ALIWAANGAMIZA BAADAYE WALE WASIOAMINI.

ALIWAANGAMIZA BAADAYE WALE WASIOAMINI.

Karibu tujifunze Biblia, Neno la Mungu wetu lililo Mwanga wa Njia zetu,  na Taa iongozayo miguu yetu (Zaburi 119:105).

Neno hili lililo Taa linasema..

Yuda 1:5 “Tena napenda kuwakumbusha, ijapokuwa mmekwisha kujua haya yote, ya kwamba Bwana, akiisha kuwaokoa watu katika nchi ya Misri, ALIWAANGAMIZA BAADAYE WALE WASIOAMINI”

Maandiko hayo yanatufundisha kuwa KUOKOLEWA sio Mwisho wa safari. Kwani ni kweli wana wa Israeli waliokolewa kutoka Misri jeshi lote.. lakini si wote walioingia nchi ya Ahadi, bali watu wawili tu  ambao ni Yoshua na Kalebu, na watoto wao ambao walizaliwa jangwani, lakini wengine wote MUNGU aliwaangamiza jangwani ijapokuwa aliwatoa Misri.

Leo wanaookolewa ni WENGI, wanaomkiri YESU ni wengi!, lakini pia ni wengi wanaoangamizwa na Bwana, kwasababu ya kutotembea na Mungu katika wokovu wao.

Wengi wa wana wa Israeli walijaa viburi (Mfano wa Dathani na Kora, soma Hesabu 16:1-50) na wengine walijaa mioyoni mwao manung’uniko na ibada za sanamu, na wengine walikuwa ni watu wa kumjaribu Mungu kila wakati..ingawa wote walikuwa wameokoka na utumwa wa Farao, lakini kwa bahati mbaya hawakuiona ile nchi ya Ahadi.

WALIOKOLEWA lakini baadaye WALIANGAMIZWA!…. WALIFUNGULIWA lakini baadaye WALIANGAMIZWA…. WALIPONYWA lakini baadaye WALIANGAMIZWA… Na jambo linalohuzinisha Zaidi ni kwamba waliangamizwa jangwani wakiwa bado wanakula Mana (Baraka za mbinguni), Vile vile waliangamizwa wakiwa chini ya WINGU NA NGUZO YA MOTO (Upako na Utumishi) na Zaidi ya yote walikuwa wameshabatizwa katika roho katika bahari ya Shamu.

Mambo haya yanabaki kuwa funzo na onyo kwetu ili tusifanya makosa kama hayo, kama maandiko yasemavyo..

1Wakorintho 10:1  “Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari;

2  wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari;

3  wote wakala chakula kile kile cha roho;

4  wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo.

5  Lakini wengi sana katika wao, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani.

6  Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani.

7  Wala msiwe waabudu sanamu, kama wengine wao walivyokuwa; kama ilivyoandikwa, Watu waliketi kula na kunywa, kisha wakasimama wacheze.

8  Wala msifanye uasherati, kama wengine wao walivyofanya, wakaanguka siku moja watu ishirini na tatu elfu.

9  Wala tusimjaribu Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu, wakaharibiwa na nyoka.

10  Wala msinung’unike, kama wengine wao walivyonung’unika, wakaharibiwa na mharabu.

11  Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.

12  Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke”.

Je unajivunia ubatizo?… Unajivunia dhehebu?…unajivunia Karama uliyo nayo?… unajivunia upako?.. Vyote hivyo wana wa Israeli walikuwa navyo, lakini wengi wao waliangamizwa.

Utakase ukristo wako, kaa mbali na dhambi!, usimjaribu Mungu, usiabudu sanamu baada ya kuokoka, jitenge na mambo ya ulimwengu, tembea na Mungu kama Yoshua na Kalebu, na Bwana atusaidie sote katika hayo.

Amen.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

SHIKA SANA ULICHO NACHO, ASIJE MTU AKAITWAA TAJI YAKO.

Je Henoko aliyeenda na Mungu alikuwa ni mwana wa Kaini? (Mwanzo 4:16)

MNGOJEE BWANA

ILI NIWE KIELELEZO KWA WALE WATAKAOMWAMINI BAADAYE.

NIFANYALO WEWE HUJUI SASA; LAKINI UTALIFAHAMU BAADAYE.

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments