KUOTA NYOKA.

KUOTA NYOKA.

Nakusalimu katika jina la mwokozi wetu YESU KRISTO, Suala la upambanuzi wa ndoto ni moja ya mambo ambayo yanawasumbua wengi, lakini kwa bahati mbaya watu wengi wamekosa kujua tafsiri ya ndoto zao, kulingana na maandiko…

Hivyo kabla ya mtu hukimbilia kupewa au kutafuta tafsiri ya ndoto yake ni vizuri kwanza akafahamu kuwa ndoto zimegawanyika katika makundi makuu matatu, kundi la kwanza ni zile ndoto zinazotokana na Mungu, kundi la pili ni zile zinazotokana na shetani na kundi la tatu ni ndoto zinazotokana na mtu mwenyewe, na hizi ndizo zinazochukua sehemu kubwa ya ndoto tunazoziota karibu kila siku, na aina hii ya tatu huwa inakuja kutokana na shughuli zetu tunazozifanya kila siku au mazingira yanayotuzunguka kila siku..

Ndoto za namna hii huwa hazibebi ujumbe wowote, hivyo hazihitaji kutafsiriwa, mara nyingi zinapaswa zipuuziwe..ikiwa hujafahamu vizuri namna ya kuitambua ndoto yako kulingana na makundi haya basi bofya somo hii ulipitie kisha ukishamaliza tuendelee…>> NITAJUAJE KAMA NDOTO NI YA MUNGU AU YA SHETANI?

Watu wengi wamekuwa wakiniuliza tafsiri ya ndoto hii ya kuota nyoka, sasa ikiwa ni ndoto ambayo inajirudia rudia, basi izingatie sana..kumbuka Nyoka katika maandiko tangu mwanzo anasimama kama ishara mbaya,

Na nyoka amebeba tabia kuu tatu, ya kwanza ni kudanganya kama tunavyomsoma pale Edeni alivyomdanganya Hawa (Mwanzo 3:1-5), tabia ya Pili ni kuuma kama biblia inavyotuambia atakugonga kisigino (Mwanzo 3:15), na ya tatu ni kumeza, kama tunavyosoma katika kitabu cha Ufunuo 12:4), pale alipotaka kummeza mtoto yule alipotaka kuzaliwa,..Na tabia hizi zote Shetani anazo na ndio maana kila mahali alifananishwa na joka, na sio kiumbe kingine chochote kama vile kondoo au njiwa.

Hivyo ndoto za namna hii nyingi zinatoka kwa shetani, na chache sana zinakuja kutoka kwa Mungu, lakini tukianza kuchambua upande mmoja mmoja hatutamaliza, wengine wanaota wanakimbizwa na nyoka, wengine wanaota wanaumwa na nyoka, wengine wanaota wameviringishwa na nyoka, wengine wanaota wapo karibu na ziwa au bahari na lijoka likubwa linatoka huko, wengine wanaota wanamezwa na joka, wengine wanaongea nayo n.k. n.k. vyovyote vile chamsingi ambacho mtu anapaswa kufahamu hapo ni kuwa ziwe zinatoka upande wa Mungu au upande wa shetani,..Ni kwamba ADUI YUPO MBELE YAKO.

Hapo Shetani yupo karibu na wewe kutimiza kazi hizo tatu au aidha mojawapo,

Jambo la kwanza ni  kukudanganya au tayari ameshakudanganya: Sasa Ikiwa upo nje ya Kristo yaani hujaokoka basi fahamu kuwa upo chini ya udanganyifu wa shetani tayari, hivyo hapo unaonyeshwa hali yako ilivyo rohoni, Jambo unalopaswa kufanya ni kurudi kwa Kristo haraka sana kabla udanganyifu haujawa mkubwa zaidi ukakuzalia matunda ya mauti, hapo ulipo tayari umepofushwa macho pasipo hata wewe kujijua. Hivyo tubu umgeukie Mungu haraka sana, maadamu muda bado upo.

Au kwa namna nyingine shetani anakaribia kukushawishi kuingia katika kosa au dhambi ambayo itakugharimu sana, hata maisha yako, hivyo angalia njia zako, uchukue tahadhari, funga milango yote ambayo unaona itakupeleka mbali na Kristo, acha kufanya vitu ambavyo sasa hivi unavifanya unaona kabisa havimpendezi Mungu, acha haraka sana, upo mtego wa shetani nyuma yake.

Pili shetani anakutegea mtego au anataka kukuletea madhara aidha katika huduma yako, au afya yako,au familia yako au shughuli yako, anataka kukugonga kisigino chako usisonge mbele, hapo unapaswa uongeze kiwango chako cha maombi kama Bwana Yesu alivyosema ombeni msije mkaingia majaribuni..Hivyo ili kumshinda silaha uliyonayo ni kuomba sana.

Tatu shetani anataka kukimeza kile ambacho Mungu amekipanda ndani yako:

Na jambo la kwanza huwa anakimbilia ni NENO LA MUNGU hilo ndilo huwa anafanya bidii sana kupambana nalo kwasababu anajua likishakuwa ndani ya mtu litakwenda kuleta madhara makubwa sana katika ufalme wake hivyo anasimama hapo karibu na wewe ili akimeze kile ulichokisikia.. inafananishwa na zile mbegu ambazo zilingukia njiani ndege wakaja kuzila,

Mathayo 13:18 “Basi ninyi sikilizeni mfano wa mpanzi.

13.19 Kila mtu alisikiapo neno la ufalme asielewe nalo, huja yule mwovu, akalinyakua lililopandwa moyoni mwake. Huyo ndiye aliyepandwa karibu na njia.”

Hivyo kwa ufupi ikiwa upo nje ya Kristo fanya hima uingie ndani, na ikiwa upo ndani ya Kristo chukua tahadhari uimarishe uhusiano wako na Kristo kwasababu shetani yupo karibu na wewe kushindana nawe kwa kila hali..

Ubarikiwe.

Group la whatsapp Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Mada Nyinginezo:

TOFAUTI KATI YA NDOTO NA MAONO NI IPI?

AMIN! NAWAAMBIA KIZAZI HIKI HAKITAPITA.

CHUKIZO LA UHARIBIFU.

JE! WEWE NI MWANA WA IBRAHIMU?

USIONDOE ALAMA YA MPAKA ILIYOWEKWA NA MABABA.

UZAO WA NYOKA.


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
9 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Drosta
Drosta
11 months ago

Mimi nimeota kuna dada 1 alikuwa rafiki yangu siku za nyuma tulikuwa tunatembea njiani yeye akawa amenitangulia mtoto wake yupo katikati na mimi nikawa nyuma yao tukaenda tukafika mbele tukakutana na mto ulikuwa una maji machafu yule dada alikuwa ametutangulia akavuka ule mto alipofuka wakati anafata mtoto wake avuke nikaliona joka kubwa jeusi lipo kwenye huo mto nilivyoona mimi nikarudi sikutaka kuvuka tena nilivyorudi nyuma nikakutana na watu nikawaelezea nilichokutana nacho ndo wakaniambia mbona tunasikia kelele yule mtoto analia atakuwa anamezwa na yule joka wakachukua mawe silaha wakakimbilia kule mtoni kwenda kumuua yule joka ndo nikashutuka nitatoka usingizini. hiyo ndoto ina maana gani Mtumishi wa Mungu

Gloria
Gloria
3 years ago

Niliota et mpnzi wangu amenunua gari zuri jeus lakin hilo gar hakuliendrsha mimi nilipanda hilo gar badae nikajiona npo na mwanaume mwngne kne hilo gar lakon kiti cha dreva hakikua na mtu tukajiona tumefika sehem alikuwepo huyo mpnz wngu tukawa tunamsubir apande ili atuendeshe akawa anaosha samak lakin hakupanda. Ina mana gani??

Esther
Esther
3 years ago

Naomba kuuliza ina maana gani hii, nmeota nyoka mara 3 ..mara ya Kwanza kaning’ata kisigino, mara ya pili nmeota nmemkuta nje ya Choo na mara ya tatu nmeota tulikua na wenzangu tulivyomuona
tu uyo nyoka tukaanza kukimbia..

Rachel Urio
Rachel Urio
3 years ago
Reply to  Esther

Jaman Mungu akubariki sana mtumishi wake, mm nimeokoka lakin siku za ivi karubun nimekuwa nikandamwa sana na majanga yaan nikanza kuomba au kufanya ibada za asubuhi na jion najikuta nimesahau na kuacha kuendelea alafu baadae nakumbuka tena naanza jipya sasa nikaamua kufunga ili nimuombe Mungu anishindie ktk hili pia nimekuwa nikiomba kazi sehemu nyingi sana lakin sifanikiwi hivyo niliunganisha maombi moja ikiwa ni Mungu aniimarishe katka maombi na pili kupata kazi maana kuna mbali nimeomba sasa jana nilifanya na nilshinda nikiomba usiku nilipolala nikaota kuna joka kubwa linapigana na mm lakin cha kushangaza nilikuwa nikiomba na likawa linaogopa sana lakin alikufa ni kama nilionyeshwa lipo uvunguni kwangu ndoto yangu ikaishia hapo

Grace
Grace
4 years ago

Mara yakwanza Nikiwa ki dato cha 4 mwaka Jana niliota nakumbizwa n nyoka Ila nilikimbia San nilipofika mbele Kuna mty alinivuta nikashutuka Mara ya pili juz niliota nmelala nyoka yupo ju ya mbao kila akitaka kunigonga namkwepa nikashutuka

Vai
Vai
4 years ago

Nimetoa Niko kama napita kwenye kibaraza za nyumba na ndani kama kuna watu na hapo ninayopika tuko wengi tunapishana ila mimi na mtu mwingine simjui tukaona nyoka kwa chini ya kibaraza wengi aina mbalimbali akanirushia panga tukarukia kwa chini na kuwaangamiza kwa kuwekata vichwa mara yule mwingine simuoni nimebaki peke yangu nikaendelea kupambana ili wasijeenda kwenye kibaraza na kudhuru watu nyoka mmoja mweusi nikamkata shingo na panga ilikatika nusu na panga likabaki hapo akawa anajikokota nilimtafuta nimalizie nikamkata anamezwa na nyoka wa kijani mrefu kiwiliwili kimeangalia juu mkia wakati nashangaa nikashtuka usingizini.Maana yake nini?