Kulingana na 1Wakorintho 3:10-15, kama inavyosema..ni kwa namna gani kazi ya mtu itateketea, na kupimwa kwa moto?”

Kulingana na 1Wakorintho 3:10-15, kama inavyosema..ni kwa namna gani kazi ya mtu itateketea, na kupimwa kwa moto?”

1Wakorintho 3:10-15 Inasema..

10 Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima, naliuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini kila mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake.

11 Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu Kristo.

12 Lakini kama mtu akijenga juu ya msingi huo, dhahabu au fedha au mawe ya thamani, au miti au majani au manyasi, kazi ya kila mtu itakuwa dhahiri.

13 Maana siku ile itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto wenyewe utaijaribu kazi ya kila mtu, ni ya namna gani.

14 Kazi ya mtu aliyoijenga juu yake ikikaa, atapata thawabu.

15 Kazi ya mtu ikiteketea, atapata hasara; ila yeye mwenyewe ataokolewa; lakini ni kama kwa moto.

16 Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?”

JIBU: Kwanza ni muhimu kufahamu kuwa wanaozungumziwa hapo ni watenda kazi (yaani watu wote wanaojiita watumishi wa Mungu), na kila mtu anapofanya kazi ya kuhubiri na kuwavuta watu kwa Kristo ni sawa na kama anajenga nyumba yake mwenyewe ya mbinguni. Kwahiyo wale watu anaowazaa kwa injili yake hiyo ndio kazi yake na ndio itakayojaribiwa kwa moto. Sasa moto ni nini, na unaijaribuje kazi ya mtu?.

Moto ni majaribu ya imani, misukosuko, adha, dhiki, au mateso shetani atakayoyaleta juu ya watu wako uliowazaa katika kazi ya kuhubiri injili.

Kwahiyo kama wale watoto wako uliowaowazaa uliwakuza katika mafundisho madhaifu wasiyowafanya wawe imara, itakapokuja dhiki, au misukosuko,au majaribu, watashindwa kusimama na mwisho wa siku wataanguka na kuteketea na kupotea kabisa. Hivyo katika siku ile Kazi yake mtu huyo itaonekana kama ni ya hasara kwasababu watu aliowazaa wote wameteketea na moto(majaribu misukosuko n.k.), Kwa mfano unakuta muhubiri injili yake siku zote imejikita katika mafanikio ya kimwilini tu,haweki mambo katika usawa hafundishi watoto wake kumjua Mungu zaidi na utakatifu na uweza wa Mungu na iMANI,na Upendo wa Mungu au mambo yahusuyo ufalme wa mbinguni, yeye mafundisho yake ni mafanikio tu ya kimwilini basi na mtumishi huyo utakuta yupo na maelfu ya wafuasi anawalea chini yake,

Sasa kipindi kitakapofika shetani naye atataka kuwajaribu wale watoto aliowazaa,..atawaletea aidha mtikisiko wa kiuchumi kidogo tu, au magonjwa, au vifungo, au wakati mwingine mafanikio makubwa kupita kiasi ili apunguze muda wake na Mungu ajikite katika mambo ya kidunia n.k. sasa kwasababu wale watoto hawakufundishwa uvumilivu, saburi na Imani, kiasi n.k.. haraka sana wataiacha ile Imani na kurudi nyuma. Na ndio hao wanafananishwa na zile mbegu zilizodondokea nyingine njiani, ndege wakapita wakazila, nyingine kwenye miamba zikakosa mizizi na kufa(Hawa ndio wale wakati wa kujaribiwa wanajitenga na Imani), wengine kwenye miiba(shughuli na udanganyifu wa mali vinawasonga, wanakuwa hawazai chochote) n.k.. Kwa namna hiyo basi safari yao ya Imani wanajikuta imeishia ukingoni. 

Hivyo kazi ya yule muhubiri mwisho wa siku yote aliyojisumbukia yanakuwa ni hasara tupu kwasababu hakuijenga nyumba yake(kondoo wake) katika ubora unaotakiwa… Kadhalika biblia inaposema yeye naye ataokoka lakini kana kwamba kwa moto, inamaanisha pia na yeye atapitia majaribu yale yale, na kama akiweza kuyastahimili yeye ataokoka lakini kazi yake itakuwa ni ya hasara, atakuwa kama mtu tu ambaye hajawahi kumtumikia Mungu kwa namna yoyote ile.

 Kwahiyo habari hiyo inatufundisha kuwa tufanye kazi ya Mungu kwa malengo, tukijua ya kuwa kazi zetu zitaenda kupimwa siku ile. Itatufaidia nini tupate maelfu wa washirika katika makusanyiko yetu kwasababu tu tunawahubiria injili laini, na siku ile tunakwenda kuonekana hatufanya chochote?. Ni heri awepo mmoja lakini chombo cha thamani chenye kumfaa Mungu kilichojengwa kwa dhahabu.kuliko kuwa na mabunda ya nyasi.

Hivyo Tusihubiri tu ilimradi kuwaburudisha washirika ili washirika waendelee kukaa katika makusanyiko yetu, hapana bali tuwajenge wawe kama mawe ya thamani ambayo moto utakapokuja kuyajaribu ndio yanazidi kuwa imara badala ya kuwa dhaifu. 

Ubarikiwe sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

UBATIZO WA MOTO

JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?

JE! HIZI ROHO SABA ZA MUNGU NI ZIPI? NA JE ZINATOFAUTIANA NA ROHO MTAKATIFU?

ROHO MBAYA KUTOKA KWA BWANA.

UPUMBAVU WA MUNGU.

IMANI NI KAMA MOTO.


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments