Sadaka ya kuinuliwa ni sadaka ya namna gani?

Sadaka ya kuinuliwa ni sadaka ya namna gani?

Jibu: Sadaka ya kuinuliwa ni sadaka ambayo mtu anaiinua mbele za Mungu. Na ni sehemu ya sadaka iliyo ya heshima kuliko nyingine yoyote ile.

Kwamfano mtu anaweza kutoa sadaka ya kawaida ya kila siku, lakini isiwe iliyo kuu na ya heshima, lakini akatenga sadaka moja ambayo itakuwa ndio kaiheshimu kuliko zote.. ambayo atakwenda kuiinua mbele za Mungu, huku akiambatanisha na haja fulani, au shukrani fulani.

Hesabu 15:18 “Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mtakapoingia nchi niwapelekayo,

19 ndipo itakapokuwa ya kwamba hapo mtakapokula katika chakula cha nchi hiyo, mtamsongezea Bwana sadaka ya kuinuliwa”.

Mara nyingi sadaka hii ya kuinuliwa inakuwa ni ya “maandalizi”, sio tu ya kufikiri siku moja na kwenda kuitoa, na pia inakuwa ni ya kujitoa kweli kweli (maana yake ni ya kiwango kikubwa, au ya kugharimu), ikiwa sio ya kugharimu inakuwa haina tofauti na sadaka nyingine.

Kumbuka pia sadaka kama Zaka, na  Malimbuko hizo sio sadaka za kuinuliwa, hizo ni sadaka ambazo ni za wajibu, na hazipo katika kundi hili la sadaka za kuinuliwa.

Kumbuka tena sadaka hii ni tofauti na sadaka nyingine, ni lazima iwe na heshima kuliko nyingine, ndio maana imeitwa Sadaka ya KUINULIWA, maana yake ni ya hadhi ya juu zaidi kuliko nyingine, “Umeiinua kuliko nyingine”.  kwahiyo ni dhambi kumtolea Mungu sadaka kilema. Na kuiinua mbele za Mungu.

 Ni dhambi kumpa Mungu sadaka ya shukrani shilingi elfu moja, na kuisongeza mbele zake na kusema nimemwinulia Bwana sadaka hii, (tena na kujiona umemtolea kikubwa mbele zake) na unatoka ukijisifu kwamba umemtolea Mungu… na wakati kakufanyia muujiza wa mamilioni. Hapo ni sawa na umeiinua sadaka ambayo haistahili kuinuliwa, hivyo ni dhambi, ni heri usingetoa kabisa.

Ni sawa na umemwahidi mtu unampelekea zawadi nzuri na kubwa sana, baada ya jambo zuri alilokufanyia na tena ukainadi zawadi hiyo na kuitukuza sana mbele zake..na mwisho wa siku unampelekea zawadi ya hadhi ya chini sana, kuliko ya alivyotarajia, na tena ukaifunga kwenye box zuri. Unadhani ni nini kitafuata?..Ni wazi kuwa yule mtu atachukia atasema ni heri usingempa hiyo zawadi au ni kama ulikuwa unataka kumpa basi ungemwambia tu kwamba utampa kitu fulani kidogo, ili ajue na kujiandaa kabisa kwamba kitakachokuja kinaweza kuwa kidogo. Lakini kwa jinsi ulivyoisifia na kuiinua zawadi hiyo, halafu anakuta ni kidogo sana, ataishia kuchukia.

Ndio hivyo hivyo, pia sadaka ya kuinuliwa..inapaswa iwe kubwa na  iwe tofauti na sadaka nyingine..vinginevyo kama huwezi  basi toa tu sadaka yako ya kawaida ya kila siku ila usiinyanyue sana mbele za Mungu.

Lakini kama Bwana kakufanyia muujiza mkubwa sana, na wewe ukasema nitamsogezea sadaka ambayo nitaiinua mbele zake, na ukamtolea sehemu kubwa sana na iliyokugharimu angalau sawasawa au karibia na kile alichokufanyia. Hapo sadaka hiyo inakuwa na nguvu mara nyingi zaidi kuliko sadaka nyingine yoyote ya kawaida. Na inaachilia matokeo haraka sana, ikiwemo kuinuliwa kwa huyo mtu. Na Mungu anawaheshimu wale wote wanaomtolea kwa moyo na kwa bidii.

Bwana atubariki na kutusaidia.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312


Mada Nyinginezo:

Je! ni vema kwa mkristo kwenda hospitali au kutumia miti shamba anapougua?

TOA SADAKA ISIYO NA KASORO KWA BWANA.

FUKUZA TAI WOTE JUU YA SADAKA YAKO.

Mlango uitwao “Mzuri” Unaozungumziwa katika Matendo 3:2 ndio upi?

Kuota upo nchi nyingine.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
M
M
2 years ago

Amina Mungu awabariki

Wilson Metta
Wilson Metta
2 years ago

MUNGU awabariki sana, kazi njema mmnayoifanya. Ninabarikiwa sana na mafundisho yenu yana nisaidia sana kiroho, ninatamani sana kuonana au kuongea nawe mtumishi wa Kristo Yesu.
Shalom.