WOKOVU NI SASA

WOKOVU NI SASA

2Wakorintho 6:1 “Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msiipokee neema ya Mungu bure.

2 (Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia; tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa)”

Saa ya Wokovu ni sasa na sio kesho! Leo ndio wakati uliokubalika, dakika hii ndio wakati uliokubalika wa kupoekea Wokovu, usiseme kesho! Kwasababu kesho huwa inajipangia yenyewe mambo yake. Jambo ambalo wengi hawalijui ni kwamba Siku ndiyo inayotengeneza matukio na sio mtu anayetengeneza matukio ya siku.

Utapanga kesho ufue na kuanika nguo zako, lakini hiyo kesho mvua ikanyesha kubwa hata ikakuzuia wewe kufua. Umepanga kesho usafiri lakini hali ya hewa ikakuzuia. Umepanga kesho usafiri kwenda mashariki lakini ghafla ukajikuta unakwenda kusini kwenye mazishi.

Hivyo kesho si ya kuitumainia kabisa kwasababu imejaa mambo ya kushtukiza. Biblia inasema..

Mithali 27:1 “Usijisifu kwa ajili ya kesho; Kwa maana hujui yatakayozaliwa na siku moja”.

Na pia Bwana Yesu alisema.

Mathayo 6:34 “Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake”.

Hivyo hakuna Tarehe, wala Mwezi wala Mwaka uliopangwa kwa wokovu…SAA YA WOKOVU NI SASA! na WAKATI ULIOKUBALIKA NDIYO SASA, na SIKU YA  WOKOVU NI SASA.

Je! Umeokoka? na kama Bado unasubiri nini? Unajitumainisha na ya kesho? je wewe una hekima kulika Mungu anayekuambia kuwa usijisiu kwa ajili ya kesho? Hivyo ni kama hujampa Yesu Kristo maisha yako, na Roho Mtakatifu anaugua ndani yako sasa juu ya dhambi zako. Usikawie, hapo ulipo piga magoti, nyosha mikono yako juu!. Tubu kwa kumaanisha kabisa kuhitaji rehema kutoka kwa Bwana.

Bwana anakuona moyo wako naye atakuokoa sasa! kwasababu amesema mwenyewe saa ya wokovu ni sasa! Hivyo leo leo utakuwa umeokoka kama umedhamiria kutubu!

Sema Bwana Yesu!, ninakuja mbele zako. Mimi ni mwenye dhambi! naomba unisamehe dhambi zangu zote, Naahidi kutokuzifanya tena! Nisaidide Bwana. Niondoe kutoka katika mstari wa wanaokwenda Jehanamu  niingize katika orodha ya wanaokwenda mbinguni. Nipe moyo safi leo! naomba Roho wako Mtakatifu aingie ndani yangu sasa! niwe Mtakatifu. Nakiri kwamba wewe ndiye Mwokozi wangu, na Bwana wangu na Mungu wangu, katika Jina la Yesu.

Amen

Kama umefuatiliza sala hiyo. Basi umeshaokoka sasa! katika saa hii hii, kwasababu yeye anasema “Wakati uliokubalika nalikusikia“. Hivyo ameshakusikia. Kwahiyo sasa Chukua hatua ya kiimani kutafuta kanisa la kiroho ambalo utaweza kubatizwa ubatizo sahihi wa maji tele na kwa jina la Yesu kama hujabatizwa! Hiyo yote ni ili kuutia muhuri wokovu ambao umeshaupata moyoni mwako leo.

Kama utapata shida katika kutafuta kanisa, unaweza kuwasiliana nasi tutakusaidia kukuelekeza kanisa karibu na mahali ulipo ambapo utaweza kupata huduma hiyo ya ubatizo na ya kufanya ushirika na watu wenye Imani moja na wewe. Tutumie ujumbe mfupi kwa kupitia namba hizi 0789001312.

Bwana akubariki. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

Nini tofauti ya haya maneno. 1) KUOKOKA, 2) WOKOVU, 3) KUONGOKA.?

UNATAKA KUBARIKIWA? BASI USIKWEPE GHARAMA ZAKE.

PENGINE MUNGU ALISHASEMA NAWE KWA NJIA HII.

Wenye kubatizwa kwa ajili ya wafu ni wakina nani?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments