Nifanyeje niwe mwombaji mzuri, wa masafa marefu?

Nifanyeje niwe mwombaji mzuri, wa masafa marefu?

SWALI: Nifanyeje niwe mwombaji mzuri, wa masafa marefu na sio mtu wa kuomba omba tu, ilimradi?


JIBU: Katika vita lazima ujue adui wako mkuu ni nani.. Bwana Yesu alisema maneno haya;

Mathayo 26:40-41

[40]Akawajia wale wanafunzi, akawakuta wamelala, akamwambia Petro, Je! Hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja?

[41]Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.

Hapa  Bwana alitarajia, wakeshe, Yaani waombe naye masafa marefu, (kama vile wewe unavyotamani uwe na nguvu hata ya kukesha katika maombi mpaka asubuhi), lakini kinyume chake, hawakuweza kumaliza hata Saa moja..matumaini yao yaliishia katikati..

Lakini Bwana Yesu alipowakuta wamelala hakuwaambia kemea pepo hilo la uchovu, au wachawi hao waliotumwa kuwafanya mpige pige miayo ya usingizi, muda wote muombapo..

Bali aliwaambia maneno haya “ROHO I RADHI, LAKINI MWILI NI DHAIFU”..Akiwa na maana roho zao kweli zilikuwa zinatamani kukesha naye kule bustanini…na ndio maana walitii wito wa kwenda kuomba..kama roho zao zisingekuwa  radhi kufanya vile muda ule wangekuwa vitandani mwao wamelala..

Lakini Bwana anawaambia kikwazo ni nini.? Kikwazo ni MIILI yao.. Huyo ndio adui wao wa kwanza wanapaswa wamuangalie, sana

Tunashindwa kuomba, hata wakati mwingine kusoma Neno,..kwasababu ya mwili,..Lakini kama tukishindana na mwili ipasavyo basi tutaweza fungua milango mingi ya rohoni.

Sasa tutawezaje kuwa hivyo?

Ni kujitengenezea ”pumzi ya kiroho”..Kama vile wanariadha wafanyavyo katika mwili, kwa kawaida yule anayefanya mazoezi sana, huwa anajiongezea pumzi ya kukimbia umbali mrefu zaidi kuliko yule asiyefanya mazoezi yoyote, Atakimbia mzunguko mmoja tayari hoi.

Unapotaka uwe mwombaji mzuri, hata wa masafa marefu, ni lazima uanze kidogo kidogo, ukikumbuka kuwa adui wako wa kwanza sio shetani bali ni mwili wako..

Hivyo unaanza siku ya kwanza kuomba  dakika 15,  kesho huna budi kuongezea nyingine 5, kesho kutwa yake nyingine 5, hivyo hivyo, bila kurudi nyuma, Sasa kwa jinsi utakavyozidi kuongeza muda wako katika maombi ndivyo utakavyoona wepesi wa kuomba..

Kipindi cha mwanzoni utaona ni shida kumaliza saa moja katika maombi…lakini kama utakuwa ni mtu wa kuomba kila siku, utaona ni jepesi sana kama tu vile unavyoomba dakika 10..

Hautatumia nguvu kufikia huo muda, kwasababu tayari pumzi ya maombi ipo ndani yako.

Pengine jambo usilolijua ni kuwa wewe usiyeomba unaweza  kudhani yule anayeweza kukesha saa nyingi katika kuomba, anapata shida sana..lakini ukweli ni kwamba wewe ambaye unasali dakika chache, ndio unayechoka sana kuliko yule..kwasababu kuna kilele fulani mtu anayeomba  huwa anakifikia ile raha ya maombi inaingia ndani yake..wala haoni ugumu wa kuendelea mbele.

Hivyo jitahidi sana..Kushindana na mwili wako, ondoa mawazo yako sana kwa shetani, ni kweli upo wasaa ibilisi atataka kuvuruga ratiba zetu za maombi, lakini si jambo la kila siku…pindi unaposikia tu kuomba unalala, halafu unasema ni shetani…Ni huo mwili wako ndugu..

Anza leo kujizoeza kuomba. Shindana na usingizi, shindana na uchovu, shindana na uvivu.

Na hatimaye utakuwa mwombaji bora..Pia usingoje kuombewa, ombewa tu muda wote, vilevile usiseme Namwachia Mungu mwenyewe afanye, na ilihali hutaki kuomba..utapata hasara..Muda mwingine Kristo anasimama kutuombea..lakini wakati mwingine anataka kusimama na sisi kuomba, Kama alivyowaambia mitume wake hapo. Kesheni pamoja nami.

Mambo muhimu yatakayoweza kukupeleka rohoni haraka sana katika uombaji wako, Ni yapi?

  • Hakikisha kabla ya maombi..pata muda kidogo kukaa katika utulivu ukiwa umefunga macho..tafakari mambo yote mazuri, Mungu aliyokufanyia tangu utotoni mpaka hapo ulipofikia, kisha mpe shukrani, tafakari, uumbaji wa Mungu, tafakari, mbinguni siku ile utakapofika, tafakari mambo yote mazuri ya Mungu. N.k.
  • Pata muda tena wa kumsifu na kumwabudu kwa kinywa chako..imba nyimbo chache za shukrani na za kumtukuza Mungu.
  • Baada ya hapo mimina moyo wako mbele za Bwana, kwa kumwomba rehema na msamaha kwa makosa yako yote..

Kisha baada ya hapo ndio uingie moja kwa moja katika vipengele vyako vya maombi.

Zingatia hayo, na Mungu atakutia nguvu, katika hatua zako za maombi.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group

Mada Nyinginezo:

TUTAWEZAJE KUMZALIA MUNGU MATUNDA?

YAFUATAYO NI MAWAZO YA ADUI HIVYO USIYASIKILIZE.

JINSI YA KUSOMA BIBLIA.

Kuna tofauti gani kati ya SALA na DUA?

Marago ni nini? ( Waamuzi 10:18)

MFANO WA MAMBO HAYO NI UBATIZO.

Ijumaa kuu ni nini? Na kwanini iitwe kuu?

FANYIKA SIPORA WA KRISTO, UNYAKUO UPO KARIBU.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
5 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Golani
Golani
10 months ago

Mungu awabari kwa kazi nzuri mnaifanya kazi ya Mungu kwa kutii agizo lake la kuwafanya watu wote kuwa wanafunzi wa Yesu. Nabarikiwa sana na masomo yenu yananisaidia kukua kiroho

Prisca komba
Prisca komba
1 year ago

Amina nimekupa na Nitatendea kaz

FABIAN BAHARIA
FABIAN BAHARIA
1 year ago

Mimi natamani sana kuomba ila kila nilitaka kuomba kuna nguvu kubwa inapambana nami maeneo ya kichwani na kifuani kiasi kwamba nalazimika kukemea hiyo hali kwanza ndio sasa niendelee kuomba.Sasa ni jambo linalojirudia mara kwa mara.Naomba msaada wenu kujua hii Nonini na pia msaada wa maombi yenu

Fabian Baharia
Fabian Baharia
1 year ago

Nahitaji kufahamu utofauti wa biblia yenye vitabu 66 na ile yenye vitabu zaidi ya hivyo