Kijicho ni nini? (Marko 7:22)

Kijicho ni nini? (Marko 7:22)

Kijicho ni nini kibiblia?


Kijicho ni kitendo kilichoaminika na jamii nyingi za zamani, kwamba mtu anaweza kukusababishia madhara au kukuletea laana, kwa kukutazama tu kwa macho yake, na hiyo inaweza ikawa amekusudia au hajakusudia kufanya hivyo. Na hiyo  huwa inasababishwa na wivu.

Imani hii hata sasa ipo kwa watu wengi, wanaamini kuwa jicho la mtu linaweza kukuloga, au kukuletea mikosi, gundu, magonjwa. N.k. Hivyo wanatumia vitu kama hirizi, na matambiko kujilinda na madhara ya watu hao.

Lakini Je katika Marko 7:22 Yesu alimaanisha hicho?

Tusome;

Marko 7:21 “Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati,

22 wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, KIJICHO, matukano, kiburi, upumbavu.

23 Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi”.

Ni wazi kuwa Yesu hakumaanisha kijicho hicho kinachoaminiwa na wengi, hapana, bali hapa alimaanisha, JICHO OVU, jicho la uchoyo, jicho la wivu, na husuda.

Kuna mahali alisema..

Mathayo 20:15 “Si halali yangu kutumia vilivyo vyangu kama nipendavyo? Au jicho lako limekuwa ovu kwa sababu ya mimi kuwa mwema”?

Maneno hayo aliyasema alipokuwa anatoa ule mfano wa Yule mtu aliyewaajiri wafanyakazi wake shambani, na mwisho wa siku akawalipa wote sawa, bila kujali huyu alifanya sana, na huyu kidogo,.Vivyo hivyo na sisi macho yetu  yanaweza yakawa maovu kwasababu ya mtu mwingine kuwepwa upendeleo kama wetu, pengine mfanyakazi mpya amekuja na analipwa mshahara sawa au zaidi ya sisi tuliokuwepo kwa muda wa miaka 20 hapo kazini. Sasa kule kuona wivu, kutaka apewe kidogo kuliko wewe, hicho ndicho kijicho chenyewe ambacho Kristo anachokizungumzia kwamba  kinamtia mtu unajisi.

Sehemu nyingine kwenye biblia inasema;

Kumbukumbu 15:9 “Jitunze, msiwe na neno lisilofaa moyoni mwako, kusema, Umekaribia mwaka wa saba, mwaka wa maachilio; JICHO LAKO LIKAWA OVU juu ya nduguyo usimpe kitu; naye akamlilia Bwana juu yako, ikawa ni dhambi kwako”.

Unaona, aina nyingine ya kijicho ndio hiyo, kumdhulumu mtu haki yake kwa lengo la kumfanya aendelee kukutumikia, au pengine kwa wivu tu ili asifaidike akaweza kujitegemea. Hivyo wewe unadhamiria kumdhulumu haki yake ya utumishi kwako. Inaweza ikawa ni housegirl wako au houseboy wako au mlinzi wako, unapomnyima maslahi yake, hicho ni kijicho ambacho kitakutia unajisi na kukufanya usikubaliwe na Mungu.

Na ndio maana Bwana Yesu alisema;

Mathayo 6:22 “Taa ya mwili ni jicho; basi jicho lako likiwa safi, mwili wako wote utakuwa na nuru”.

Tunapaswa tuliondoe “jicho ovu” ndani yetu, Na hiyo inatokana na jambo moja tu, nalo ni kuushinda wivu. Wivu ukiondoka ndani ya mtu hataona uchungu kwa mwenzake kufanikiwa, hataona sababu ya kumdhulumu mfanyakazi wake, hataona sababu ya kumuundia visa jirani yake. Na matokeo yake Kijicho hufa ndani yake. Bwana atusaidie tuyatendee kazi na hayo. Ili nafsi zetu zisinajisike.

Shalom.

Tazama tafsiri za maneno mengine ya biblia chini.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Nini tofauti kati ya Husuda, faraka na uchafu?

MZAZI, JALI MAISHA YA KIROHO YA MTOTO WAKO.

GOGU NA MAGOGU, Katika biblia ni nani?

Nini maana ya K.K, na B.K?  (B.C na A.D).

NI KWA NAMNA GANI ROHO HUTUTAMANI KIASI CHA KUONA WIVU?

SAMEHE KUTOKA NDANI YA MOYO WAKO.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments