Je! mtu anapofunga kwa muda wa SAA 24,anapaswa kunywa maji au kitu chochote?

Je! mtu anapofunga kwa muda wa SAA 24,anapaswa kunywa maji au kitu chochote?

JIBU: Biblia haijatoa masharti yoyote ya kufuata katika kufunga kwamba ufunge masaa 12 au 26 au 36 au mwezi,nk.. hapana. Kwasababu kitendo chenyewe cha kufunga ni kitendo kinachotoka rohoni na sio mwilini. Hivyo kwa jinsi mtu atakavyoguswa moyoni au atakapoona yeye mwenyewe umuhimu wa kufunga kwa muda fulani, pengine kutokana na ugumu wa hali fulani anayopitia kiroho ama haja fulani anataka kupeleka kwa Mungu, ndipo anapolazimika kujichagulia mwenyewe aina ya ufungaji wake utakaoendana na haja zake, (isipokuwa labda awe ameagizwa na Mungu mwenyewe aina ya mfungo anaopaswa afunge).   Mfano tunaweza tukamwona mtu kama Danieli ukisoma katika

Danieli 10: 1 “Katika mwaka wa tatu wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, Danielii, ambaye jina lake aliitwa Belteshaza, alifunuliwa neno; na neno lile lilikuwa kweli; maana ni vita vikubwa; naye akalifahamu neno lile, akaelewa na maono hayo.

2 Katika siku zile mimi, Danielii, nalikuwa nikiomboleza muda wa majuma matatu kamili.

3 SIKULA CHAKULA KITAMU, WALA NYAMA WALA DIVAI HAIKUINGIA KINYWANI MWANGU,WALA SIKUJIPAKA MAFUTA KABISA, hata majuma matatu kamili yalipotimia”.  

Hivyo kulingana na habari hiyo Danieli kwa kuona vita kubwa mbele yake na kutaka kufahamu mambo gani yatakayokuja kutokea huko mbeleni, ikamlazimu afunge wiki tatu, pasipo kula chakula kitamu wala kujipaka mafuta, Kadhalika na Musa, kwa kuwa alifahamu anakwenda kukutana na uso wa Mungu na kupokea amri za Mungu kule mlimani ilimlazimu afunge siku 40 usiku na mchana bila kula chochote, Pia wakati wa Esta wayahudi walipoona wanapitia hatari ya kuuawa walifunga siku tatu usiku na mchana bila kula chochote, kadhalika na wengine mfano Nehemia, Daudi, Mitume Pamoja na Bwana wetu YESU KRISTO hata yeye wakati wa kwenda kujaribiwa na shetani nyikani alifunga siku 40 usiku na mchana bila kula wala kunywa chochote. n.k.  

Hivyo unaona hapo inategemea na sababu ya mtu kuingia katika mfungo huo, ndio kinachopelekea aina ya kujinyima nafsi. wapo watu wengine wanafunga saa 24 au zaidi kwa kunywa maji tu pasipo chakula na wanaweza kwenda hivyo kwa siku tatu au zaidi,.Wapo wengine wanaweza kufunga pasipo kula chakula wala maji kwa siku kadhaa, wapo wengine wanafunga kwa kutokula chakula walichokizoea, mfano walikuwa wanakula nyama mara mbili kwa siku, wanaamua kujinyima kwa kutokula chakula kitamu kama nyama kwa muda wa labda mwezi mmoja hivi au zaidi wanakuwa wanakula tu pengine maji na mkate basi.n.k.   Vyovyote vile nawe ukiamua kufunga kwa kutokunywa maji saa 24, au kwa kunywa maji tu katika ufungaji wako wote, ni uamuzi wako, lakini kumbuka kwa jinsi unavyojinyima zaidi ndivyo unavyoongeza nguvu zako za kiroho, Biblia inaonyesha wengi walikuwa wanafunga pasipo kula wala kunywa kwa kiwango cha chini ni saa 12 (yaani jua linapochomoza mpaka linapozama). Hivyo kufunga kokote kule utapata thawabu kama kama ukizingatia yale Bwana aliyosema katika Mathayo 6:16.  

Hivyo unapofunga kumbuka kuzingatia pia viwango vya rohoni kama usafi, utakatifu,(kwa kujitenga na dhambi) n.k. vinginevyo mfungo wako utakuwa ni sawa na bure kama wapagani wanavyofanya, Kwa kulijua hilo zaidi soma mistari ifuatayo. Bwana akiwaambiwa watu wake;  

Isaya 58:3 ” Husema, Mbona tumefunga, lakini huoni? Mbona tumejitaabisha nafsi zetu, lakini huangalii? Fahamuni, siku ya kufunga kwenu mnatafuta anasa zenu wenyewe, na kuwalemea wote watendao kazi kwenu.

4 Tazama, ninyi mwafunga mpate kushindana na kugombana, na kupiga kwa ngumi ya uovu. Hamfungi siku hii ya leo hata kuisikizisha sauti yenu juu,

5 Je! Kufunga namna hii ni saumu niliyoichagua mimi? Je! Ni siku ya mtu kujitaabisha nafsi yake? Ni kuinama kichwa kama unyasi, na kutanda nguo za magunia na majivu chini yake? Je! Utasema ni siku ya kufunga, na ya kukubaliwa na Bwana?

6 Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira?

7 Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe?

8 Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa Bwana utakufuata nyuma ukulinde.

9 Ndipo utaita, na Bwana ataitika; utalia, naye atasema, Mimi hapa. Kama ukiiondoa nira; isiwepo kati yako, wala kunyosha kidole, wala kunena maovu;

10 na kama ukimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi yako, na kuishibisha nafsi iliyoteswa; ndipo nuru yako itakapopambazuka gizani; na kiwi chako kitakuwa kama adhuhuri.

11 Naye Bwana atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui.

12 Na watu wako watapajenga mahali palipokuwa ukiwa; utaiinua misingi ya vizazi vingi; nawe utaitwa, Mwenye kutengeneza mahali palipobomoka; na, Mwenye kurejeza njia za kukalia.

13 Kama ukigeuza mguu wako usihalifu sabato, usifanye anasa yako siku ya utakatifu wangu; ukiita sabato siku ya furaha, na siku takatifu ya Bwana yenye heshima; ukiitukuza, kwa kutokuzifanya njia zako mwenyewe, wala kuyatafuta yakupendezayo, wala kusema maneno yako mwenyewe;

14 ndipo utakapojifurahisha katika Bwana; nami nitakupandisha mahali pa nchi palipoinuka; nitakulisha urithi wa Yakobo baba yako; kwa maana kinywa cha Bwana kimenena hayo.  

Ubarikiwe sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

NJIA SAHIHI YA KUFUNGA.

BWANA YESU ALIKUWA ANAMAANISHA NINI KUSEMA MARKO 2:19″WALIOALIKWA HARUSINI WAWEZAJE KUFUNGA MAADAMU BWANA-ARUSI YUPO PAMOJA NAO?”

MUNGU NDIYE ANAYEISHAWISHI MIOYO.

NINI MAANA YA HUU MSTARI ” NIMEVIPIGA VITA VILIVYO VIZURI, MWENDO NIMEUMALIZA, IMANI NIMEILINDA;”?(2TIMOTHEO 4:7)

MWE NA HASIRA, ILA MSITENDE DHAMBI.

SIKUKUU 7 ZA KIYAHUDI ZINAFUNUA NINI KWETU?


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
9 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
1 year ago

Tuu pamoja katika Imani Bwana Yesu Akubariki sawa sawa na Zaburi 20:1-9

Minia
Minia
1 year ago

Amina, Ubarikiwe Mtumishi

Gesbon mwandelile
Gesbon mwandelile
2 years ago

Amina mtumishi naomba kuuliza eti mfungo unaanza saanga mpk mda gani wa kufungua

Anonymous
Anonymous
1 year ago

Alafu kuna mwandelile amanifundisha hisabat alikuwa ana nikong’oa kichwa kama sielewi, ila huyu mtumishi ameeleza, rudia maandishi utaelewa mtumishi, barikiwa amem

Grace
Grace
2 years ago

Ameen be blessed mtumishi nimejifunza kitu kuhusu kufunga

Herry Nziku
Herry Nziku
2 years ago

Asante sana

Glorry Joseph
Glorry Joseph
2 years ago

Amen nimejifunza sana kuhusu kufunga ubarkiwe mtumish