KUOTA UNAJISAIDIA SEHEMU ZA WAZI.

KUOTA UNAJISAIDIA SEHEMU ZA WAZI.

Kuota Unajisaidia sehemu za wazi. Maana yake ni nini?


Ndoto hii, imekuwa ikiotwa mara kadhaa wa kadha na watu wengi. Kwa mfano mtu mmoja alinisimulia ndoto yake, anasema katika ndoto alijikuta yupo stendi ya basi, na pale palikuwa na watu wengi sana, ghafla akaanza kujisaidia lakini yeye alikuwa anajitahidi kufanya vile asionekana..Na alipomaliza akidhani hajaonekana wakati akiwa anarudi nyumbani mtu mmoja ambaye alikuwa anamjua akamfuata akamwambia mbona nilikuona unajisaidia pale stendi?..Anasema kwa kweli aliposikia hivyo   alijisikia aibu sana.

Na ndivyo ilivyo ndoto za namna hii, ni lazima mwisho wa siku utajisikia aibu tu, wengine wanaota wamejinyea, mavi, wengine wakiwa shuleni, kazini, uwanjani n.k. ..kwasababu kitendo cha kujisaidia huwa sikuzote ni cha aibu na ndio maana kinafanyika kwa siri chooni.. Lakini ikiwa unajisaidia kwa wazi ni Mungu anakuonyesha ni jinsi gani, mambo yako machafu yatakavyokuja kuwa dhairi siku moja mbele za watu wengi..kama hutatubu dhambi zako au hutasimama imara leo hii kwa Mungu wako.

Inaweza isiwe sasa, lakini kumbuka siku ile ya hukumu inafika..ambapo mambo yote yaliyokuwa yanafanyika kwa siri yatawekwa wazi.

2Wakorintho 5:10  “Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya”

1Wakorintho 4:5  “Basi ninyi msihukumu neno kabla ya wakati wake, hata ajapo Bwana; ambaye ATAYAMULIKISHA YALIYOSITIRIKA YA GIZA, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo kila mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu”.

Unaona? Hivyo ikiwa hujatubu dhambi zako, maisha yako bado ni machafu, YESU KRISTO bado hajaingia ndani yako kukusafisha uwe hai..Ni heri ukaamua kufanya hivyo kabla nyakati hizo mbaya hazijafika..Huu ndio wakati wa wewe, kusema basi..Nahitaji kuanza upya na Kristo..Usiseme mimi ni muislamu, hata wewe Unapaswa umgeukie YESU Kristo kwasababu yeye ndio njia na kweli na Uzima ya kukufikisha wewe mbinguni.

Ukimkaribisha leo maishani mwako, atakupokea na kukufanya upya. Unaona ni hali gani ulijisikia ulipojiona unafanya kitendo cha aibu katikatika ya umati wa watu..Sasa embu fikiria siku ile ya hukumu, Maisha yako yataanza kutazamwa  na Mungu mbinguni, pamoja na majeshi ya malaika zake, pamoja na watakatifu wa Mungu mamilioni kwa mamilioni..wote wanakutazama siku ile ulivyokuwa unazini na mume au mke ambaye si wako, watakutazama ulivyokuwa unajisaga kisirisiri mwenyewe nyumbani mwako..watakutazama ulivyokuwa unafanya mustarbation kwa siri chumbani, watakutazama ulivyokuwa unaangalia picha za uchafu, lakini kwa nje unaonekana wewe ni mwema, watakutazama mimba ulizotoa japo ulikuwa unajulikana kama ni mwanamke mstaarabu, machoni pa watu watu..watakutazama ufiraji uliokuwa unaufanya kwa mkeo, japo kwa nje unaonekana mtu unayejiheshimu….Siku hiyo watakutazama..Ni itakuwa ni AIBU KUU, ambayo utatamani hata usingezaliwa.

Lakini hayo yote ya nini mpaka yakukute wakati Kristo bado anakupenda?..Njoo kwa YESU ayabadilishe maisha yako leo hii..biblia inasema..saa ya wokovu ni sasa..Umeshindwa kuacha pombe, lakini Ukimruhusu Yesu aingie maishani mwako, ataikata hiyo kiu ya pombe, itakwisha kabisa..Umeshindwa kuacha uzinzi lakini ukimfuata Yesu leo hii, atakusaidia na hiyo hali utaishinda..na mambo mengine yote maovu unayoyatenda saa hii, ukimkabisha Yesu maishani mwako atakugeuza..anachohitaji kwako ni moyo wa toba tu basi..Na kumaanisha kweli kweli wala sio kujaribu..

Hivyo ikiwa umemaanisha kufanya hivyo..

Basi uamuzi unaoufanya ni wa busara sana ambao hautakaa uujutie maisha yako yote kama ilivyokuwa hata kwetu sisi. Unachopaswa kufanya, hapo ulipo, chukua muda mchache ujitenge peke yako. Kisha piga magoti, kisha fuatisha sala hii kwa Imani, ukijua kuwa Mungu yupo hapo karibu na wewe pembeni yako kukusikia..Kisha ukiwa sasa katika utulivu Sema sala hii kwa sauti.

EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU  MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.

ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.

AMEN.

Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithitisha toba yako kwa Vitendo ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo, Sasa Mungu akishaona umegeuka kwa vitendo basi toba yako anaipokea na atakuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako. Vile vile unahitaji, kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwambudu Mungu, na kujifunza biblia ili uukulie wokovu. Na vilevile ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.

Ubarikiwe sana

Group la whatsapp Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi

Mada Nyinginezo:

Tofauti kati ya ndoto na Maono ni ipi?

KUOTA UPO UCHI.

FUATILIA NDOTO HII, UTAJIFUZA KITU.

MTETEZI WAKO NI NANI?

DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.

CHUKIZO LA UHARIBIFU

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Imani Rulazigula
Imani Rulazigula
1 year ago

Natamani kujiunga kwenye group nipate mafundisho