KUOTA UNAPAA.

KUOTA UNAPAA.

Mpaka mtu au kitu kiweze kupaa ni wazi kuwa kimefanikiwa kushinda hali inayoweza kukivuta chini. Na ndio maana kinachopaa kama ndege huwa kina kasi zaidi na kinaona mbali sana tofauti na kitu kinachotembea. Hata mtu akijiona kwenye ndoto anapaa kutoka sehemu moja hadi nyingine huwa anajiona ni mwepesi sana, na anayokasi tofauti na anavyoota ndoto nyingine.

Sasa ndoto hizi zinaweza kutoka katika vyanzo viwili, chanzo cha kwanza ni kwa Yule mwovu. ili kujua ndoto uliyoota inatoka kwa Yule mwovu, utaona pengine unapaa na watu usiowajua na wanakupeleka usipojua, au unaenda sehemu za kutisha, na unapoamka unakuwa huna amani umejawa na hofu na wasiwasi mwingi, ukiona hivyo fahamu kuwa ndoto hiyo ni ya kutoka kwa Yule mwovu, hivyo kama wewe ni mkristo, unapaswa uikemee saa hiyo hiyo kwa jina la YESU na mambo kama hayo hayatakutokea tena..

Lakini ikiwa unaota unapaa tu katika mazingira ya kawaida labda tuseme nyumbani, au hata kama ni maeneo usiyoyajua lakini ni ya asili na unajiona unaowezo wa kuruka mbali sana kama vile upo mwezini, na ndoto hiyo inajirudia rudia na ukiamka huoni chochote,kawaida tu, basi unapaswa uzingatie kwasababu ni Mungu anakupitishia ujumbe wake hapo na hivyo umefanya vema kutafuta kujua tafsiri yake.

Sasa kama bado upo nje ya YESU KRISTO, Mungu anakuonya furaha yako, au mafanikio yako, ni ya muda tu, Kwasasa unaweza ukawa katika hali ambayo huwezi ukajifananisha na wengi, pengine umefanikiwa, au umesoma zaidi, au umepiga hatua Fulani, lakini mwisho wako utakuwa ni mbaya sana, kama hutamrudia muumba wako. Unapojiona unapaa ni ishara ya kufanikiwa Fulani.

Ayubu 20:4 “Je! Hujui neno hili tangu zamani za kale, Tangu wanadamu kuwekwa juu ya nchi,

5 Ya kuwa shangwe ya waovu ni kwa muda kidogo, Na furaha ya wapotovu ni ya dakika moja tu?

6 Ujapopanda ukuu wake mpaka mbinguni, Na kichwa chake kufikilia mawinguni;

7 Hata hivyo ataangamia milele kama mavi yake mwenyewe; Hao waliomwona watasema, Yuko wapi?

8 ATARUKA MFANO WA NDOTO, asionekane; Naam, atafukuzwa kama maono ya usiku,”

Hivyo tubu umgeukie Mungu, kama ulikuwa unafanya mambo maovu, Tubu, uishi kama mkristo, kama ulikuwa unafanikiwa kutoka katika biashara haramu kama uuzaji pombe, au madawa ya kulevya,  au rushwa au ushirikina acha mara moja mgeukie yeye…Bwana YESU anasema itakufaidia nini kuupata ulimwengu mzima halafu upate hasara ya nafsi yako.?..Unafanikiwa sasa lakini mafanikio yako yatakupoteza hivyo mgeukie Mungu..Bwana anakupenda na ndio maana anakuotesha ndoto za namna hiyo.

Lakini kama upo ndani ya Kristo, basi fahamu kuwa Mungu anakusisiza uzidi kumtazama yeye zaidi kwasababu anaompango wa kukushushia vipawa vya kimbinguni zaidi, kwasababu sikuzote mbinguni ndipo vipawa vilipo..

Zaburi 68:18 “Wewe umepaa juu, umeteka mateka, Umepewa vipawa katikati ya wanadamu; Naam, hata na wakaidi, Bwana Mungu akae nao”.

Hivyo songa mbele, kama ulikuwa unalegalega ungeza nguvu zaidi Bwana yupo karibu na wewe usiangalie mazingira yanayokuzunguka, zidi kumtafuta Mungu kwa bidii.ili kupaa kwako kusiishie tu hapa duniani bali mpaka mbinguni..Kama vile Kristo, alimpendeza Mungu akapaa hadi mbinguni kwa Baba, na sisi pia tumewekewa siku moja ya kupaa  moja kwa moja na siku hiyo ndio ile siku ya UNYAKUO ambayo tutwenda kumlaki Bwana Yesu mawinguni. Maran Atha!

Ubarikiwe!

Group la whatsapp Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi

Mada Nyinginezo:

KUOTA UPO UCHI.

KUOTA UNAFANYA MTIHANI.

KUOTA NYOKA.

KUOTA MTU ALIYEKUFA.

FUATILIA NDOTO HII, UTAJIFUZA KITU.

MTETEZI WAKO NI NANI?

UNYAKUO.


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
8 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Steve
Steve
10 months ago

Amen

Finda
Finda
2 years ago

Asante sana mtumishi, ila kwa zaidI ya mara tatu sasa nikiamka asubuhi nasikia tumbo likinguruma. Kunguruma kwa tumbo hakunisumbui ila sauti inayotoka ndio inanitia wasiwasi, maana ni sauti ya njiwa (in HD form) maana yake ni nini?

Selina
Selina
3 years ago

Asante san Kwa ujumb maan naotaga napaa

Finda
Finda
3 years ago

Amina mtumishi, ubarikiwe sana

robert mwangi
robert mwangi
3 years ago

hujambo natarajia uko xalama,pia mimi nimekuwa nikiota nikipaa juu angani kwa muda xaxa

James
James
4 years ago

Amen
Nimebarikiwa na maelezo kuhusu ndoto ya kupaa angani.
Hata usiku wa kuamkia siku ya leo nimeota nkipaa.
Ninahii ndoto kwa mda mrefu sasa