Swali: Katika Kutoka 3:2 tunasoma kuwa Mungu alisema na Nabii Musa kupitia kile kijiti ambacho kilikuwa kinawaka moto lakini hakikuteketea, je kulikuwa kuna sababu gani au ufunuo gani katika ishara ile?
Jibu: Tuanze kusoma mstari ule wa kwanza mpaka ule wa tatu, ili tupate kuielewa vizuri habari..
Kutoka 3:1 “Basi huyo Musa alikuwa akilichunga kundi la Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani; akaliongoza kundi nyuma ya jangwa, akafika mpaka mlima wa Mungu, hata Horebu. 2 Malaika wa Bwana akamtokea, KATIKA MWALI WA MOTO ULIOTOKA KATIKATI YA KIJITI; AKATAZAMA, NA KUMBE! KILE KIJITI KILIWAKA MOTO, NACHO KIJITI HAKIKUTEKETEA. 3 Musa akasema, Nitageuka sasa, niyaone maono haya makubwa, na sababu kijiti hiki hakiteketei”
Kutoka 3:1 “Basi huyo Musa alikuwa akilichunga kundi la Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani; akaliongoza kundi nyuma ya jangwa, akafika mpaka mlima wa Mungu, hata Horebu.
2 Malaika wa Bwana akamtokea, KATIKA MWALI WA MOTO ULIOTOKA KATIKATI YA KIJITI; AKATAZAMA, NA KUMBE! KILE KIJITI KILIWAKA MOTO, NACHO KIJITI HAKIKUTEKETEA.
3 Musa akasema, Nitageuka sasa, niyaone maono haya makubwa, na sababu kijiti hiki hakiteketei”
Lengo la Mungu kumwonyesha Musa Ono hilo kubwa, halikuwa kumburudisha au kumsisimua, bali ulikuwa ni ujumbe wa MUNGU kwa Musa na kwa Israeli wote ambao watasumiliwa baadae.
Na ujumbe huo si mwingine Zaidi ya ule tuusomao katika Isaya 43:1-4..
Isaya 43:1 “Lakini sasa, Bwana aliyekuhuluku, Ee Yakobo, yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu. 2 Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; UENDAPO KATIKA MOTO, HUTATEKETEA; WALA MWALI WA MOTO HAUTAKUUNGUZA. 3 Maana mimi ni Bwana, Mungu wako; Mtakatifu wa Israeli, mwokozi wako, nimetoa Misri kuwa ukombozi wako; nimetoa Kushi na Seba kwa ajili yako. 4 Kwa kuwa ulikuwa wa thamani machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa, nami nimekupenda; kwa sababu hiyo nitatoa watu kwa ajili yako; na kabila za watu kwa ajili ya maisha yako”
Isaya 43:1 “Lakini sasa, Bwana aliyekuhuluku, Ee Yakobo, yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu.
2 Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; UENDAPO KATIKA MOTO, HUTATEKETEA; WALA MWALI WA MOTO HAUTAKUUNGUZA.
3 Maana mimi ni Bwana, Mungu wako; Mtakatifu wa Israeli, mwokozi wako, nimetoa Misri kuwa ukombozi wako; nimetoa Kushi na Seba kwa ajili yako.
4 Kwa kuwa ulikuwa wa thamani machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa, nami nimekupenda; kwa sababu hiyo nitatoa watu kwa ajili yako; na kabila za watu kwa ajili ya maisha yako”
Hapo katika mstari wa Pili (2) anasema… “UENDAPO KATIKA MOTO, HUTATEKETEA; WALA MWALI WA MOTO HAUTAKUUNGUZA”.
Na hiyo ndio sababu ya Mungu kumwonesha Musa ono lile, kwamba watakapopita (wana wa Israeli) katika Moto (yaani majaribu mbalimbali) hawataungua..mfano wa kile kijiti kilichowaka moto lakini hakikuteketea.
Hivyo kwa ufunuo huo Israeli walielewa kuwa Mungu anasema nao, kwamba atakuwa pamoja nao katika mapito yote, hivyo wasiogope majaribu wala moto watakaokutana nao, kwani hautawateketeza, kinyume chake utawateketeza maadui zao…mfano wa akina Shadraka, Meshaki na Abednego, ambao walitupwa katika tanuru la moto, na badala ya moto ule kuwala wao, uligeuka na kuwala maadui zao wale walioshika na kuwatupa motoni.
Danieli 3:20 “Kisha akawaamuru baadhi ya watu mashujaa wa jeshi lake kuwafunga Shadraka, na Meshaki, na Abednego, na kuwatupa katika ile tanuru iliyokuwa ikiwaka moto. 21 Basi watu hao wakafungwa, hali wamevaa suruali zao, na kanzu zao, na joho zao, na mavazi yao mengine, wakatupwa katikati ya ile tanuru iliyokuwa ikiwaka moto. 22 Basi kwa sababu amri ya mfalme ilikuwa ni kali, na ile tanuru ilikuwa ina moto sana, mwako wa ule moto ukawaua wale watu waliowashika Shadraka, na Meshaki, na Abednego. 23 Na watu hao watatu, Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakaanguka, hali wamefungwa, katikati ya ile tanuru iliyokuwa inawaka moto. 24 Ndipo Nebukadreza akastaajabu, akainuka kwa haraka; akanena, akawaambia mawaziri wake, Je! Hatukutupa watu watatu, hali wamefungwa, katikati ya moto? Wakajibu, wakamwambia mfalme, Kweli, Ee mfalme. 25 Akajibu, akasema, Tazama, mimi naona watu wanne, nao wamefunguliwa, wanatembea katikati ya moto hali hawana dhara; na sura yake yule wa nne ni mfano wa mwana wa miungu”
Danieli 3:20 “Kisha akawaamuru baadhi ya watu mashujaa wa jeshi lake kuwafunga Shadraka, na Meshaki, na Abednego, na kuwatupa katika ile tanuru iliyokuwa ikiwaka moto.
21 Basi watu hao wakafungwa, hali wamevaa suruali zao, na kanzu zao, na joho zao, na mavazi yao mengine, wakatupwa katikati ya ile tanuru iliyokuwa ikiwaka moto.
22 Basi kwa sababu amri ya mfalme ilikuwa ni kali, na ile tanuru ilikuwa ina moto sana, mwako wa ule moto ukawaua wale watu waliowashika Shadraka, na Meshaki, na Abednego.
23 Na watu hao watatu, Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakaanguka, hali wamefungwa, katikati ya ile tanuru iliyokuwa inawaka moto.
24 Ndipo Nebukadreza akastaajabu, akainuka kwa haraka; akanena, akawaambia mawaziri wake, Je! Hatukutupa watu watatu, hali wamefungwa, katikati ya moto? Wakajibu, wakamwambia mfalme, Kweli, Ee mfalme.
25 Akajibu, akasema, Tazama, mimi naona watu wanne, nao wamefunguliwa, wanatembea katikati ya moto hali hawana dhara; na sura yake yule wa nne ni mfano wa mwana wa miungu”
Ni hivyo hivyo hata sasa, Mungu anawalinda wale wote wamwaminio na kumtumainia yeye, wanakuwa kama kijiti kilichopo motoni lakini hakiteketei.. Wengine wakipitia majaribu wanapotea kabisa, lakini watu wa Mungu wanapita katikati ya moto na wanatoka salama.
Je umempokea Bwana YESU?. Je yeye ni tumaini lako na ngao yako?..Kama upo nje ya Kristo fahamu kuwa Moto utakuunguza, na ibilisi atakumaliza. Lakini ukiwa ndani ya YESU utakuwa salama.
Mpokee YESU kama bado hujampokea, hizi ni siku za mwisho naye amekaribia kurudi sana.
Waebrani 10:37 “Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, Yeye ajaye atakuja, wala hatakawia. 38 Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye”.
Waebrani 10:37 “Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, Yeye ajaye atakuja, wala hatakawia.
38 Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye”.
Maran atha!
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Naomba kufahamu maana ya “sura ya kijiti” katika Marko 12:26.
UFALME WA MUNGU HAUPATIKANI KIRAHISI.
KWANINI MUNGU ALIMTUMIA MUSA KWA VIWANGO VILE?
DUNIANI MNAYO DHIKI.
UJIO WA BWANA YESU.
Rudi Nyumbani
Print this post