Noeli ni nini, na je! Neno hili linapatikana katika biblia?

Noeli ni nini, na je! Neno hili linapatikana katika biblia?

Noeli kwa lugha ya kilatini ni neno linalomaanisha, “siku ya kuzaliwa” , lakini linalenga mahususi siku ya kuzaliwa kwa mfalme wa ulimwengu duniani (yaani Yesu Kristo). Na kwa lugha ya kifaransa neno hili  linaweza kumaanisha aidha “habari njema” au “msimu  wa Krisimasi” kwa ujumla.

Pengine Neno hili umeshawahi kulisikia sana likiitwa kwa jina la watu, au likitajwa katika nyimbo moja maarufu ijulikanayo kama “Noeli ya kwanza”;

Hivyo kwa maneno mafupi, hili ni neno linalomaanisha kusheherekea au kutangazwa kwa habari njema za kuzaliwa kwa Bwana Yesu duniani. Popote unapolisikia likitajwa basi ujue hizo ni habari za kuzaliwa kwa Yesu au msimu wote wa sikukuu ya Krisimasi kwa ujumla, Disemba 25

Kumbuka Neno hili halipo mahali popote katika biblia, Utalisikia sana sana katika madhebehu makongwe kama vile Katoliki, Anglikana na Lutheran.

Lakini Je ni takwa sisi wakristo kusheherekea Noeli /Krisimasi? Je! Ni kweli Yesu alizaliwa Disemba 25?.. Ili kufahamu fungua hapa >> KRISIMASI NI NINI?

Bwana akubariki.

Tazama maana nyingine ya maneno ya kibiblia chini;

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

SIFONGO NA SIKI NI NINI?

Sadaka ya kuinuliwa ni sadaka ya namna gani?

Herode aliliwa na chango, Je, chango ni nini kibiblia?

Mruba ni mdudu gani kwenye biblia?(Mithali 30:15)

Rudi nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
MUZAMIL MUHAMMAD
MUZAMIL MUHAMMAD
21 days ago

Kwani mfalme wa ulimwengu ni nani maana kuna wakati huwa mnatuambia SHETANI na wakati mwengine mnatuambia YESU ila MIMI binafsi naamini MUNGU ndio mfalme wa kweli wa ulimwengu.
TAFADHALI tufundisheni mambo kwa uhalisia na sio kutubadilishia maelezo kila mnapoamua kufanya hivyo.