Kwanini Kristo aitwe Mwana-kondoo. (Yohana 1:29)

Kwanini Kristo aitwe Mwana-kondoo. (Yohana 1:29)

Yohana 1:29 “Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!”.

Bwana Yesu sehemu nyingine anajulikana hivi kama Mwana-kondoo kufuatia tabia ya kondoo ilivyo.

Kondoo ni mnyama mpole sana na mnyenyekevu, tofauti na Mbuzi.. Kondoo Anapokatwa manyoya yake huwa hajigusi anatulia sana, na pia hawezi kujichunga mwenyewe huwa anamtegemea mchungaji asilimia mia. Tofauti na mbuzi au Ng’ombe.

Lakini pamoja na hayo kondoo aliyekomaa ambaye tayari kashaota pembe ijapokuwa ni mpole lakini kuna vipindi vichache vichache anakuwa na hasira hususani wakati wa mvua, na pia anapokutana na kondoo mwingine aliye wajinsia kama yake. Hivyo Bwana Yesu hajajifananisha na kondoo aliyekomaa, kwasababu anazo kasoro nyingi.. bali anajifananisha na kondoo mchanga, (mwana-kondoo) ambaye bado hata hajaota pembe, ambaye hawezi kupambana, aliye mnyenyekevu na mpole.

Bwana Yesu naye ni mpole mfano wa huyo.. Maandiko yanamshuhudia hivyo..

Mathayo 21:5  “Mwambieni binti Sayuni Tazama, mfalme wako anakuja kwako, MPOLE, naye amepanda punda, Na mwana-punda, mtoto wa punda”.

Na yeye mwenyewe anajishuhudia hivyo  katika Mathayo 11:28.

Mathayo 11:28  “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

29  Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; KWA KUWA MIMI NI MPOLE na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;

30  kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi”.

Je umemfuata Yesu aliye mpole?..yeye anayeongea nawe kwa sauti ya upole moyoni mwako, kwamba utubu dhambi?.

Kama bado unasubiri nini?

Okoka leo na ukabatizwe na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu nawe utapata ondoleo la dhambi…na jina lako litaandikwa katika kitabu cha uzima cha mwanakondoo na utakuwa na nafasi katika mji ule, mbingu mpya na nchi mpya.

Ufunuo 21:27 “Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo”.

Maran atha.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Upole ni nini?

LISHA KONDOO WANGU, LISHA WANA-KONDOO WANGU.

Je ni kweli Musa alikuwa mtu mpole kuliko wote duniani?

JE! UNAMPENDA BWANA?

MWANANGU, NIPE MOYO WAKO;

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
1 year ago

Mungu awabariki. Nimejifunza jambo la Muhimu Sana