Biblia inasema tusikopeshe kwa riba, je! Wanaowakopesha watu kwa riba wanafanya dhambi?
JIBU: Biblia imezuia kutozana riba ndugu kwa ndugu tu..lakini kwa wengine nje ya ndugu sio dhambi kuwatoza riba.
Kumbukumbu 23:19 “Usimkopeshe ndugu yako kwa riba; riba ya fedha, riba ya vyakula, riba ya kitu cho chote kikopeshwacho kwa riba; 20 mgeni waweza kumkopesha kwa riba, ila usimkopeshe ndugu yako kwa riba; ili Bwana, Mungu wako, apate kukubarikia katika yote utiayo mkono wako, katika nchi uingiayo kuimiliki”.
Kumbukumbu 23:19 “Usimkopeshe ndugu yako kwa riba; riba ya fedha, riba ya vyakula, riba ya kitu cho chote kikopeshwacho kwa riba;
20 mgeni waweza kumkopesha kwa riba, ila usimkopeshe ndugu yako kwa riba; ili Bwana, Mungu wako, apate kukubarikia katika yote utiayo mkono wako, katika nchi uingiayo kuimiliki”.
Kwa mfano ndugu yako unamwona anayoshida, anaomba umkopeshe fedha kidogo, halafu wewe unatumia ile fursa kumwambia aongeze na kiwango kingine cha fedha juu yake(riba), kama faida yako, Hiyo ni dhambi, akikopa, basi arudishe kile kile alichokopa..Usigeuze shida za ndugu yako kuwa mtaji..
Katika hali ya kawaida hata bila kuambiwa na mtu au kufundishwa, ukiwa na nyumba ya biashara, halafu ndugu yako wa karibu amekuja kukaa hapo kwa kipindi fulani tu.. Huwezi kumwambia alipie kodi kamili kama watu wengine, anaweza kulipia tu zile gharama za kawaida ndogo ndogo lakini sio kulipia kila kitu..hakuna mtu mwenye utu anaweza kumfanyia hivyo ndugu yake.
Hali kadhalika katika Ukristo, wote tuliomwamini Yesu Kristo tunafanyika kuwa ndugu..Upendo wa Kristo unatuunganisha pamoja.tunakuwa tunapendana bila masharti..Upendo huo unatufanya kusiwepo hata na hamu ya kutaka faida kutoka kwa ndugu zetu katika Imani kama vile ilivyo katika ndugu zetu wa mwili. Ndio hapo biblia inatuasa kwamba tusitozane riba sisi kwa sisi. Lakini kwa mtu mwingine nje na ndugu zetu wa kimwili na kiimani, tunaweza kuwatoza ili tupate faida katika tunavyovifanya..kwasababu riba ndio inayokifanya kile kitu au ile shughuli ile iendelee mbele zaidi.
Lakini tukiwatoza ndugu zetu kwa lengo la kupata faida hapo upendo wa Kristo haupo ndani yetu, na hivyo tunafanya dhambi na kumkosea Mungu.
Ezekieli 22:12 “Ndani yako wamepokea rushwa ili kumwaga damu; umepokea riba na faida; nawe kwa choyo umepata mapato kwa kuwadhulumu jirani zako, nawe umenisahau mimi, asema Bwana MUNGU.
Ubarikiwe.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
USILETE UJIRA WA KAHABA, NYUMBANI KWA MUNGU.
Je! ni sahihi kwa Mkristo kusherekea siku yake ya kuzaliwa.[Birth day]?
USIWE NA HOFU, USHUKAPO CHINI.
EWE MKE! HESHIMA YAKO IPO KWA WAKWE ZAKO.
JINSI NEEMA YA MUNGU ILIVYOKUWA KUBWA KWA MKE WA LUTU.
Rudi Nyumbani:
Print this post
Nauliza kwenye Upande wa kukopa kwenye mabenki na kurudisha riba je ni dhambi?
Ubarikiwe sana mpendwa kwa mafundisho mazuri kila siku yananijenga kwenda hatua ingine ya uelewa