Ukichunguza kwa karibu utaona kuwa Bwana alikuwa katika utaratibu wa kuwaponya watu wote waliokuwa wanamfuata lakini hakuwa anazungumza chochote baada ya kuwaponya, kwasababu hakuona kitu kingine cha ziada ndani yao. Lakini kwa akida aliona kitu cha ziada, vivyo hivyo na kwa yule mwanamke aliyekuwa anatokwa na damu kwa muda wa miaka 12 (Luka 8:43), aliona makutano wote wanataka njia zile zile za kuponywa tu, kuwekewa mikono, kutembelewa nyumbani, kuombewa, wengine walishatuma maombi ya kumwona Bwana pengine mwezi mmoja kabla, wengine walikuwa wameshamaliza ngazi za chini, wameshatoka kuwaona mitume, sasa wanakaribia ngazi ya juu ya kumfikia YESU, n.k.
Lakini yeye alisema kwanini nipitie shida zote hizo,pengine angetaka kusubiria mpaka zamu yake ifike ingemchukua mwaka mzima, isitoshe kulikuwa na watu wenye matatizo makubwa hata kuliko yeye, lakini yeye alisema “nikishika pindo la vazi lake tu nitapona saa hiyo hiyo”, ALIMUHESABIA kuwa kama mikono yake inaponya kwanini na vazi lake lisiponye pia?. Kadhalika na yule mwanamke wa Tiro (Mathayo 15:21), Kadhalika na Zakayo naye. n.k.