watu tu! Wale wenye kuamini mambo hayo, na lengo lake Shetani ni lile lile KUDANGANYA WANADAMU. Kuwatoa wanadamu katika kuamini kuwa kuna Mungu na kuwafanya waamini kuna viumbe wengine wanaoishi sayari za mbali wenye akili nyingi zinazowazidi wao…Hivyo wanaweza kuwatumainia wao kuwaletea msaada na utatuzi wa mambo yao ya kiteknolojia na kijamii…
Ni kama vile MASIHI wao wanamngojea. Kumbuka shetani ana vitengo vingi vya kuwapotosha wanadamu, anatumia uchawi kuwapotosha wale watu wanaoamini kuna uchawi, anatumia manabii wa uongo na waalimu wauongo kuwapotosha wale wanaokwenda kanisani wasioamini katika uchawi bali Mungu…na anatumia uongo wa Ma-ALLIENS Kuwadanganya wale watu wasioamini kuwa kuna Mungu, ili waendelee kuamini hivyo hivyo kuwa hakuna Mungu bali kuna viumbe wengine huko angani. Kazi yake ni kuwa akishagundua unapenda nini na upo wapi, anakutafutia upotoshaji katika hicho hicho kitu unachokipenda.
Nimewahi kusoma ushuhuda mmoja, mwanamke mmoja ambaye alikuwa ndio amempa Kristo maisha yake ila hajasimama vizuri, anasema alikuwa anapenda sana kusoma habari za ma-Alliens, na moyoni mwake alikuwa ameshaanza kuamini na kushawishika kuwa kwa namna moja au nyingine ni lazima kutakuwepo na viumbe wengine tofauti na wanadamu wanaoishi mojawapo ya zile sayari kule juu, sasa wakati akiwa katika uchunguzi wake akitamani sana siku moja awaone..maana alisikia shuhuda nyingi mbali mbali kuwa watu wamewaona na wengine wametokewa…anasema siku moja wakati anaendesha gari lake usiku wakati yupo njiani anarejea nyumbani..ghafla mbele ya barabara mbali kidogo akaona kitu kama mwanga Fulani mzuri sana alivyozidi kutazama aliona kile kitu kikakaribia mpaka pale gari lake lilipo na akafunga breki anasema hicho kitu kilikuwa kama ndege Fulani mfano wa kisahani hivi (spaceship).
Na alipokiona ni kama kilikuwa kimetengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu, ambayo duniani kwasasa haipo. Na vile viumbe vilivyomo mule ndani hakuviona isipokuwa alisikia tu sauti ikizungumza na yeye ndani yake ikimwambia wao ni viumbe kutoka sayari ya mbali wamekuja kuusaidia ulimwengu..Huyo dada anasema ndani ya moyo wake akafurahi sana akahisi kama ndoto yake imetimia ya kuwaona Ma-Aliens…Lakini kipindi kifupi nyuma alisikia injili na kuamua kumfuata Bwana Yesu, lakini alikuwa mguu mmoja nje mwingine ndani..
Hivyo akajikuta tu anawauliza swali hao viumbe..akawauliza “huko mlipo mnamwabudu Yesu?”..havikujibu, alipozidi kuviuliza hilo swali ndipo vikamjibu na kumwambia “sisi hatumwabudu Yesu nyinyi wanadamu ndio mnaomwabudu, sisi sio wanadamu”..wakati anaendelea kuwauliza wao wanamwabudu nani hicho chombo chao kikaondoka mbele yake..Baadaye, anasema kutoka na mwanga ule aliouna ulianza kumletea shida kila alipokuwa anasoma biblia alikuwa anaona mwanga tu, haoni chochote, lakini siku alipokuja kuombewa na hizo roho kumtoka ndipo akaja kufahamu kuwa alichokiona sio ma Aliens kama alivyokuwa anafikiri bali ni mapepo yaliyojigeuza na kujifanya kuwa ni ma aliens. Kwahiyo kwa kuhitimisha, elimu ya ma-ALIENS ni elimu ya shetani kabisa, iliyotengenezwa kuzimu kwa lengo na nia ya kuwapoteza watu wasiamini kuhusu Mungu bali waamini utafiti wa kisayansi juu ya uwepo wa viumbe wengine zaidi ya wanadamu. Na jambo hili limewaathiri sana watu wa Ulaya, huku kwetu ndio nalo linaanza kukita mizizi.
Ubarikiwe.
Mada Nyinginezo:
HUDUMU YA MALAIKA WATAKATIFU.
MIHURI SABA
KUNDI LA MALAIKA WALETAO MABAYA.
HUDUMA YA UPATANISHO.
ROHO YA MPINGA KRISTO IKITENDA KAZI SIKU HIZI ZA MWISHO.
MVUTO WA TATU!
Rudi Nyumbani:
Print this post
Nashukuru kwakunifumbua
Nimefurahi Sana kuujua ukweli huu maana tumekua tukisikia habari hizi za aliens lakini ukweli wake katika biblia hatuuoni lakini kupitia somo hili binafsi nimebarikiwa sana na MUNGU wa mbinguni awabariki Sana
Amen ubarikiwe pia
Amen nimefurah Sana kuujua ukweli kuhusu ili somo LA hawa ma aliens mana nlshaskia watu wakisema dalili za kuja Kwa Yesu kna ishara za viumbe hawa znaonekana huko ulaya kumbe ni ujanja wa shetani kuendelea kuudanganya ulimwengu nyakati hizi za mwisho.Mungu azidi kuwabariki Sana mashujaa .Tukiwa ndani ya Kristo tutaifahamu kweli na kweli itatuweka huru
Kuna udanganyifu mwingi upo duniani kwasasa, hivyo ni kuwa macho tu, katika utulivu wa Roho huku tukifunza Neno la Mungu kwa bidii.