Mwanamke Mshunami

Mwanamke Mshunami

SWALI: Katika Biblia tunamsoma Mwanamke mmoja aliyeitwa Mshunami, ambaye alimsaidia Nabii Elisha sehemu ya malazi wakati wa huduma yake..Mwanamke huyu aliitwa Mshunami

2 Wafalme 4:12 “Akamwambia Gehazi mtumishi wake, Mwite yule Mshunami. Naye alipokwisha kuitwa, akasimama mbele yake. 13 Akamwambia, Sema naye sasa, Tazama, wewe umetutunza sana namna hii; utendewe nini basi? …”

Sasa Swali Mshunami maana yake nini?

JIBU: Ukisoma Mlango huo kuanzia juu kidogo, utaona kuwa Mshunami sio jina la mtu bali ni jina la sehemu..

2 Wafalme 4:8 “Hata ikawa siku moja, Elisha alikwenda Shunemu; na huko kulikuwa na mwanamke mmoja mwenye cheo; naye akamshurutisha aje ale chakula. Ikawa kila alipopita njia ile, huingia kula chakula”.

Kwahiyo Mshunami sio jina la Mtu, bali ni jina la mahali…Katika Israeli kulikuwa na mahali panapoitwa “SHENEMU” Kwahiyo mtu yeyote awe mwanamke au mwanamume kama ametokea sehemu hiyo basi aliitwa Mshunami…Ni sawa na nchi Tanzania, yeyote aliyetokea huko ataitwa Mtanzania.

Hivyo SHUNEMU ilikuwa ni Eneo la Israeli, lililokuwa urithi wa kabila la Isakari…Tunalithibitisha hilo katika kitabu cha…

Yoshua 19:17 “Kisha kura ya nne ilitokea kwa ajili ya Isakari, maana, ni kwa ajili ya wana wa Isakari kwa kuandama jamaa zao.

18 Na mpaka wao ulifikilia Yezreeli, na Kesulothi, na Shunemu

Na sio tu huyu mwanamke aliyemsaidia Nabii Elisha alitokea huko shunemu, kuna wanawake wengine pia biblia imerekodi walitokea huko huko shunemu…Mmoja wapo na Abishagi aliyeletwa kwa Mfalme Daudi

1 Wafalme 1:3 “Basi wakatafuta kijana mzuri mipakani mwote mwa Israeli, wakamwona Abishagi, Mshunami, wakamleta kwa mfalme.

4 Naye kijana huyo alikuwa mzuri sana; akamtunza mfalme, akamtumikia; walakini mfalme hakumjua”

Mungu akubariki


Mada Nyinginezo:

VIFUNGO VYA GIZA VYA MILELE.

TUSIFUNGWE NIRA PAMOJA NA WASIOAMINI.

KWANINI TUWE WENYE BUSARA KAMA NYOKA?

JE! NI KWELI DUNIA ILIUMBWA TAKRIBANI MIAKA 6000 ILIYOPITA? NA JE! SHETANI ALIKUWEPO DUNIANI WAKATI DUNIA INAUMBWA?

TUMEAMBIWA TUNAPOSALI TUSIPAYUKE-PAYUKE, JE! HUKO KUPAYUKA PAYAUKA NDIO KUPI?


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Imani
Imani
2 years ago

I’m on line now