Kuota unafanya Mtihani.

Kuota unafanya Mtihani.

Hii ni moja ya ndoto ambayo inaotwa na watu wengi sana, na hii huwa inachukua maumbile tofauti tofauti, wengine utakuta wanaota wanafanya mitihani na hawajajiandaa, wanachoshtukia tu ni wakati wa mtihani umefika, na hakuna chochote walichofanya wanajiuliza siku zote alikuwa wapi…wengine wanaota wanafanya mtihani mgumu sana lakini wenzao wanaonekana wanafahamu cha kujaza yeye hajui,

wengine wanaota kama walikatisha masomo wakaondoka, baadaye waliporudi muda umeshapita mitihani ya mwisho imekaribia, wengine wanaota wamerudia madarasa ya nyuma ambayo tayari wameshayavuka siku nyingi na ni lazima wayavuke ili waendelee na madarasa ya mbele, wengine wanaota wapo wanafundishwa, wengine wanapewa adhabu, wengine wapo tu n.k.…Kwa ufupi ndoto unazoota upo katika mazingira ya shule, zote zina maudhui moja.

Na ndoto hizi huwa zinatesa sana, zinaweza kujirudia hata kila baada ya wiki au mwezi, au miezi kadhaa, inategemea na mtu na mtu, lakini ni ndoto ambazo haziachi kuja.

Biblia inasema..

Ayubu 33:14 “Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.

15 Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;”

Mungu siku zote huwa anapenda kutumia vitu vinavyotuzunguka kutufikishia sisi ujumbe fulani , na ndio maana utaona Bwana Yesu alipokuwa anafundisha mifano yake yote alikuwa anatumia mambo ya kawaida tu yanatozunguka sikuzote ili kutufikishia sisi ujumbe na tuulewe utaona wakati mwingine alitumia mifano ya ndege, wafanyabiashara, wafalme, harusi n.k…

Hivyo na Mungu ili kukufikisha ujumbe wake wa wokovu huwa anapenda kutumia mfano wa kitu ambacho kimetukuka sana mbele yako, kitu chenye maana sana kwako ambacho ukikikosa anajua kabisa umekosa maisha na hicho si kingine zaidi ya  ELIMU.

Kufunua kuwa Ipo elimu iliyokuu ambayo inayo ufunguo sio tu wa maisha ya hapa bali pia wa maisha ya ulimwengu unaokuja, na hiyo si nyingine zaidi ya Elimu ya Ufalme wa Mbinguni..Mungu anakuonyesha hali yako ya kiroho ilivyo kupitia maisha yako ya shuleni, kama unavyojiona upo shuleni hujajiandaa, au mtihani ni mgumu basi katika roho ndivyo hivyo ulivyo..  kuwa upo nyuma, na unapaswa ushinde, yapo madarasa haujayavuka bado, upo pale pale kiroho umekwama, unatamani uendelee mbele unashindwa au unaona ni ngumu kwasababu bado hujayamaliza madarasa ya nyuma Mungu aliyokupa.

Hivyo unapaswa uongeze bidii yako kwa Mungu, ili ufike pale Mungu anapotaka kufika, ongeza kiwango chako cha maombi, jifunze Neno la Mungu sana, ishi maisha yanayompendeza Mungu, punguza muda wa kuihangaikia dunia, na ongeza muda wako wa kumtafuta Mungu, kwasababu yeye ndio ufunguo wa kweli wa maisha yako ndugu. Ukimpata Mungu umepata vyote.

Mathayo 6:33 “Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.”

Hivyo ukiwa na bidii na  Mungu akaridhika na wewe basi atakuvusha na kukupeleka katika kiwango kingine cha kiroho na kiufahamu. Kumbuka Mungu anakupenda na ndio maana anakuonyesha ndoto kama hizo, Hivyo usipuuzie ungeza bidii yako kwake.

Ubarikiwe.

Group la whatsapp Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi

Mada Nyinginezo:

NITAONGEZAJE NGUVU ZANGU ZA ROHONI?

TABIA ZA ROHONI.

NI WAKATI GANI SHETANI ANAPENDA KUMSHAMBULIA MWAMINI?

ZIFAHAMU HUDUMA KUU (10) ZA SHETANI DUNIANI.

HATA ILIPOTIMIA SIKU YA PENTEKOSTE.

MTEGEMEE MUNGU, NA SI MWANADAMU.


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
19 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
PASKAZIA FABIAN
PASKAZIA FABIAN
5 months ago

Nimeewa
Naomba kuuliza ukiota unadondika kwenye mti maana yake ninj

Rehema Nelson
Rehema Nelson
1 year ago

Ahsantee nimeelewa.

Aisa
Aisa
1 year ago

Usiku wankuamkia leo trh 9/2/23, nimeota Niko nafanya mitihani, na sijasoma wala sijui Cha kujibu! Pia kuna ndoto niliota miaka km miwili imepita kwamba niliingia nyumbani kwa tu nikangatwa Sana ma mbwa mkono wangu wa Julia, niliumia Sana nikatoka nje tena nikangatwa na mbwa!

Mercy cheli
Mercy cheli
1 year ago

Huwa naota nafanya mapenzi na aliyekuwa mume wangu maanake

Anonymous
Anonymous
1 year ago

I was understnd

privah
privah
1 year ago

Shalom.. Niliota nafanya mtihani ila nikawa wa kwanza kumaliza kabla ya wote na nikatoka nikawaacha wengne ina maana Shalom.. Niliota nafanya mtihani ila nikawa wa kwanza kumaliza kabla ya wote na nikatoka nikawaacha wengne ina maana gani

Steven Tindwa
Steven Tindwa
2 years ago

Shalom man of God. I ask for your spiritual assistance about my dream which is bothering me until now because I don’t know the meaning of this dream. I dreamed that I’m doing an exam of English subject and I did not finish, then I woke up, after waking up then I slept again and I dreamed that I’m doing exam of kiswahili subject and Didi not finish too. What is the massage of to me through this dream? Please help me.

Andy
Andy
2 years ago

Asante ubarikiwe nimeota hivyo hivyo najiandaa kufanya mtihani halafu sijajiandaa kabisa yani kama nilikuwa doja wa shule natokea Shuleni naambiwa kuna Mtihani, asante sana Mungu akubariki

Anonymous
Anonymous
2 years ago

Asante ubarikiwe nimeota hivyo hivyo najiandaa kufanya mtihani halafu sijajiandaa kabisa yani kama nilikuwa doja wa shule natokea Shuleni naambiwa kuna Mtihani, asante sana Mungu akubariki

Anonymous
Anonymous
1 year ago
Reply to  Anonymous

Nimeota nafanya mtihani na mtihani ulikuwa rahis sanaaa je hiyo in maana gani?

Emmanuel Kitengule
Emmanuel Kitengule
2 years ago

Asante sana mwalimu, binafsi kati ya ndoto ambazo zimenisumbua kwa muda mrefu ni hizi.Nimepata maarifa sasa, Asante sana kwa mafafanuzi haya kwani yanakidhi sana shauku yangu ya kujifunza.

Anonymous
Anonymous
2 years ago

Ameni

Anonymous
Anonymous
3 years ago

Amen

BENEDICT MNYASUMBA
BENEDICT MNYASUMBA
3 years ago

Asante Kwa tafsiri yako

Denis DiDas
Denis DiDas
3 years ago

Asante kwa tafsuri yako, ukweli unaweza