Kwanini kuna watu wanafanyiwa deliverance (Maombi ya kufunguliwa), lakini baada ya muda wanarudiwa tena na hali ile ile sababu ni nini?

Kwanini kuna watu wanafanyiwa deliverance (Maombi ya kufunguliwa), lakini baada ya muda wanarudiwa tena na hali ile ile sababu ni nini?

JIBU: Tunakosa maarifa tukidhani kuwa tunapowaombea watu maombi ya kufunguliwa kwa mfano kutoa Pepo.Ni kwamba tunawatoa kweli wale Pepo na hapo hapo mtu yule anakuwa ameshafunguliwa, Hapana ukweli ni kwamba hatutoi pepo moja kwa moja bali tunakuwa TUNAWAFUKUZA PEPO KWA MUDA TU wanakwenda mahali watakapokaa pale kwa kipindi fulani cha muda. Na baadaye wakisha tulia kwa muda,wana tabia ya kurudi kuangalia maskani zao za kwanza zikoje, Kwasababu kama ingekuwa ndio hivyo kirahisi rahisi tu Bwana asingesema tena maneno haya;  

Mathayo 12: 43 Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate.

44 Halafu husema, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija, aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa.

45 Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya.”  

Unaona? Watu wengi wanaosumbuliwa na vifungo vya shetani au mapepo, kwa kudhani kuwa mtumishi yule anapomwombea na pepo kulipuka ndio kafunguka moja kwa moja, hapana hiyo ni hatua ya kwanza ya yule pepo kukuacha, ila bado yupo na wewe, bado ana hati zote za kukumiliki wewe.

Hivyo kwa wakati ule mfupi baada ya kuombewa kwa Imani huyo Pepo ataondoka, na baada ya hapo utaanza kuona unafuu mkubwa katika maisha yako kwa kipindi kifupi tu cha wakati. Lakini yule pepo aliyefukuzwa hawezi kuiachia milki yake kirahisi hivyo anachofanya, ni kurudi kuona je! yule mtu analo badiliko lolote katika maisha yake?. Na kama asipoona ndio anakwenda kuchukua mapepo mengine saba maovu kuliko yeye (anafanya hivyo ili kwamba siku nyingine asisumbuliwe kutolewa kirahisi), na ndio unakuta yule mtu yale matatizo aliokuwa nayo kwanza yanarudi na kuzidi kuwa mengi, hali yake ya mwisho inakuwa mbaya kuliko ile ya kwanza.  

Zipo shuhuda nyingi ndio utasikia mtu anasema nilikwenda kuombewa na mtumishi fulani, nikapona ugonjwa uliokuwa unanisumbua pale pale lakini baada ya mwezi ile hali imenirudia tena, na safari hii ndio imekuwa mbaya zaidi kuliko hata ya mwanzo..Sasa wengi wa watu kama hawa hawajajua au hawajafundishwa utendaji kazi wa hizi roho ovu.  

Kumbuka KUFUNGULIWA kwa mtu, kunaanzana na yeye mwenyewe, ikiwa mtu hataki kufunguliwa basi hata aombeweje hawezi kufunguka. Kadhalika watu hawajui kuwa vipo vifungo/mapepo mengine ambayo hayajidhihirishi kwa nje(yaani hayalipuki) kama mapepo mengine yanavyofanya. yamekaa ndani tu,na mengine yanakuja ndani ya mtu na kuondoka, hivyo haya yote huwezi kuyatambua kwa kutegemea kusubiria uombewe. Ni lazima ufahamu mtu yoyote ambaye hajazaliwa mara ya pili (yaani kwa kumwamini YESU KRISTO na kubatizwa katika ubatizo sahihi) kwa namna moja au nyingine kuna roho au vifungo vya uovu vinaambatana naye hatakama yeye anajiona yupo sawa.  

Hivyo basi pepo linapofukuzwa ndani ya mtu, ni wakati wa mtu yule haraka sana kuchukua hatua ya kumkabidhi Bwana maisha yake yote kwa kumaanisha kuacha maisha ya dhambi na kubatizwa katika ubatizo sahihi na kupokea Roho Mtakatifu. Kwa kufanya hivyo atakuwa ameondoa hati miliki zote za pepo lile kurudi, na sio tu mapepo yale yanayojidhihirisha bali hata na yale yasiyojidhihirisha yanakuwa hayana nafasi ya kurudi na hivyo mtu yule anakuwa UMESHAFUNGUKA KIKABISA KABISA. Na ndio maana Bwana alipokwisha kuwafungua watu aliwaambia wasitende dhambi tena, maana ya kutokutenda dhambi ni kumwamini yeye (Bwana Yesu, kwa kutubu na kuzaliwa mara ya pili).   Hivyo deliverance ambayo itaweza kumfungua mtu MOJA KWA MOJA ni kuzaliwa mara ya pili, na sio kuombewa tu na pepo kulipuka halafu basi.  

Ubarikiwe sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

TOBA IGUSAYO MOYO WA BWANA.

FAIDA ZA MAOMBI.

UPONYAJI WA YESU.

VIFUNGO VYA GIZA VYA MILELE.

BABA YANGU ANATENDA KAZI HATA SASA!.

NGUVU ZA ZAMANI ZIJAZO:


Rudi Nyumbani:

 

 

 

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
5 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Simon mwiti mutie
Simon mwiti mutie
3 years ago

Barikiweni sana watumishi wa mungu na asila neema kutoka kwa mungu alie mbinguni kama vinye aliniasilia mimi

pastor mika omwamba
pastor mika omwamba
3 years ago

Leave your message nakusalimu bwana asifiwe Niko na upungufu kitogo kufusia Watoto kanisani ukiwesa usumame nami

Jackson.Temba
Jackson.Temba
3 years ago

Ev.Jackson.T.Temba
Nimefurahishwa na kujifunza somo zuri kuhusiana na kuvunja madhabahu bado nintaendelea kufuatilia makala zako kwa faida ya kuujenga Mwili wa Kristo
Pokea baraka kwa kuwafundisha watu kweli ya Mungu kwa usahihi