Mruba ni mdudu gani kwenye biblia?(Mithali 30:15)

Mruba ni mdudu gani kwenye biblia?(Mithali 30:15)

Mithali 30:15 Mruba anao binti wawili, Waliao, Nipe! Nipe! Kuna vitu vitatu visivyoshiba kamwe, Naam, vinne visivyosema, Basi!

16 Kuzimu; na tumbo lisilozaa; Nchi isiyoshiba maji; na moto usiosema, Basi!

Mrubu au ruba ni mdudu mfano wa  mnyoo, ambaye anapatikana sehemu za maji maji , na matope, kama vile kwenye madimbwi, mito, au mifereji. Wanaangukia katika kundi la wadudu wafyonza damu. Wana midomo ambayo inavutika kama mipira, kiasi kwamba wakinasa mahali, labda tuseme  kwenye ngozi au sehemu laini ya mwili ni ngumu kuwatoa, watakaa hapo wakifyonza tu damu mpaka basi,..Tazama picha juu.

Zamani walisifika kwa kuwanata sana sana farasi, kwenye pua zao na ndimi zao, pale walipokuwa wanakwenda kunywa maji kwenye mito.

Tabia pekee ya hawa wadudu ni kuwa, wanaponasa mahali hawatoki, kazi yao ni  kufyonza tu damu, bila kutosheka, watafanya hivyo hata kukaribia kupasuka. Hawana tabia ya kuridhika,.

Sasa picha aliyokuwa anaitoa huyu mfalme Aguri bin yake, ni kuwa kuna baadhi ya watu wanaweza kufananishwa na mdudu huyu na uzao wake;

Tujiulize je na sisi ni miruba?

Ikiwa  siku tu tunafanya maovu hatutosheki.. leo tunalewa, kesho tunalewa, kesho kutwa tunalewa..ukiona upo hivyo ujue wewe ni mruba usiye choka kusema nipe!, nipe.!

Tuna tamaa za mali, zilizopitiliza, mpaka tunafanya mambo yasiyompendeza Mungu, leo tunataka tuwe kama Yule, kesho kutwa kama Yule, hivyo tunaiba, tunatapeli , tunadhulumu n.k…Huo ni Uruba! Haswaa.

Paulo alisema ..

1Timotheo 6:6 “Walakini utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa.

7 Kwa maana hatukuja na kitu duniani, tena hatuwezi kutoka na kitu;

8 ila tukiwa na chakula na nguo tutaridhika na vitu hivyo.

9 Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu.

10 Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi”.

Ridhika, na urefu wako, ridhika na rangi yako, ridhika na familia yako, ridhika na kipato chako. Ukiwa mtu wa kuridhika utaishi maisha ya amani, na ndivyo Mungu atakavyokuzidishia. Lakini ukiwa kama mruba, ambaye anafyonza tu damu,  haridhiki mpaka anakaribia kwenda kupasuka. Ujue upo katika hatari mbaya sana ya kuanguka katika imani ikiwa wewe ni mkristo.

Bwana atusaidie katika hilo;

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

KUNA MAJIRA MUNGU ATAIVURUGA MIPANGO YETU.

Ngome ni nini?  Kwanini Mungu anafananishwa na ngome?

Ni kwanini mifugo ya Yakobo iliongezeka kwa wingi kiasi kile?

Nyinyoro ni nini?

Je ni wanyang’anyi wawili waliomtukana Bwana Yesu au mmoja?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments