(Ndoto ya Ndugu Yusufu, kutoka Tabora, mwaminio wa ujumbe wa Malaki 4:5)
Mbarikiwe sana ndugu zangu, Ndugu zangu naomba nisaidieni kupata tafsiri ya hii hii njozi maana imenitatiza sana:
Niliota kwamba BWANA YESU KRISTO amekuja duniani .lakini alipokuja aliwakuta watu baadhi wakiendeleea na shughuli zao (hawakujua kuwa amekuja) .na alipo fika alichukua watu baadhi akatoka nao kidogo nje ya kijiji kile (lakini kuna mtu mwingine alisema kwamba kuna kitu amesahau sehemu basi akaamua kukirudia hicho kitu ;huku wale wengine ambao BWANA YESU kawatoa nje ya kijiji wakiambatana nae)_..
Sasa tulipofika mwisho wa kijiji kile (pembezoni mwa kijiji ) BWANA YESU akasema anaanza kubagua Kondoo na mbuzi kwenye lile kundi alilotoka nalo kwenye kile kijiji .. .tulipokuwa katika kujiandaa ghafla nikaona Kondoo na mbuzi mbele yetu ..basi watu wakaanza kwenda kwenye Kondoo na wengine kwenye mbuzi..
Bwana alipomaliza kuwabagua .akaenda tena kwenye kondoo ndicho kilicho nishangaza AKAANZA TENA KUWABAGUA HAO KONDOO TENA. alikuwa ananyosha kidole mkono wa kulia wanakuja kwake.. Lakini walikuwa kama wanataka kugombaniana kwenda kwa Bwana. Kati ya lile kundi walitoka watu wachache sana wa kwenda na Bwana. Sasa baada ya kuwachagua Bwana akaenda kama kwenye kitu cha usafiri hivi.(sikukifahamu ) na alipofika akaingia kwanza na sisi tukafuata nyuma lakini kabla ya kuanza kuingia akafika yule aliye omba ruhusa kule mwanzo afuate kitu sehemu akasema nae anasitahili awe na BWANA lakini Bwana hakumkubalia .. Yule ndugu alilia sana akisema nae anastahili kuingia kwenye ule usafiri.
Na nilipokuwa nawaangalia ndugu niliokuwa nao sikumwona hata mmoja ninaye fahamiana nae.( hata mama yangu sikumwona hata baba ,wadogo zangu,hata ndugu na dada zikumwona hata mmoja) .ndio nikaaanza kusikitika nikitaka kulia ghafla ikaja sauti ikiniambia kwamba (nilikuwa kama nafikiria ikisema HAKITAINGIA KILICHO KINYONGE .na tena ikasema kwamba WALIO CHAGULIWA KABLA YA KUWEKWA MISINGI YA ULIMWENGU.).
Ndipo nikasikia Bwana akisema akimwita ndugu fulani..nilisika akisema PETRO KUNA CHAKULA .NIKAMWONA BWANA KAMA ANAANDAA CHAKULA HIVI. (Lakini cha kushangaza haya yote yalikuwa yakifanyika chini duniani) Baada ya hapo nikaona Mwanga mkali mbinguni. Hapohapo nikaamka . Nini maana yake ya hii njozi MUNGU wa mbinguni awafunulie maana yake. Shalom.
Ni wazi kuwa Bwana amekuonyesha maono ya siku za mwisho..Na ndoto hiyo tutaichapisha ili na wengine pia wanufaike kwasababu ujumbe huo haukuhusu wewe mwenyewe bali pia unalihusu kanisa la Kristo kwa ujumla, ambao ni sisi sote humo humo kwa ujumla. Kwanza kuwa upande wako unapaswa uamini kuwa bibi-arusi wa Kristo ni tofauti na Kanisa la Kristo kwa ujumla, mke ni tofauti na suria japo wote wanaweza kuwa ni milki ya Bwana arusi .Maana yake ni kuwa wanaoitwa wakristo ni wengi lakini bibi-arusi wa Kristo ni wachache sana, na ndio hao peke yao watakaokwenda kwenye unyakuo, na kutokana na uchache wao dunia haitajua kitu kitakachokuwa kinaendelea.,
Tofauti na watu wengi wanavyodhani kuwa unyakuo ukifika duniani kote kutakotekea machafuko ya kila namna, kila mtu atajua, ajali zitatokea mabarabarani, mamilioni ya watu watapotea, kana kwamba njia ya mbinguni ni njia nyepesi kuiingia kama shetani anavyowadanganya watu, biblia inasema kule hakitaingia kilicho kinyonge, na kama ingekuwa wengi Bwana asingesema Kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu, Embu kaa chini ufikirie siku za Nuhu walipona watu wangapi kama sio watu nane(8) tu kati ya mabilioni ya watu waliokuwa ulimwenguni?, Bwana asingesema tena kuja kwake kutafanana na kama zilivyokuwa siku za Lutu, siku zile walipona watu watatu (3) tu kati ya malaki ya watu waliokuwa katika miji ile…Ukisoma tena mahali pengine alisema “mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.(Mathayo 7:14)”..Yote hayo yanathibitisha kuwa mbinguni sio kurahisi kama watu wanavyokufikiri au wanavyofundishwa.. Unyakuo hautakuwa kwa mtu yeyote ambayo hajaonyesha nia ya kuuingia, sio kusema tu nimeokoka basi! Na kuendelea kuishi mtu anavyojisikia.
Na ndio maana hapo kwenye ndoto umeona kumbe hata katikati ya kondoo bado kulikuwa na mchujo..Hiyo inalingana na maandiko kabisa kama tukitazama mfano wa wale wanawali 10, (Katika Mathayo 25) ambao wote walikuwa ni wanawali (mabikira) safi, wote walikuwa wanamsubiria Bwana wao, isipokuwa katikati yao wengine walikuwa wenye busara na wengine wapumbavu. Wale wenye busara walichukua taa zao pamoja na mafuta ya ziada, lakini wale wapumbavu hawakubeba mafuta ya ziada katika vyombo vyao, na wakati ambao Bwana wao sasa anakuja ili awachukue taa zao zikawa zinaanza kuzima , Hivyo wale wapumbavu wakawaomba wenzao wawapunguzie kidogo, lakini wale wakasema hapana tukiwapa hayawezi kututosha sisi pamoja na nyie ni heri mshike njia mkanunue ya kwenu, na walipokwenda kununua, wakati wanarudi wakakuta tayari mlango umeshafungwa..Bwana akawaambia Amin, nawaambia, siwajui ninyi.
Unaona? Siku hizi ni siku za mwisho, na inasikitisha kuwa idadi kubwa ya watu wanaojiita ni wakristo sio wakristo kweli kweli, wanaitwa hivyo kwasababu tu wamezaliwa katika familia za kikristo, lakini ukiangalia mienendo yao, tabia zao, uvaaji wao, mazungumzo yao, yapo mbali kabisa na Ukristo, yaani ni wakristo-jina.
sasa hao ni ndio wale mbuzi uliowaona wakitengwa mbali na wale kondoo…Kadhalika wapo ambao kweli walianza vizuri na Bwana walisimama imara lakini ilifika wakati wakaanza kupoa mguu mmoja ukawa nje, mwingine ndani, mwanzoni macho yao yalikuwa yakielekea mbinguni, wamejitenga mbali na dhambi, wamethibitika katika imani lakini ikafikia wakati wakaanza kupoa mfano wa wale wanawali wapumbavu ambao hawakuwa na mafuta ya ziada katika taa zao. Na mafuta ya ziada ni UHAI WA ROHO WA MUNGU NDANI YA MTU. Sasa wakaanza kumzimisha Roho wa Mungu ndani yao, huko nyuma walianza vizuri lakini kidogo kidogo, wakaanza kupoa, mambo ya ulimwengu huu yakaanza kuwasonga, lakini ukiwatazama huwezi kujua kuwa wanamizigo ya kando inayowavuta, ibadani wanahudhuria, watavaa mavazi ya kujisitiri, hata katika maombi utawakuta, wanafanana kabisa na wale wakristo waaminifu waliosimama imara mbele za Mungu kwa uaminifu wote isipokuwa wao ni vuguvugu tu, sasa hao ndio wale kondoo uliowaona wakichambuliwa katikati ya kondoo…Walipaswa waende na wale wengine lakini kwa upumbavu wao wamebaki..
Ndugu hatupaswi kupoa kwa namna yoyote, hizi ni nyakati za mwisho, kanisa hili tunaloishi, ndilo kanisa la mwisho lijulikanalo kama Laodikia, Ndio lile la mwisho kati ya yale 7 yazungumziwayo katika kitabu cha Ufunuo 2&3, Israeli imeshakuwa taifa huru tena, Ni nini tunachokisubiria sasa kama sio UNYAKUO.
Na Bwana anasema Kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika siku za kuja kwake mwana wa Adamu,.Ikiwa utautazama upepo wa ulimwengu na kujifariji kwa mambo maovu yanayoendelea, ukidhani kuwa Bwana anatumia ile kauli ya “wengi wape”. Utajikuta unaingia katika gharika ya dhiki kuu, wakati wengi wapo mbinguni kwenye karamu ya mwanakondoo. Ndugu Unyakuo hautakuwa wa wazi kama watu wanavyodhani, unyakuo utakuwa ni SIRI, Na watakaofahamu ni wale wanawali werevu, wachache sana. Lakini dunia nzima itakuwa buzy wakati huo kumfurahia mpinga-Kristo na utawala wake.
Uamuzi ni wako ndugu unayesoma ujumbe huu, Kristo anarudi, na wala hatakawia, atakusanya ngano ghalani mwake na magugu atayatupa katika moto usiozimika…Tubu dhambi sasa, ukabatizwe, na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu, kwasababu hatuna wakati mwingi katika kizazi hichi.
Ubarikiwe.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Zinazoendana:
TABIA YAKO NI YA MNYAMA GANI?
USHUHUDA WA RICKY:
WALIPO WAWILI AU WATATU KWA JINA LANGU
Rudi Nyumbani
Print this post
Nimebarikiwa sana na mafundisho,ila hiyo ndoto ya huyu ndugu yangu ni halisia
Mungu akubariki kwa ufafanuzi wa neno la Mungu. Kazi yako ni njema sana ndugu utalipwa usipozimia roho. Hapo anavyosema kama vile siku za Nuhu au suku za rutu hamaanishi uchache Wa kiasi hicho Bali akimaanisha jinsi ambavyo hiyo siku ya kujakwake haijulikani.
Pia baada tu ya unyakuwo watu watajua kwamba kuna jambo kubwa limetendeka maana ni jambo la kutisha hilo. Maana ili Kazi ya mpinga kristo ifanyike na ionekane kwa wale atakaowatawala atakuwa anajaribu kuituliza dunia kuwapoza baada ya mfadhaiko utakotokea baada ya unyakuwo, ndio maana kwa watakokataa kuipokea chapa ya nembo Yake atawadhuru kwa mateso.
Ubarikiwe na Bwana Yesu endelea na Kazi ya Kristo ndugu.
Naomba kufafanuliwa ndoto hii,nilichota maji kwenye basin ya kuoga katika harakati ya kubeba yakawa yananimwagikia,huku watu nyuma wananiita nimeacha maji chafu,na hayo maji Safi niliyobeba sikuyaoga bunde tu nikashtuka usingizini.