Ijumaa kuu ni nini? Na kwanini iitwe kuu?

Ijumaa kuu ni nini? Na kwanini iitwe kuu?

Ijumaa kuu ni ijumaa ya mwisho kabisa ya Bwana wetu Yesu Kristo kuwepo hapa duniani, ni siku ile ambayo alipitia mateso mengi, na kusulibiwa, na kufa na kisha kuzikwa. Siku hii huadhimishwa na wakristo wengi ulimwengu, kama kukumbuka la mateso ya Bwana wetu Yesu Kristo kila mwaka.

Kwanini iitwe ijumaa kuu?

Lakini swali ni kwanini iitwe ijumaa kuu na sio ijumaa ya mateso au ya huzuni? Kwanini iwe kuu? Wakati siku hiyo ilikuwa ni siku mbaya sana ya mamlaka ya giza, ya huzuni na masumbufu ya Yesu mwokozi wetu?

Ni kweli kwa jicho la nje! Ni siku isiyo nzuri, lakini kwa jicho la Roho ni siku ya furaha sana tena sana kwetu sisi wanadamu, Kwani ni siku ambayo kwa mara ya kwanza tulifutiwa mashtaka yetu ya hukumu, tangu tulipopoteza uzima pale Edeni. Kwani asingekufa Yesu, tusingepata msamaha wa dhambi.. Hivyo kifo chake, kilileta ukombozi mkuu sana kwetu, na matokeo yake hatupaswi kulia, kinyume chake tufurahie, kwani siku kama ya leo, karibia miaka 2000 iliyopita, tuliwekwa huru…Hivyo ni sahihi kuitwa ijumaa kuu na sio ijumaa ya mateso.

Ni sawa na mfano wa Samaki anayevuliwa, yeye kwa upande wakw kweli atapitia mateso ya kufa, lakini yule anayemvua atafurahia kupata kitoweo. Hivyo tunaweza kusema ni uchungu kwa Samaki lakini furaha kwa mvuvi..

Kifo cha Bwana wetu Yesu kilikuwa ni faida kubwa kwetu, kwasababu kama damu yake isingemwagika, tusingepata ondoleo la dhambi zetu (Waebrania 9:22).

Na je! kuna agizo lolote la kutokula nyama siku hii ya ijumaa kuu?

Jibu ni La, desturi ya kutokula nyama (ya wanyama-damu moto), ni pokeo tu la kanisa katoliki, ambao kwa mujibu wao, wanafanya hivyo kwa heshima ya Kristo, kuutoa mwili wake, kama sadaka kwetu, kwasababu nyama ni chakula cha starehe, hawafanyi hivyo ili kuyatafakari mateso ya Bwana, na sio tu katika siku ya ijumaa kuu, bali  pia siku ya jumatano ya majivu, pamoja na ijumaa nyingine zote, zinazofuata katika mfungo  hawali nyama .

Lakini agizo hilo halipo mahali popote katika maandiko. Kama ukila haufanyi makosa, au usipokula vilevile haufanya makosa.

Lakini swali lingine ni je! Kuadhimisha sikukuu hii ni dhambi?

Jibu ni la!, Biblia haijatupa agizo wala katazo la mtu kuiadhimishi siku Fulani kwa Mungu wake.

 Ni kwa jinsi yeye anavyoamini tu!.

Warumi 14:5 “Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku, mwingine aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe.

6 Yeye aadhimishaye siku, huiadhimisha kwa Bwana; naye alaye, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu; tena asiyekula, hali kwa Bwana, naye pia amshukuru Mungu”.

Hivyo ikiwa wewe hauoni kama siku ya ijumaa kuu inafaida yoyote kwako, basi usimuhukumu yule ambaye anaiadhimisha kwa Mungu wake, lakini pia wewe ambaye unaidhimisha usimuhukumu yule ambaye haiadhimishi. . Ikiwa unaona mfungo huo kwa kipindi hicho cha pasaka hauna maana kwako, hufanyi kosa, lakini pia usimuhukumu yule ambaye anafunga kwa ajili ya Bwana wake aliyemfia msalaba.Ndivyo ilivyo

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Easter ni nini?. Na je tunaruhusiwa kuisheherekea?

PASAKA NI NINI? NA JE TUNARUHUSIWA KUSHEHEREKEA PASAKA?

Je! kuna sikukuu za pasaka mbili? (Hesabu 9:11)

SIKUKUU 7 ZA KIYAHUDI ZINAFUNUA NINI KWETU?

Mwandamo wa mwezi/Mwezi mpya Ni nini kibiblia?

BIBLIA INAITAJA NJIA KUU YA MFALME, NJIA HII NI IPI?

KRISIMASI (CHRISTMAS) NI NINI? JE IPO KATIKA BIBLIA?

Panda/ Sauti ya panda ni nini kibiblia?(Danieli 3:5)

KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 3

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
2 years ago

Amina

Joseph
Joseph
2 years ago

Amina mbarikiwa