SHIKA SANA ULICHO NACHO, ASIJE MTU AKAITWAA TAJI YAKO.

SHIKA SANA ULICHO NACHO, ASIJE MTU AKAITWAA TAJI YAKO.

Ufunuo 3:11 “Naja upesi. SHIKA SANA ULICHO NACHO, asije mtu akaitwaa taji yako”.

Hapo anasema “..Asije mtu.” na si “..Asije shetani”. Maana yake anayeitwaa taji ya mtu ni MTU, kwasababu shetani yeye taji lako au langu halimsaidii kitu, kwasababu haendi kulivaa.. lakini mwingine akilichukua litaenda kumfaa anakokwenda!.

Labda tuzidi kuliweka hili vizuri..

Aliyelichukua Taji la “Yuda Iskariote” ni mtu aliyeitwa “Mathiya”… baada ya Yuda kushindwa kushikilia alichopewa…

Matendo 1:24  “Kisha wakaomba, wakasema, Wewe, Bwana, ujuaye mioyo ya watu wote, tuonyeshe ni nani uliyemchagua katika hawa wawili,

25  ashike mahali katika huduma hii na utume huu, alioukosa Yuda, aende zake mahali pake mwenyewe.

26  Wakawapigia kura; kura ikamwangukia Mathiya; naye akahesabiwa kuwa pamoja na mitume kumi na mmoja”.

Vile vile aliyeichukua Taji ya “ESAU” ni ndugu yake “YAKOBO”…Baada ya kuidharau ile haki yake ya mzaliwa wa kwanza kwa tamaa ya chakula kimoja tu.

Waebrania 12:16 “Asiwepo mwasherati wala asiyemcha Mungu, kama Esau, aliyeuuza urithi wake wa mzaliwa wa kwanza kwa ajili ya chakula kimoja.

17  Maana mwajua ya kuwa hata alipotaka baadaye kuirithi baraka, alikataliwa (maana hakuona nafasi ya kutubu), ijapokuwa aliitafuta sana kwa machozi”

Umeona unapoacha kuthamini kile ulichopewa, basi mwingine atakichukua,..unapoacha kuthamini nafasi yako mwingine ataichukua.. Unapoacha kuthamini huduma yako uliyopewa na Mungu, mwingine ataichukua na utapoteza thawabu zako.

> Umepewa huduma ya Uinjilisti, usiipuuzie na kuifanya kilegevu.. Bwana anaweza kuiondoa kwako na kumpa mwingine atakayeifanya vizuri na kwa ushujaa.

> Umepewa huduma ya maombezi, fanya hayo kwa bidii, usipuuze kwani Bwana anaweza kuiondoa kwako na kumpa mwingine ikiwa utaipuuza.. na thawabu yako (Taji yako) utakuwa umeipoteza.

> Umepewa huduma ya kukirimu (kwamba kupitia ulivyopewa unahudumia watumishi na kazi ya Mungu) basi usidharau neema hiyo kwasababu Bwana anaweza kuiondoa kwako na kumpa mwingine na hivyo Taji yako ikaondoka, fanya uliyojaliwa na BWANA kwa bidii sana..(Na huduma nyingine zote ni hivyo hivyo).

SHIKA SANA ULICHO NACHO!!.. SHIKA SANA ULICHO NACHO!!!… SHIKA SANA ULICHO NACHO!! Kwasababu kina thamani kubwa!.. Hakikisha unakizalia matunda.

Na majira haya, shoka lipo kwenye mashina ya miti kukata kila tawi lisilozaa,

Luka 3:9 “Na sasa hivi shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni”.

Bwana atusaidie tusikatwe. Lakini Neno ni moja tu kwetu. TUSHIKE SANA TULIYO NAYO!!!

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Kwanini Bwana Yesu alivikwa taji ya miiba?

YUDA ISKARIOTE! MTUME ALIYECHAGULIWA NA BWANA YESU.

MAUMIVU  NYUMA-YA-HUDUMA.

FAHAMU MAISHA YA YESU KABLA YA HUDUMA.

Je vazi alilovikwa Bwana Yesu lilikuwa la Zambarau au Jekundu?

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments