KUOTA UMEACHWA NA GARI.

KUOTA UMEACHWA NA GARI.

Kuota umeachwa na gari, Maana yake ni nini?


Hii ni ndoto inayowapata watu wengi sana.Hususani wale ambao walishaokoka, lakini mambo mengine ya kidunia yanawasonga sasa hivi..Au walisharudi nyuma kabisa na kuacha wokovu

Ndogo hii inakuja katika maumbile tofuati tofauti wengine wanaota wameachwa na ndege, wengine wanaota wameachwa na wenzao ambao walikuwa wanakwenda pamoja,  lakini wengi wao wanaota wameachwa na gari walilokuwa wanasafiria.

Kwa mfano mtu mmoja alinihadhithia ndoto hii, ambayo rafiki yake aliiota ikawa inamsumbua sana..

Aliota alikuwa kwenye basi anasafiri, sasa lile basi likafika mahali kwenye foleni, na yeye baada ya kuona vile limesimama pale,  akaamua kushuka kidogo, na aliposhuka tu lile gari likaanza safari, anasema akaanza kulikimbilia, kumbe wakati analikimbilia kulikuwa na watu wengi nao wanalikimbilia lile gari, mchanganyiko wamama, watoto, na watu wengine n.k. Lakini baadaye yeye akajitahidi kwa nguvu sana kuliwahi akafanikiwa kuingia lakini kwa shida sana, na alipofika ndani akakuta siti yake imeshakaliwa na mtu mwingine..Ikimbidi ajikalie tu mwenyewe pale pembeni, lakini baada ya muda mfupi mzee mmoja akatokea akamsukuma atoke hata pale alipokuwa amekaa, akiwa hana sehemu ya kukaa kwa bahati nzuri akaona siti moja ipo wazi pembeni yake akaenda kuikalia na muda huo huo akashtuka..

Nilipo hoji nikagundua kuwa mtu huyo alikuwa ameokoka lakini baadaye alirudi nyuma, amesongwa na mambo ya ulimwengu huu..Na pale Mungu alikuwa anamwonyesha mwenendo wake jinsi ulivyo alipoona anakawia kukipata kile alichokuwa anakitafuta katika njia yake ya wokovu akaamua kwenda kukitafuta katika mambo ya ulimwenguni..Na hiyo itamgharimu kwasababu upo wakati atatamani kurudi lakini itakuwa ngumu sana kwake kwasababu wokovu sio safari ya kujaribu jaribu kama yule mke wa Lutu alivyofanya, aligeuka mara moja tu, na saa hiyo hiyo akageuka kuwa jiwe la chumvi.

Ikiwa na wewe ni mfano wa mtu kama huyu umeota ndoto ya namna hii umeachwa na basi ujue huo ni ujumbe kamili kutoka kwa Mungu, kuwa unaupoteza wokovu wako, na kuwa ukiendelea katika hali hiyo inayoendelea sasahivi ya kujitenga na wokovu, au kusongwa na mambo ya ulimwengu basi hautaupata tena daima na nafasi yako atapewa mwingine..

Lakini kama wewe hujaokoka kabisa yaani Bwana YESU hajayabadilisha maisha yako, wala huna habari na Mungu.. wewe umekuwa mkristo jina tu, au Muislamu, au huna dini kabisa..Hapo ni Mungu anakuonyesha jinsi gani inavyoogopesha na inavyosikitisha mtu unapoachwa safarini..Sasa jiulize, kwa mtu ambaye haujaanza kabisa safari, yeye atakuwa katika hofu nyingi kiasi gani?..Ndivyo ilivyo hali yako wee Upo katika dhambi, upo mautini, mbingu ipo mbali na wewe.

Sikia sauti ya Kristo, inayokuambia njoo kwangu leo.. Uanze naye safari njema ya kuelekea ufalme wa mbinguni. Kukutana na ujumbe kama huu si bure, Ni Mungu anazungumza na wewe.

Yesu anasema..

Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.(Yohana 14:6)..

Ikiwa unataka na wewe kwenda mbinguni basi YESU ndiye njia..wala hakuna mwingine.

Vile vile biblia inasema..

Isaya 35:8 “Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia hiyo”.

Dunia hii inapita na mambo yake..Utauhangaikia huu ulimwengu mpaka lini, Ukifa leo, ni nani atakuwa mgeni wako huko uendako?. Ni nani atakayekupokea, utaulizwa safari yako ilikuwa ya kuelekea wapi, utajibu nini..Kwanini leo usichukue tiketi yako mkononi, uanze maisha mapya na Bwana Yesu..Kwasababu ni kweli atayabadilisha maisha yako na wewe mwenyewe utaona ni jinsi gani umeianza safari njema, ya uhakika na yenye matumaini..Ulevi, uzinzi, starehe, sema leo ni mwisho ninaamua kumgeukia Kristo.

 Ikiwa unataka kufanya hivyo leo.

Basi uamuzi unaoufanya ni wa busara sana ambao hautakaa uujutie maisha yako yote kama ilivyokuwa hata kwetu sisi. Unachopaswa kufanya, hapo ulipo, chukua muda mchache ujitenge peke yako. Kisha piga magoti, kisha fuatisha sala hii kwa Imani, ukijua kuwa Mungu yupo hapo karibu na wewe pembeni yako kukusikia..Kisha ukiwa sasa katika utulivu Sema sala hii kwa sauti.

EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU  MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.

ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.

AMEN.

Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithitisha toba yako kwa Vitendo ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo, Sasa Mungu akishaona umegeuka kwa vitendo basi toba yako anaipokea na atakuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako. Vile vile unahitaji, kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwambudu Mungu, na kujifunza biblia ili uukulie wokovu. Na vilevile ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.

Ubarikiwe sana

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

FUATILIA NDOTO HII, UTAJIFUZA KITU.

PENGINE MUNGU ALISHASEMA NAWE KWA NJIA HII.

KUOTA UPO UCHI.

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

USHUHUDA WA RICKY:

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Geofrey
Geofrey
1 year ago

Nimeota niko na wangu tunasafiri na basi kutoka mkoani kuelekea Dar. Mara dereva akashuka gari likawa linayumba. Kondakta hakuchukua hatua. Nikaamua kuingilia Kati kuliendesha kea nyuma. Nikaliegesha pembeni maana lilikuwa linataka kusababisha ajali. Mara dereva akarudi anaingia kwenye gari mm nikiwa nimetoka kidogo. Kurudi, gari limeondoka na wangu wadogo wawili. Nikabaki nahangaika