Panda/ Sauti ya panda ni nini kibiblia?(Danieli 3:5)

Panda/ Sauti ya panda ni nini kibiblia?(Danieli 3:5)

SWALI: Biblia inaposema “hapo mtakapoisikia sauti ya Panda” Inamaanisha nini. Panda ni nini?


Panda ni pembe ya kondoo mume, ambayo ilitumika zamani kama tarumbeta.

Ilipopigwa iliashiria aidha kutangaza jambo jipya na kutoa tahadhari;

Danieli 3:5 wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, lazima kuanguka na kuiabudu sanamu ya dhahabu, mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha.

Danieli 3:7,10, 15, 2Wafalme 12:13

Panda Iliashiria pia kutangaza vita;

1Wafalme 1:41 “Basi Adonia, na wageni wote waliokuwa pamoja naye, wakasikia hayo walipokuwa wamekwisha kula. Naye Yoabu aliposikia sauti ya panda alisema, Za nini kelele hizi za mji uliotaharuki?”

Lakini zaidi ya yote, Panda ilitumika pia katika kumsifu na kumwimbia Mungu.

Zaburi 98:5 “Mwimbieni Bwana zaburi kwa kinubi, Kwa kinubi na sauti ya zaburi.

6 Kwa panda na sauti ya baragumu. Shangilieni mbele za Mfalme, Bwana.

2Nyakati 5:13 “hata ikawa, wenye panda na waimbaji walipokuwa kama mmoja, wakisikizisha sauti moja ya kumsifu na kumshukuru Bwana nao wakipaza sauti pamoja na panda na matoazi na vinanda, wakimsifu Bwana, wakisema, Kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele; ndipo nyumba ikajawa na wingu, naam, nyumba ya Bwana,

Nasi pia, ni wajibu wetu kumwimbia Mungu wetu na kumsifu, kwa kila namna ya ala ya muziki, tunaweza leo tusitumie pembe za wanyama kumsifu, lakini tuna ala za kisasa, ambazo ni bora kuliko zile za zamani. Hivyo tukimwimbia Mungu kwa ustadi, lakini katika Roho na kweli, nasi pia tutauona utukufu wa Mungu, na Nyumba zetu zitajawa na wingu, kama alivyofanya kwa wana wa Israeli walipokuwa wanaliwekwa wakfu hekalu la Mungu.

Shalom.

Tazama maana ya ala nyingine za muziki chini, zilizotumika enzi za biblia.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Kinubi ni nini katika biblia? (1Samweli 16:16, 23)

Matoazi na Matari ni nini? (Kutoka 15:20)

Nguo za magunia katika biblia ni zipi?

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita..

CHAPA YA MNYAMA

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments