Vivyo hivyo na wewe unayejijua ni mkristo, kumbuka shetani atakusubiria katika engo hiyo pia, wakati unapitia mazingira magumu, hatakuja wakati upo kwenye raha, au mafanikio, atakutafuta kwenye shida, na misiba, huko ndipo atakapokuletea hata vipengele vya maandiko kichwani mwako, ili tu kukutoa katika mstari wa imani, atakuleta vishawishi vingi, wa watu wengi wa ajabu, atakupa mpaka njia mbadala ya kufanya kama vile alivyomshauri Bwana Yesu ageuze jiwe liwe mkate.
Lakini nataka nikuambie kupitia shida, au udhaifu au taabu ya kitambo fahamu kuwa sio uthibitisho kuwa Mungu amekuacha maadamu unafahamu kuwa uhusiano wako na Mungu bado upo, usiikate imani ndugu..kuwa kama Daudi aliposema Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu nijapopita katika bonde la uvuli wa Mauti, sitaogopa kwa maana wewe upo pamoja nami, gongo lako na fimbo yako vyanifariji.(Zaburi 23).
Tukirudi pia katika mifano ile ile ya Wanyama wawindao kama simba au chui huwa wanapenda kumvamia yule aliye dhaifu, wakishakosa aliye peke yake katika kundi, au aliye mtoto katika kundi, huwa wanatafuta aliyedhaifu, au mgonjwa, kwasababu hawatasumbuka sana katika kumkamata..shetani naye ni kama simba angurumaye akitafuta mtu ammeze..maandiko yanasema hivyo… 1 Petro 5:8