Jibu: Tusome,
Marko 12:26 “Na kwa habari ya wafu ya kwamba wafufuliwa, hamjasoma katika kitabu cha Musa, SURA YA KIJITI, jinsi Mungu alivyomwambia, akisema, Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo?”
Neno “sura” kama lilivyotumika hapo sio “uso”..kama huu wenye pua, na macho na masikio.. bali limetumika kuwakilisha “mlango fulani” katika maandiko.. Kama tunavyojua tukitaka kupata habari Fulani katika maandiko, huwa tunafungua biblia na kusema fungua kitabu Fulani, mlango Fulani utapata habari hiyo.
Kwamfano tukitaka kupata habari ya kufufuka kwa Bwana tunazipata katika kitabu cha Luka Mlango wa 24..Sasa badala ya kutumia neno mlango, wakati mwingine tunatumia neno “Sura”..hivyo ni sawasawa na kusema “habari za kufufuka kwa Bwana Yesu tunazipata katika kitabu cha Luka sura ya 24”.
Kadhalika hapo Mtume Paulo alikuwa anamaanisha “Sura ile katika maandiko ambayo Mungu alizungumza na Musa kupitia kile kijiti kilichokuwa kinawaka moto lakini hakiteketei”.. Na hiyo si nyingine zaidi ya ile sura ya 3 katika kitabu cha “Kutoka”…tusome.
Kutoka 3:1 “Basi huyo Musa alikuwa akilichunga kundi la Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani; akaliongoza kundi nyuma ya jangwa, akafika mpaka mlima wa Mungu, hata Horebu. 2 Malaika wa Bwana akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kijiti; akatazama, na kumbe! Kile kijiti kiliwaka moto, nacho kijiti hakikuteketea. 3 Musa akasema, Nitageuka sasa, niyaone maono haya makubwa, na sababu KIJITI HIKI HAKITEKETEI. 4 Bwana alipoona ya kuwa amegeuka ili atazame, Mungu akamwita kutoka KATIKATI YA KILE KIJITI, akasema, Musa! Musa! Akasema, Mimi hapa. 5 Naye akasema, Usikaribie hapa; vua viatu vyako miguuni mwako; maana mahali hapo unaposimama ni nchi takatifu. 6 Tena akasema, Mimi ni Mungu wa baba yako, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo. Musa akaficha uso wake; kwa maana aliogopa kumwangalia Mungu. 7 Bwana akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri”
Kutoka 3:1 “Basi huyo Musa alikuwa akilichunga kundi la Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani; akaliongoza kundi nyuma ya jangwa, akafika mpaka mlima wa Mungu, hata Horebu.
2 Malaika wa Bwana akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kijiti; akatazama, na kumbe! Kile kijiti kiliwaka moto, nacho kijiti hakikuteketea.
3 Musa akasema, Nitageuka sasa, niyaone maono haya makubwa, na sababu KIJITI HIKI HAKITEKETEI.
4 Bwana alipoona ya kuwa amegeuka ili atazame, Mungu akamwita kutoka KATIKATI YA KILE KIJITI, akasema, Musa! Musa! Akasema, Mimi hapa.
5 Naye akasema, Usikaribie hapa; vua viatu vyako miguuni mwako; maana mahali hapo unaposimama ni nchi takatifu.
6 Tena akasema, Mimi ni Mungu wa baba yako, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo. Musa akaficha uso wake; kwa maana aliogopa kumwangalia Mungu.
7 Bwana akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri”
Kwahiyo “Sura” ni “Mlango”..Na kijiti kilichozungumziwa hapo sio kipande kidogo cha mti, bali ni “kichaka”.
Hivyo kikubwa tunachoweza kujifunza hapo ni kwamba Mungu ni Mungu wa walio hai… Alijitambulisha kwa Musa kama Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo.. Kwasababu Watu hao ingawa wamekufa sasa, lakini huko waliko wanaishi…kama Bwana Yesu mwenyewe alivyosema katika kitabu cha Yohana..
Yohana 11:25 “Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi”
Hivyo Ibrahimu, Isaka na Yakobo wanaishi sasa, na hivyo Mungu ni Mungu wao hata sasa… kadhalika na sisi tukiishi kwa kumwamini Yesu, na kuishi kulingana na mapenzi yake hapa duniani, tutakapokufa bado tutakuwa tunaishi katika paradiso ya raha, na baadaye tutafufuliwa kutoka huko paradiso na kuvikwa miili ya utukufu na kwenda na Bwana mbinguni, katika siku ile ya unyakuo..
Waebrania 11:16 “Lakini sasa waitamani nchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni. KWA HIYO MUNGU HAONI HAYA KUITWA MUNGU WAO; maana amewatengenezea mji”.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Kwanini Yakobo alimshinda Mungu, Je! Mungu huwa anashindwa na wanadamu?
Naye aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika-vunjika..
MWANZO WA INJILI YA YESU KRISTO.
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1
Rudi nyumbani
Print this post