Je! Ni sahihi mtu kubatizwa kwenye maji ya KISIMANI?

Je! Ni sahihi mtu kubatizwa kwenye maji ya KISIMANI?

JIBU: Kwanza ni muhimu kufahamu maana ya hili neno UBATIZO.Hili ni neno la kiyunani lijulikanalo kama (BAPTIZO), lenye maana ya”KUZAMISHWA”. Kwahiyo kama tafsiri ya jina lake ilivyo, mtu anapobatizwa ni lazima azamishwe mwili wake wote katika maji, Na kumbuka haisemi ni katika mto, bahari, ziwa, au kisima, n.k. La! Maagizo yametolewa ni kuzamishwa.  

Kwahiyo Hakuna tatizo lolote mtu kubatizwa/kuzamishwa kisimani, ili mradi tu, maji yawe mengi ya kuweza kumzamisha mwili wote, hivyo iwe kwenye mto, kisima, chemchemu, pipa au baharini au kwenye dimbwi, popote pale la muhimu ni azamishwe mwili wote uzame usionekane na abatizwe kwa jina la Yesu Kristo. Ubatizo mwingine wowote tofauti na huo ni Batili. Hivyo Mtu huyo anapaswa akabatizwe tena.Kumbuka Nyakati za mtume Paulo kulikuwa na watu waliokuwa wanaujua ubatizo tu wa Yohana wa Toba, hawakuufahamu ubatizo uletao ondoleo la dhambi, Lakini Paulo alipowahubiria na kuamini wakabatizwa tena kwa ubatizo sahihi soma..  

Matendo 19: 1 “Ikawa, Apolo alipokuwa Korintho, Paulo, akiisha kupita kati ya nchi za juu, akafika Efeso; akakutana na wanafunzi kadha wa kadha huko;

2 akawauliza, Je! Mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia.

3 Akawauliza, Basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, Kwa ubatizo wa Yohana.

4 Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu.

5 Waliposikia haya WAKABATIZWA KWA JINA LA BWANA YESU.

6 Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri. 7 Na jumla yao walipata wanaume kumi na wawili.”  

Na wewe pia unaweza ukawa umebatizwa kwa ubatizo usio sahihi, hivyo usione aibu kwenda kubatizwa tena, ili kufanya imara wito wako na uteule wako.   Ni muhimu kufahamu kuwa hakuna ubatizo wa kunyinyuziwa kulingana na maandiko…Na ubatizo sahihi ni muhimu mno haupaswi kuupuziwa kwa namna yoyote ile. Kadhalika hakuna chuo chochote cha kupitia ndipo ukabatizwe, pale mtu tu anapoamini na kutubu kabisa kwa kumaanisha kuziacha dhambi zake moja kwa moja anapaswa aende akabatizwe kwa ajili ya ondoleo la dhambi zake na kupokea kipawa cha ROHO MTAKATIFU.  

Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? 38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu”.  

Ukipata muda pia pitia mistari hii ,( Matendo 8:16, 10:48).  

Ubarikiwe sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

MADHARA YA KUUPIZIA MAAGIZO YA MSINGI MUNGU ANAYOKUPA.

JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?

JE! UNAWEZA KUBATIZWA NA USIPOKEE ROHO MTAKATIFU?. NA JE! UNAWEZA KUPOKEA ROHO MTAKATIFU KWA KUWEKEWA MIKONO?

NI HALALI KUBATIZA WATOTO WADOGO?

MKUU WA GIZA.

UPONYAJI WA YESU.


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments