Biblia inaposema kwamba “kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo lakini utauwa wafaa kwa mambo yote..inamaana gani”? (1Timotheo 4:8).

Biblia inaposema kwamba “kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo lakini utauwa wafaa kwa mambo yote..inamaana gani”? (1Timotheo 4:8).

JIBU: Kama ukisoma vifungu vya juu katika hiyo habari utaona, ni kuwa kulikuwa na baadhi ya watu wanawashurutisha watu kwa kuwaambia kushika mambo ya mwilini ndio bora na kunafaa kwa uzima wa mtu, kwa mfano kuzingatia aina Fulani ya vyakula, kwamba usile kambale, au usile nguruwe, au ni lazima utahiriwe unapozaliwa, au ni lazima unawe mikono pale unapokula, au kutawadha, au ni lazima mtu afanye mazoezi ya mwili, au mtu ili awe mtakatifu ni lazima mtu asioe,… n.k…   Na huku wamesahau au wamepuuzia kabisa mambo ya muhimu ya rohoni yaani kumcha MUNGU na utakatifu wa roho zao….  

Na ndio hapa Paulo anamwambia Timotheo Ni kweli kwa namna moja au nyingine vinaweza vikampa mtu uzima wa mwili wake, na afya njema, hapa duniani lakini haviwezi kumpa uzima huko anapokwenda…Vitu kama hivyo haviwezi kumpa mtu daraja la moja kwa moja kwenda mbinguni, haviwezi kuzuia vitu kama tamaa za mwili n.k.

Wakolosai 2:20 “Basi ikiwa mlikufa pamoja na Kristo mkayaacha yale mafundisho ya awali ya ulimwengu, kwa nini kujitia chini ya amri, kama wenye kuishi duniani,

21 Msishike, msionje, msiguse;

22 (mambo hayo yote huharibika wakati wa kutumiwa); hali mkifuata maagizo na mafundisho ya wanadamu?

23 Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kunyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali; LAKINI HAYAFAI KITU KWA KUZIZUIA TAMAA ZA MWILI”.  

Unaona?. Na ndio maana Paulo anamshauri Timotheo jambo jema la kuchagua…Nalo ni Utauwa, (Utakatifu), kuwa mtu wa rohoni, au kwa namna nyingine ni KUWA NA HOFU YA MUNGU ambalo hilo tu ndio linaweza kuyadhibiti mambo yote ya mwilini na rohoni….Ukiwa na hofu ya Mungu, ukimcha Mungu hata usipozingatia mlo kamili, bado Mungu atakulinda tu na kukupa afya, na bado juu yake utakuwa na ahadi ya uzima wa milele..Tofauti na Yule mtu anayezingatia lishe bora na huku maisha yake ya rohoni yapo chini, anaweza kweli akapata afya njema, na mwonekano mzurimkwa kitambo tu lakini siku akifa atakuwa wapi kama moyo wake ni mchafu..  

Unaweza ukawa umehangaika kujipatia mali ili uwe na maisha bora hapa duniani, ni kweli hapo ni sawa na umejipatia nguvu za mwilini, kwani mali ni ulinzi, zinaweza kukulinda kwa sehemu Fulani, lakini roho yako haiwezi kulindwa na mali…lakini ukiwa ni mtu wa rohoni, mtauwa, mtakatifu, unayemcha Mungu, unayeyajua maandiko, anayezijua ahadi za Mungu, analisimama imara katika Imani,..Mali ameahidiwa kuzipata halikadhalika uhakika kwa maisha ya milele upo. Sasa Kwanini na sisi tusichague fungu hilo?

1Timotheo 4:8 “Kwa maana kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, lakini utauwa hufaa kwa mambo yote; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye.

Hivyo tusipoteze muda mwingi kwa vitu vya muda tu, bali tujishuhulishe zaidi na vile vitakavyotusaidia kwa mambo yote..Hiyo ni hesabu rahisi sana na inayoeleweka.

Ubarikiwe.


Mada Nyinginezo:

NITAONGEZAJE NGUVU ZANGU ZA ROHONI?

MAJARIBU MATATU YA YESU KRISTO

ROHO ZILIZO CHINI YA MADHABAHU:

UTHABITI WA AGANO LA MUNGU KWA MKRISTO.

ALAMA KATIKA VIPAJI VYA NYUSO.

MIISHO YA ZAMANI.


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments