LISHA KONDOO WANGU, LISHA WANA-KONDOO WANGU.

LISHA KONDOO WANGU, LISHA WANA-KONDOO WANGU.

Masomo maalumu kwa watumishi wa Mungu,

Je kibiblia ni jukumu la wachungaji peke yao kulichunga kundi? Na mitume na manabii hiyo si kazi yao??….. kama ndio basi huenda Bwana Yesu alikosea alipomwambia Petro ambaye ni Mtume, alichunga kundi lake..

Tusome,

Yohana 21:15  “Basi walipokwisha kula, Yesu akamwambia Simoni Petro, Je! Simoni wa Yohana, wewe wanipenda kuliko hawa? Akamwambia , Naam ,Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, LISHA WANA-KONDOO WANGU.

16  Akamwambia tena mara ya pili, Simoni wa Yohana, wanipenda? Akamwambia, Ndiyo, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, CHUNGA KONDOO ZANGU.

17  Akamwambia mara ya tatu, Simoni wa Yohana, wanipenda? Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, Wanipenda? Akamwambia, Bwana, wewe wajua yote; wewe umetambua ya kuwa nakupenda. Yesu akamwambia, LISHA KONDOO ZANGU”.

Kumbe kazi ya kuchunga, na kulisha kondoo si ya mchungaji peke yake, bali hata ya mitume, na waalimu na manabii na wainjilisti… Ikiwa na maana kama Bwana amekupa watu chini yako ni lazima ujue kuwa unawajibu wa kuwachunga na kuwalisha…pasipo kuweka visababu sababu.

Sasa leo hatutazungumzia sana kuhusiana na KUCHUNGA kondoo.. lakini tutalitazama jukumu la KULISHA KONDOO ulilopewa wewe kama mtumishi wa Mungu.

Awali ya yote ni muhimu kujua kondoo ni nani?

Kondoo ni mnyama asiyeweza kujiongoza mwenyewe na Bwana Yesu anao watu ambao siku zote hawataweza kusimama wenyewe (maana yake siku zote watahitaji msaada tu ili waendelee kudumu katika Imani na katika kuifanya kazi ya Mungu). Na kundi hili ni kubwa kuliko lile kundi la watumishi wa Mungu.

Kundi la hili lisipochungwa vizuri na kulishwa ipasavyo linaharibika na kupotea kabisa, na shetani ndilo analolitafuta sana….

Sasa Bwana alimpa jukumu Petro, na anakupa jukumu wewe kama mtumishi wa Mungu, pasipo kujali karama yako, kuwa LISHA KONDOO WAKE lakini si tu kondoo bali pia WANA-KONDOO, Haya ni makundi mawili ambayo ni lazima ujifunze kuyatofautisha.

Tofauti ya kondoo na Mwana kondoo, ni hii; Kondoo aliyekomaa anajulikana kwa jina hilo la “Kondoo” na kondoo aliye chini ya umri wa mwaka mmoja anaitwa “mwana-kondoo”. Sasa Bwana alimwambia Petro alishe makundi hayo yote mawili, na anatuambia pia sisi..

Chakula cha kondoo aliyekomaa ni tofauti na cha yule mchanga.. huwezi kuwalisha wote chakula kinachofanana, kwani kundi moja litadhoofika.. ukimpa maziwa kondoo aliyekomaa, atadhoofika, vile vile ukimpa chakula kigumu kondoo mchanga ataathirika.. kwahiyo ni lazima ujifunze kukigawanya chakula kulingana na makundi ya watu walio chini yako.

Ni lazima uwe na chakula cha waongofu wapya, na chakula cha waliokomaa kiimani, na ni  sharti lazima Makundi yote yale chakula cha kushiba..

Ni lazima chakula chako kilenge kuwakuza wale kondoo wachanga (maana yake wakue kiroho) na kuwanenepesha wale kondoo waliokomaa (maana yake wajae maarifa). Tukiwa watumishi wa aina hiyo basi mbele zake Bwana tutaonekana tunampenda lakini kama hatuwalishi inavyopaswa na huku tunajivuna kuwa sisi ni watumishi wa Mungu, basi bado hatujalijua pendo la Kristo?.

Hivyo Kama Mtumishi wa Mungu jenga tabia ya kulitazama kundi lako (Sawasawa na Mithali 27:23)..usisieme mimi ni Mtume sina karama hiyo?, na huku unawalisha watu mambo yasiyowajenga, hata Petro alikuwa ni Mtume na si mchungaji lakini alipewa hilo jukumu na Bwana la kulisha vizuri kondoo watakaokuwa chini yake, usiseme mimi ni Nabii sina wito huo na huku unawalisha watu maono ya uongo na mafundisho manyonge…hata Musa alikuwa ni nabii lakini alibeba jukumu hilo la kuwalisha watu amri, na sheria za Mungu.

Maran atha.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

JE! UNAMPENDA BWANA?

“Nitampiga mchungaji na kondoo wa kundi watatawanyika”,Maana yake nini?

Nitajuaje kuwa nimesamehewa dhambi zangu?

NI LIPI KATI YA MAKUNDI HAYA, WEWE UPO?

USIMLAANI KIZIWI, WALA USITIE KWAZO MBELE YA KIPOFU.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Ezra ndambuki
Ezra ndambuki
10 months ago

Wamtumainio bwana nikama mlima sayuni hawatatingishika milele habari hizi zinao uzito mwingi Sana hasa katika hao wachungaji maana kwakweli ukizielewa kwa undani zaidi kundi ulilonalo sio rahisi lipotee Bali kwa kupuuza ni huangamifu

EDGAR WILSON SANANE
EDGAR WILSON SANANE
10 months ago

Naam Barikiwa sana! Kweli kila mtu aliyekwisha kumpokea Bwana Yesu kristo anakazi ya kufanya ili kuujenga ufalme wa Mungu. Mfano waimbaji na makundi ya sifa na mahabusu wamtukuze Mungu ktk Roho na kweli maana kuna watu wanainuliwa na kutiwa moyo kuendelea na safari ya wokovu.

Anonymous
Anonymous
10 months ago

Hakika MUNGU atusaidie kwakweli atupe huo ujasiri ya kuwalisha na kuwajenga na wengine