Nini tofauti kati ya Husuda, faraka na uchafu?

Nini tofauti kati ya Husuda, faraka na uchafu?

SWALI: Husuda ni nini?, faraka ni nini? na uchafu ni nini katika biblia?


JIBU: Husuda limeonekana sehemu kadhaa katika biblia na maana yake ni “WIVU”  na mtu kuwa na HUSUDA/WIVU ni Dhambi…..Ifuatayo ni baadhi ya mistari iliyozungumzia husuda.

Wagalatia 5:21 “HUSUDA, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu”

Na mwingine ni huu…

1Petro 2:1 “Basi, wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na HUSUDA na masingizio yote”

Na mingine ambayo unaweza kusoma kwa muda wako ni hii; Tito 3:3,Mathayo 27:18, Marko 15:10, Warumi 1:29, 1Wakorintho 3:3 n.k

Faraka ni nini?

Neno Faraka inatokana na neno mafarakano…Tafsiri yake inakaribiana na tafsiri ya neno matengano, na kuwa na faraka ni dhambi, Biblia imekataza wakristo kufarakana..na baadhi ya mistari kwenye biblia inayozungumzia “faraka” ni kama ifuatayo.

1Wakorintho 1:10 “Basi ndugu, nawasihi, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba nyote mnene mamoja; wala pasiwe kwenu FARAKA, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja”

Na mwingine ni..

1Wakorintho 12:25 “ili kusiwe na FARAKA katika mwili, bali viungo vitunzane kila kiungo na mwenziwe”

Na mingine ambayo unaweza kuisoma kwa muda wako ni kama ifuatayo; 1Wakorintho 11:17 na Wagalatia 5:20.

Uchafu ni nini?

Uchafu kila kitu kinachomtia mtu unajisi…mfano uasherati, ulawiti, ufiraji, ulevi na mambo yanayofanana na hayo, vile vile wachafu wote hawataurithi ufalme wa mbinguni biblia inasema hivyo….Baadhi ya mistari katika biblia inayozungumzia uchafu ni kama ifuatayo.

2Wakorintho 7:1″Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu”

Na mwingine ni huu..

Wagalatia 5:19 “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, UCHAFU, ufisadi,

20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,

21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu”.

Na mingine inayozungumzia uchafu ni Waefeso 4:19,Wakolosai 3:5, 1Wathesalonike 4:7 n.k

Je umeokoka?..Je una husuda? au una faraka au ni mchafu?..Biblia imesema watu wa namna hiyo hawawezi kuurithi uzimwa wa milele…Mpe Kristo leo maisha yako ayaokoe kama hujaokoka.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

KUOTA UNAJISAIDIA SEHEMU ZA WAZI.

YA KALE YAMEPITA, TAZAMA YAMEKUWA MAPYA

KUSAMBAA KWA ROHO YA MPINGA-KRISTO.

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

WAKAMCHA BWANA, NA KUITUMIKIA MIUNGU YAO WENYEWE.

HAKIKISHA UNALIELEWA NENO.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Mosest Hamis Amrani
Mosest Hamis Amrani
2 years ago

Mungu akubariki sana mtumishi

Joshua Ngogo
Joshua Ngogo
3 years ago

nimelipenda sana hili somo