Jibu: Turejee,
Mwanzo 4: 16 “Kaini akatoka mbele za uso wa Bwana, akakaa katika nchi ya Nodi, mbele ya Edeni. 17 Kaini akamjua mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Henoko; akajenga mji akauita Henoko, kwa jina la mwanawe”.
Mwanzo 4: 16 “Kaini akatoka mbele za uso wa Bwana, akakaa katika nchi ya Nodi, mbele ya Edeni.
17 Kaini akamjua mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Henoko; akajenga mji akauita Henoko, kwa jina la mwanawe”.
Henoko aliyeenda na Mungu hakuwa mwana wa Kaini, kwasababu Uzao wa Kaini wote ulilaaniwa, na hivyo hakutoka nabii yeyote wala mtu yeyote mwenye rekodi ya kumpendeza Mungu katika huo uzao, bali uzao wote uligharikishwa na ile gharika.
Swali kama ni hivyo kwanini Henoko aonekane hapa kama ni uzao wa Kaini?.
Jibu ni kwamba Huyu Henoko anayetajwa hapa katika (Mwanzo 4:16) sio yule aliyeenda na Mungu, bali alikuwa ni Henoko mwingine, kwasababu jina hilo ‘Henoko’ hakuwa nalo mtu mmoja tu!, bali ni wengi waliitwa kwa jina hilo, kama tu leo majina yetu yanavyoweza kuwa ya watu wengine mahali pengine.
Lakini yule Henoko, aliyekuwa mtumishi wa Mungu, na aliyempendeza Mungu alitokea katika Uzao wa Sethi na habari zake tunazisoma katika Mwanzo mlango wa 5.
Mwanzo 5:18 “Yaredi akaishi miaka mia na sitini na miwili, akamzaa Henoko. 19 Yaredi akaishi baada ya kumzaa Henoko miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake. 20 Siku zote za Yaredi ni miaka mia kenda na sitini na miwili, akafa. 21 Henoko akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela. 22 Henoko akaenda pamoja na Mungu baada ya kumzaa Methusela miaka mia tatu, akazaa wana, waume na wake. 23 Siku zote za Henoko ni miaka mia tatu na sitini na mitano. 24 Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa”.
Mwanzo 5:18 “Yaredi akaishi miaka mia na sitini na miwili, akamzaa Henoko.
19 Yaredi akaishi baada ya kumzaa Henoko miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake.
20 Siku zote za Yaredi ni miaka mia kenda na sitini na miwili, akafa.
21 Henoko akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela.
22 Henoko akaenda pamoja na Mungu baada ya kumzaa Methusela miaka mia tatu, akazaa wana, waume na wake.
23 Siku zote za Henoko ni miaka mia tatu na sitini na mitano.
24 Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa”.
Huyo ndio Henoko aliyeenda na Mungu, ambaye alikuwa mwana wa Yaredi wa uzao wa Sethi, na alikuwa ni mtu wa saba kutoka kwa Adamu (Yuda 1:14). Lakini yule mwingine alikuwa mwana wa Kaini.
Ni sawa Lameki aliyetajwa katika Mwanzo 4:18-19, ambaye alioa wake wawili, na yule aliyetajwa katika Mwanzo 5:28-31 ambaye alikuwa ni baba yake Nuhu… Hawa walikuwa ni Lameki wawili tofauti wenye tabia mbili tofauti, ingawa majina yao yalifanana…ndivyo ilivyo pia kwa hawa Henoko wawili tuliojifunza habari zao.
Sasa Ni jambo gani tunaloweza kujifunza kwa Henoko aliyeenda na Mungu?
Alikuwa ni mtu aliyeenda na Mungu; Maana yake Njia zake zilimpendeza Mungu mpaka kufikia hatua ya Mungu kumtwaa, na kabla ya Mungu kumtwaa biblia inasema alionyeshwa ujio wa Bwana, siku ile atakayokuja na watakatifu wake kwaajili ya vita vya Harmagedon na utawala wa miaka 1000 duniani.
Yuda 1:14 “Na Henoko, mtu wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hao, akisema, Angalia, Bwana alikuja na watakatifu wake, maelfu maelfu, 15 ili afanye hukumu juu ya watu wote, na kuwaadhibisha wote wasiomcha Mungu, kwa ajili ya kazi zao zote za upotevu walizozitenda bila kumcha Mungu, na kwa ajili ya maneno magumu yote ambayo hao wenye dhambi wasiomcha Mungu wameyanena juu yake”
Yuda 1:14 “Na Henoko, mtu wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hao, akisema, Angalia, Bwana alikuja na watakatifu wake, maelfu maelfu,
15 ili afanye hukumu juu ya watu wote, na kuwaadhibisha wote wasiomcha Mungu, kwa ajili ya kazi zao zote za upotevu walizozitenda bila kumcha Mungu, na kwa ajili ya maneno magumu yote ambayo hao wenye dhambi wasiomcha Mungu wameyanena juu yake”
Bwana atusaidie na sisi tuwe watu wa kwenda na Bwana katika njia zake kama alivyokuwa Henoko.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Je! tunapaswa kukiamini Kitabu cha Henoko?
JE! Kaini alimpatia mke wake wapi?
Mtu wa kwanza kufa alikuwa nani?
Wanefili walikuwa ni watu gani?
EPUKA MAKUNDI ILI UTAKATIFU WAKO UDUMU!.
Rudi nyumbani
Print this post
Mungu Awabariki kwa makala nzuri
Amina ubarikiwe mtumishi wa BWANA