Kinubi ni nini katika biblia? (1Samweli 16:16, 23)

Kinubi ni nini katika biblia? (1Samweli 16:16, 23)

Vyombo vya muziki vilivyotumika zamani katika biblia viligawanyika katika makundi makuu matatu.

  1. Vyombo vilivyopulizwa: Mfano Baragumu, filimbi, Tarumbeta, pembe, panda,
  2. Vyombo vilivyopigwa na kutoa sauti : Mfano Tari, Zomari, ngoma, kengele.
  3. Vyombo vilivyopigwa kwa kukwanyuliwa nyuzi zake: Mfano kinanda, kinubi, zeze, Santuri.

Kinubi, ni moja ya ala ya muziki, iliyopigwa kwa kukwanyua nyuzi zake aidha kwa kidole au kwa kifaa kingine kidogo. Kinubi kwa wayahudi kilikuwa kinatengenezwa kwa nyuzi kumi za utumbo mdogo wa kondoo.

Kuona jinsi kinavyopigwa..tazama video hii youtube >> https://www.youtube.com/watch?v=cS5d2wD8OoI

Bibia inamuonyesha Daudi alikitumia kifaa hichi, kwa ajili ya kumtuliza Mfalme Sauli, pale roho mbaya kutoka kwa Bwana ilipokuwa inamjia.

1Samweli 16:16 “Basi bwana wetu na atuamuru sisi watumishi wake waliopo hapa mbele yako watafute mtu aliye stadi wa kupiga kinubi; basi itakuwa, roho ile mbaya kutoka kwa Mungu itakapokujilia, yeye atapiga kinubi kwa mkono wake, nawe utapona…..

23 Ikawa, ile roho mbaya kutoka kwa Mungu ilipomjilia Sauli, ndipo Daudi akakishika kinubi, akakipiga kwa mkono wake, naye Sauli akaburudishwa, na ile roho mbaya ikamwacha”.

Wana wa Lawi pia walivitumia kumsifia Mungu wakati hekalu la Mungu lilipokuwa linajengwa.(2Nyakati 5:12)

Biblia pia inatuonyesha wale watu watakaotoka katika dhiki kuu siku ile, watakuwa na vinubi vyao mikononi wakimwimbia Kristo.

Ufunuo 15:2 “Tena nikaona kitu kama mfano wa bahari ya kioo iliyochangamana na moto, na wale wenye kushinda, watokao kwa yule mnyama, na sanamu yake, na kwa hesabu ya jina lake, walikuwa wamesimama kando-kando ya hiyo bahari ya kioo, wenye vinubi vya Mungu.

3 Nao wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu, na wimbo wa Mwana-Kondoo, wakisema, Ni makuu, na ya ajabu, matendo yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi; Ni za haki, na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa mataifa”.

Je! Na sisi tunapaswa tutumie vinubi katika kumwimbia Mungu?

Jibu ni ndio, ala yoyote ile ya mziki, iwe ni ngoma, iwe ni gitaa, iwe ni njuga, iwe ni zeze, iwe ni marimba, n.k. vinafaa katika kumwimbia Mungu. Isipokuwa tu hatupaswi kuimba kwa staili za kinua. Bali tunapaswa tumwimbie Mungu katika uzuri na utakatifu.

Zaburi 150:1 “Haleluya. Msifuni Mungu katika patakatifu pake; Msifuni katika anga la uweza wake.

2 Msifuni kwa matendo yake makuu; Msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.

3 Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni kwa kinanda na kinubi;

4 Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi;

5 Msifuni kwa matoazi yaliayo; Msifuni kwa matoazi yavumayo sana.

6 Kila mwenye pumzi na amsifu Bwana. Haleluya”.

Bwana akubariki.

Tazama ala nyingine za muziki chini.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Santuri ni nini? (Danieli 3:5,10)

Matoazi na Matari ni nini? (Kutoka 15:20)

Aina za dhambi

Kijicho ni nini? (Marko 7:22)

USIPIGE MATEKE MCHOKOO!

GOGU NA MAGOGU, Katika biblia ni nani?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Lawi Gideon
Lawi Gideon
2 years ago

Muendelee kuweka masomo mazuri. Mme furahishwa nayo.