Bwana Yesu sio tu mzaliwa wa kwanza wa waliokufa bali pia ni mzaliwa wa kwanza wa wanadamu wote walio hai.
Kwanini ni mzaliwa wa kwanza wa walio hai pia?.
Ni Kwasababu wote walio hai, hawana budi kuzaliwa tena mara ya pili ili wahesabike kuwa wana wa Mungu (Yohana 3:6). Ndio maana Bwana Yesu anabaki kuwa mzaliwa wa kwanza wa wanadamu wote..kwasababu ni yeye pekee tu ndiye aliyezaliwa mkamilifu, hana haja ya kuzaliwa mara ya pili, lakini sisi wengine wote hatuna budi kuzaliwa mara ya pili…
Warumi 8:29 “Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ILI YEYE AWE MZALIWA WA KWANZA MIONGONI MWA NDUGU WENGI”.
Na ni kwanini yeye pia ni Mzaliwa wa kwanza wa waliokufa!.
Kabla ya kujua ni kwanini yeye ni mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, ni vyema tukajua kwa kina maana ya kuzaliwa.. Kuzaliwa ni kitendo cha kutoka katika upeo mmoja kuingia katika upeo mwingine..Tunapozaliwa hapa ulimwenguni, ni kwamba tumetoka katika upeo mwingine tusioujua sana ulio juu, na kuja katika huu ulimwengu.. hapo tunasema tumezaliwa.. Kadhalika mtu anayetoka katika upeo mwingine ulio chini na kuja katika huu ulimwenguni, naye pia huyu kazaliwa!, kwasababu hakuwepo katika ulimwengu lakini sasa yupo!..kuzaliwa huko ndio tunakuita kufufuka!
Hivyo baada ya Kristo kufa, yeye pekee ndiye mtu wa kwanza kufufuka!. (kuzaliwa kutoka katika wafu)
Sasa utauliza kama yeye ni wa kwanza vipi wale watu waliofufuliwa na nabii Elisha kabla yake, na Eliya, au vipi kuhusu Lazaro ambaye Bwana mwenyewe alimfufua!..
Kumbuka hao wote ni kweli walifufuliwa lakini baadaye walikuja kufa tena!.. Lazaro ni kweli alifufuliwa lakini alikuja kufa tena!..na wengine wote ni hivyo hivyo.. Lakini Bwana Yesu alipofufuka hakufa tena, yupo hai milele na milele..Na baada yake yeye ndio wafu wote wanafuata kufufuliwa, ili wasife tena.. ambapo yeye anabaki kuwa mzaliwa wa kwanza kutoka katika mauti..
Ndio maana biblia inasema..
Wakolosai 1:17 “Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye.
18 Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, NI MZALIWA WA KWANZA KATIKA WAFU, ili kwamba awe mtangulizi katika yote.
19 Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae;
20 na kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake; kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi, au vilivyo mbinguni”.
Na tena inasema..
Yohana 1:5 “tena zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi aliye mwaminifu, MZALIWA WA KWANZA WA WALIOKUFA, na mkuu wa wafalme wa dunia. Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake”
Pia unaweza kusoma Waebrania 1:5, 1Wakorintho 15:20, na Wakolosai 1:15.. Inaelezea zaidi juu ya Kristo kama mzaliwa wa kwanza waliokufa.
Hivyo kwa hitimisho ni kwamba Kristo ndiye Mzaliwa wa kwanza wa kila kitu.(Ni mwanzo na Mwisho) Na mzaliwa wa kwanza siku zote ndiye mrithi!..sisi wengine tuliozaliwa mara ya pili katika roho ni kama wadogo zake. (Yeye ndio wa kwanza, sisi tunafuata) .Hivyo na sisi tunapozaliwa mara ya pili, tunazirithi ahadi za Mungu pamoja na Kristo..
Lakini kama hatutazaliwa mara ya pili, hatutaweza kuwa warithi..
Sasa tunazaliwaje mara ya pili?
Tunazaliwa mara ya pili, kwa kumwamini Yesu kama mzaliwa wa kwanza wa vitu vyote, na kwamba yeye ndiye aliyakabidhiwa urithi wote wa ahadi za Mungu, kwasababu ndiye mzaliwa wa kwanza..
Na baada ya kujua hilo na kuamini hilo, basi hatua inayofuata ni kutubu dhambi zetu zote tunazozifanya kwa wazi au kwa siri, na kujinyenyekeza chini yake na kisha tunatafuta ubatizo sahihi, ambao ni ule wa maji mengi na kwa Jina la Yesu Kristo kulinga na (Matendo 2:38) na kwa ubatizo wa Roho Mtakatifu ambao tutakuwa tumeupokea, huo unatufanya kuwa wakamilifu..Kwasababu Bwana Yesu mwenyewe alisema katika Marko 16:16, kwamba aaminiye na kubatizwa ataokoka, na pia alifafanua vizuri kwa Farisayo Nikodemo maana ya kuzaliwa mara ya pili, kwamba ni kwa Maji na kwa Roho.. Maana yake kwa ubatizo wa maji na wa Roho Mtakatifu!.
Yohana 3:4 “Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?
5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.
6 Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.
7 Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili”
Na kumbuka kuzaliwa ni hatua ya kwanza tu!..huna budi kuukulia wokovu kwa kumtafuta Mungu kwa bidii, unapozidi kumtafuta Mungu, ndivyo unavyozidi kukua kiroho, na hatimaye unafikia utimilifu ule Mungu anaotaka wewe uufikie.
Bwana atubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho mengin
Mada Nyinginezo:
About the author