Sodoma ipo nchi gani?

Sodoma ipo nchi gani?

Sodoma ipo nchi gani?


Sodoma na Gomora ni miji iliyokuwa katika nchi ya Kaanani (Ambayo ndio Israeli ya Sasa). Miji hii miwili ni moja kati ya miji mitano iliyokuwa katika bonde la Yordani..mingineyo  ikiwemo, ni Adma, Seboimu, na Lasha.

Kama tunavyoijua habari, miji hii miwili (yaani Sodoma na Gomora) ndiyo iliyokuwa kiini cha maovu yote katika bonde hilo.

Mwanzo 19:24 “Ndipo Bwana akanyesha juu ya Sodoma na juu ya Gomora kiberiti na moto toka mbinguni kwa Bwana.

25 Akaangusha miji hiyo na Bonde lote, na wote waliokaa katika miji hiyo, na yote yaliyomea katika nchi ile”.

Hata hiyo mingine nayo haikupona, nayo pia iliangamizwa;

Kumbukumbu 29:23 “ya kuwa nchi yake nzima ni kibiriti, na chumvi, na kuteketea, haipandwi, wala haizai, wala nyasi hazimei humo, kama mapinduko ya Sodoma na Gomora, Adma na Seboimu, aliyoipindua Bwana kwa ghadhabu yake na hasira zake”;

Lakini ni tahadhari gani tunapaswa tuchukue tunaposoma habari ya miji hii miovu?

Licha ya kuwa ilikuwa ni miovu lakini biblia inatuambia ilikuwa ni miji yenye kuvutia sana, mfano wa Edeni, Bustani ya Bwana soma (Mwanzo 13:10). Mfano tu wa dunia ya sasa. Ulimwengu wa sasa umejengeka na unavutia kuliko ule wa zamani,hilo lipo wazi, starehe za wakati ule haziweki kulinganishwa hata kidogo na starehe za wakati huu, lakini maovu yake ni  zaidi ya yale ya Sodoma na Gomora.

Ushoga sio jambo la kushangaza tena, kiasi kwamba nchi zimefanikiwa kuhalalisha jambo hilo, na sehemu nyingine mpaka kwa yanayoyaita makanisa (ambayo kiuhalisia si makanisa), yamevuka mpaka huo na kuhalalisha ushoga bila hata kuogopa kumuhusianisha Mungu na matendo kama hayo maovu. Hiyo ni kuonyesha kuwa mwisho wa huu ulimwengu upo karibuni sana. Wapo watu wanajidanganya kuwa hii dunia haitaangamizwa, kwasababu Mungu alishasema hivyo wakati ule wa Gharika kuwa hatagharikisha.. Lakini hawajui kuwa ni kweli Mungu hatauangamiza huu ulimwengu kwa maji, lakini amesema ataugharikisha moto. Ambapo kila mtu mwovu, na kila kitu kitafumuliwa, biblia inasema hivyo soma.

2Petro 3:7 “Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu……..

10 Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.

11 Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa,

12 mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka”?

Unaona?  Swali la kujiuliza ni je! Sisi tumejiwekaje? Katika kipindi hichi cha mwisho? Je na sisi tutapumbazwa na Ulimwengu huu kama Lutu na mke wake? Tukaacha kubaki mahali Mungu alipotuweka tukaenda kushikamana na mambo ya ulimwengu huu yanayodanganya?. Huu ni wakati wa kujiokoa nafsi yako, na si wakati wa kumwangalia ndugu, au rafiki, au mjomba anasemaje, kwasababu mwisho upo karibu.

Je umeokoka?

Kama bado na upo tayari kufanya hivyo leo, huo ni uamuzi wa busara sana kwako, kama upo tayari kumpa Yesu maisha yako leo, basi fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba, na maelekezo mengine >>>>  SALA YA TOBA

Bwana akubariki sana.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

JINSI SODOMA NA GOMORA ILIVYOKUWA INAVUTIA SANA..

MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

Israeli ipo bara gani?

CHUKIZO LA UHARIBIFU

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments