Kuota upo nchi nyingine.

Kuota upo nchi nyingine.

Kuota upo nchi nyingine.


Kama tunavyojua ukisafiri mahali ambapo ni tofuati na makazi yako ya asili, utakutana na mabadiliko mengi sana, hususani pale unapovuka mipaka na kuingia katika nchi nyingine, si ajabu kukutana na hali ya hewa ya aina nyingine, kukutana na watu wa jamii nyingine, kukutana na lugha gheni, n.k..

Na hiyo itakufanya usijione upo huru sana kama ulivyokuwa katika nchi yako mwenyewe.Na wakati mwingine inaweza kukufanya ujione haupo sehemu salama sana, kwasababu sio nchi yako, na haujaizoea.

Wana wa Israeli walipokuwa wanachukuliwa utumwani kupelekwa Babeli, wakiwa njiani walilia sana, hata wale wakaldayo,walipowashurutisha wawaimbie nyimbo za nchini mwao walikataa, wakasema tutaimbaje wimbo wa Bwana nchi ya ugenini?

Zaburi 137:1 “Kando ya mito ya Babeli ndiko tulikoketi, Tukalia tulipoikumbuka Sayuni.

2 Katika miti iliyo katikati yake Tulivitundika vinubi vyetu.

3 Maana huko waliotuchukua mateka Walitaka tuwaimbie; Na waliotuonea walitaka furaha; Tuimbieni baadhi ya nyimbo za Sayuni.

4 Tuuimbeje wimbo wa Bwana Katika nchi ya ugeni”?

Kwasababu walijua kabisa wanakwenda katika nchi ambayo sio ya kwao, katika mazingira ambayo hawajayazoea. Kwenye tamaduni mpya,

Hivyo unapojiona kwenye ndoto upo katika nchi ya ugenini, unaishi huko, au unatembea, Yapo mambo mawili hapo ambayo Mungu anakuonyesha.

Jambo la kwanza; Ikiwa wewe umeokoka, (yaani umeokolewa na Bwana Yesu), Hapo ni Mungu anakuonyesha wazi jinsi itakavyokuwa pale utakapotoka katika hifadhi yake. Utakuwa kama mtumwa, hivyo, jiangalie na jithibitishe, zidi kukaa katika mapenzi ya Mungu na kama ulikuwa umeshaanza kupoa, basi mgueukie Mungu wako kwa moyo wako wote. Ili ubakie katika nchi yako ya wokovu aliyokukusudia.

Lakini ikiwa hujaokoka, ni Mungu anakuonyesha hali yako ilivyo leo hii, upo katika nchi ya ugenini, japo hustahili kuwepo huko. Maisha yako yapo ugenini, hivyo huwezi kuwa huru, huwezi kuwa na amani, haijalishi pataonekana  ni pazuri namna gani, Wana wa Israeli walilia, walipokuwa wanaenda ugenini. Hivyo na wewe pia uliye dhambini, upo ugenini, pengine kampani unazotembea nazo sio ambazo Mungu amekukusudia utembee nazo, Mungu anakuhitaji wewe ukae na watakatifu wenzako uyatafakari maisha ya mbinguni. Pengine ulevi, anasa, wizi n.k., sivyo ambavyo vinakupasa mtu kama  wewe, na hilo unalijua kabisa, lakini bado unashikama nalo.

Embu yatafakari maisha yako, Je! Tangu ulipokuwa katika maisha ya dhambi ni raha gani umeipata au faida gani umepata?. Kwanini usizingatie kurudi nyumbani, kama yule mwana mpotevu aliyekwenda kuponda mali katika nchi ya mbali, lakini baadaye akazingatia kurudi kwa baba yake..Kwanini na wewe usizingatie kurudi kwa Baba yako wa mbinguni leo umwombe msamaha baada ya kupotea kwa muda mrefu.?

Ukisoma biblia utamwona Kaini yule aliyemuua ndugu yake ndiye aliyekuwa mtu asiye na kikao duniani, kama vile mapepo. Je na wewe unataka uwe mtu asiye na makao yake maalumu?

Leo hii ukikubali kutubu dhambi zako, Yesu atakupokea na kukusamehe, haijalishi wewe ni wa dini gani au dhehebu gani. Atakupokea, na kukukaribisha kwake, na atakupa raha nafsini mwako. Hivyo Kama upo tayari kufanya hivyo leo, basi fungua hapa kwa ajili ya maelekezo ya sala ya Toba, na Bwana akubariki. >>> SALA YA TOBA

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312/

Pia kwa ushauri/ratiba za ibada/ maombezi.

Jiunge kwenye magroup yetu ya Whatsapp kwa masomo ya kila siku ya Neno la Mungu.

Group la whatsapp  Jiunge na channel yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP

Mada Nyinginezo:

KUOTA UMEACHWA NA GARI.

KUOTA UPO UCHI.

Wakaldayo ni watu gani?

HEKIMA YA KIMUNGU, INAINGIAJE MIOYONI MWETU?

PALE AHADI ZA MUNGU ZINAPOKUJARIBU.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments