Kuna hukumu za aina ngapi?

Kuna hukumu za aina ngapi?

JIBU: Kulingana na biblia zinaonekana Hukumu kuu Nne za Mungu mwenyezi zitakazokuja mbeleni.. HUKUMU YA KWANZA:..Ni hukumu ya watakatifu watakaonyakuliwa kwenda mbinguni, hukumu hii siyo ya kulaumiwa wala ya adhabu, bali ni ya thawabu, kila mtakatifu atalipwa kulingana na taabu na Uaminifu wake aliokuwa nao katika kuifanya kazi ya injili akiwa hapa duniani,

 2 wakorintho 5:9-10 “Kwa hiyo, tena, ikiwa tupo hapa, au ikiwa hatupo hapa, twajitahidi kumpendeza yeye. Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya.”

Pia tukisoma warumi 14:12 biblia inasema; “Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu.” 

Tunajua nyaraka hizi mbili Paulo hakuziandika kwa watu wasioamini bali kwa wakristo kwahiyo hukumu hizi zinazozungumziwa hapa zinawahusu watakatifu tu ndipo taji la kila mtu litang’aa kulingana na kazi yake alipokuwa duniani. HUKUMU YA PILI: Hii itakuja baada ya ile siku kuu ya kutisha Bwana kupita, baada ya ile dhiki kuu, itawahusisha wale wakristo walioachwa katika unyakuo, ambao walikataa kuipokea ile chapa ya mnyama, na kuuliwa na mpinga kristo, sasa hawa nao watakufufuliwa tena, kulingana na..

Ufunuo 20: 4 “Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu.

5 Hao wafu waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu”.

 Hivyo wote watakaoikata chapa ya mnyama watafufuliwa na kuhukumiwa na wale watakatifu watakaokuja na Bwana siku ile, kisha baada ya kuhukumiwa nao pia watapewa neema ya kuingia katika ule utawala wa Amani wa Bwana Yesu Kristo wa miaka 1000.

Japo hawatakuwa daraja moja na wale watakatifu wa Mungu waliokuja na Bwana. HUKUMU YA TATU; hukumu hii pia itakakuwepo katikakati hapo, kati ya siku ile Bwana atakapokuja, na kabla ya utawala wa miaka 1000 kuanza, hii itakuwa kwa watu wote waliowafanyia fadhila watakatifu wa Mungu walipokuwa duniani,pamoja na wayahudi katika kile kipindi cha dhiki kuu, ndipo Kristo atakapowatenganisha kondoo na mbuzi…..

Tunasoma. 

Mathayo 25: 31 “Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake;

32 na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi;

33 atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto.34 Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu;

35 kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha;

36 nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia.

37 Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha?

38 Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika?

39 Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia?

40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.

41 Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;

42 kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe;

43 nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama.

44 Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie?

45 Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi.

46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele”.

 Kwahiyo hawa nao(Kondoo), watapewa neema ya kuingia katika utawala wa miaka 1000, Bali mbuzi (waovu), Watakwenda katika lile ziwa la moto.HUKUMU YA NNE:..Hii itakuwa baada ya ule utawala wa miaka 1000 kuisha pale Kristo atakapokaa katika kiti chake cha enzi cheupe kuwahukumu mataifa ukisoma 

Ufunuo 20:11“Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.

12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.” 

Hii itakuwa ni hukumu ya mataifa kwa wale wengine wote waliobakia na wale waliozaliwa ndani ya ule utawala wa miaka 1000 na wale ambao hawakuwa katika ule ufufuo wa kwanza, Na wale wote walioipokea ile chapa ya mnyama watahukumiwa wote kulingana na matendo yao na baada ya hapo wataingia katika lile ziwa la moto wale wote ambao majina yao hayakuonekana katika kitabu cha UZIMA. huko kutakuwako na kilio na kusaga meno. Kisha mbingu mpya na nchi mpya zitafuata, ambapo huko dhambi, wala hukumu havitakuwepo tena, wala mateso, wala uchungu, wala shetani, wala waovu, wala shida, wala magonjwa. Mambo ya kwanza yatakuwa yamepita Bwana atayafanya yote kuwa mapya katika ile Yerusalemu mpya itakayokuja.Na tutakuwa huko milele na milele na BWANA. Amina. 

Ubarikiwe sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

KUMWAMBIA MTU MWENYE DHAMBI KUWA ATAKWENDA KUZIMU ASIPOTUBU JE! NI KUHUKUMU?

JE NI KWELI TUTAWAHUKUMU MALAIKA? SAWASAWA NA 1WAKORINTHO 6:2

UFUFUO WA UZIMA NA WA HUKUMU.

KITABU CHA UZIMA

KITABU CHA UKUMBUSHO


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments