SIFONGO NA SIKI NI NINI?

SIFONGO NA SIKI NI NINI?

SWALI: Sifongo na siki ni nini, alizopewa Bwana Yesu pale Msalabani?

JIBU: Tusome..

Yohana 19: 28  “Baada ya hayo Yesu, hali akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe, akasema, Naona kiu.

29  Kulikuwako huko chombo kimejaa siki; basi wakatia sifongo iliyojaa siki juu ya ufito wa hisopo, wakampelekea kinywani.

30  Basi Yesu alipokwisha kuipokea ile siki, alisema, Imekwisha. Akainama kichwa, akaisalimu roho yake”

Sifongo ni kiswahili cha neno la kiingereza “sponge” ambalo sisi tumezoea kujitaja neno hilo kama SPONCHI au SPONJI...Sasa yapo masponchi ya aina nyingi…yaliyozoeleka sana ni yale yaliyotengenezwa na malighafi ya godoro, Mara  nyingi yanatumika kwa kuoshea vyombo na matumizi mengine, kwasababu yanakuwa yanauwezo wa kufyoza maji na kutengeneza povu. Enzi za zamani (za Bwana Yesu) yalikuwepo pia masponji, ambayo yalikuwa yanakaribiana sana kufanana na haya ya kwetu ya sasa. (Tazama picha chini, mfano wa sifongo za kale)

sifongo

Hivyo Sifongo ni sponji. Sasa tukirudi kwenye maandiko tunasoma yule askari, alitwaa hiyo Sifongo na kulitia kwenye SIKI, na lengo la kufanya hivyo ni ili hiyo SIKI ijifyonze kwenye hiyo sifongo.

SASA SIKI NI NINI?

Siki ni kiungo ambacho kinakuwa katika kimiminika, kinachotengenezwa kwa kuchachushwa kama vile zinavyotengenezwa pombe…Na kimiminika hicho kazi yake ni kuongeza ladha kwenye chakula au kukihifadhi chakula kisiharibike…Zipo siki za aina nyingi kulingana na jamii za watu na tamaduni. Huku kwetu Afrika hususani Afrika mashariki, Siki haziwi katika mfumo wa kimiminika kizito sana…lakini nchi nyingine zinatengenezwa viwandani na kuwa kama Maji (mfano wa hizo ni zile vanilla zinazotumika kwenye ice-cream na keki ambazo zinakuwa zinahifadhiwa kwenye kachupa kadogo), na pia maeneo ya Mashariki ya kati, ikiwemo Taifa la Israeli, siki zao zilitengenezwa na Zabibu, hivyo zilikuwa hazina tofauti sana na Divai.

Kwahiyo siki iliyotumika pale msalabani ilikuwa ni kama Divai, lakini si divai kabisa…Na zilitumika katika matumizi ya vyakula.  Hivyo wale askari walichovya sifongo kwenye siki na kuiweka kwenye mti, ili ifike juu pale msalabani alipokuwepo Bwana Yesu.(Tazama mfano wa siki ya divai katika picha ya juu kabisa ya somo hilo)

Na kwasababu siki kwaasili ni INA UKALI, inaukakasi na ni chungu na ina tindikali nyingi, kwa ufupi haifai kuwekwa katika kinywa cha mwanadamu kwa ukali wake, walifanya vile ili Mwili wa Bwana Yesu ukaukiwe maji…kwasababu walimsikia akisema Naona kiu.

Sasa ipo siri kubwa sana katika tukio hilo lililotendeka hapo juu msalabani, Kama utapenda kufahamu zaidi siri hiyo basi unaweza kufungua hapa >> YESU ANA KIU NA WEWE

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

Hanithi ni nini katika biblia? (kumbukumbu 23:17)

Mlima Gerizimu na Ebali ni ipi, na umuhimu wao rohoni ni upi?

Pomboo ni nini katika biblia?(Kutoka 25:5, Ezekieli 16:10)

Mkomamanga ni nini? Na katika biblia unawakilisha nini?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
5 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
QUATERMA ALLAN
QUATERMA ALLAN
1 year ago

AMINA MTUMISHI WA KRISTO YESU BABA YETU MILELE

Caroline Nnko
Caroline Nnko
1 year ago

Amen barikiwa kwa kazi njema.tunajifunza mengi sana ktk mwili wa Kristo.

Finda
Finda
3 years ago

Bwana Yesu asifiwe mtumishi wa MUNGU. Nimekuwa nikiota ndoto napaa hadi mawinguni kama ndege nikiwa naenda sehemu fulani. Nakuwa nafurahi sana kuangalia chini nikiona mawinguni, mito na misitu mingi ya kupendeza. Wakati mwingine nakua nakimbia mbio ila kwa spidi isiyo ya kawaida. Nini maana yake ?