JITAHIDI KUJA KABLA YA WAKATI WA BARIDI.

JITAHIDI KUJA KABLA YA WAKATI WA BARIDI.

2Timotheo 4:21  “Jitahidi kuja kabla ya wakati wa baridi. Eubulo akusalimu, na Pude, na Lino, na Klaudia, na ndugu wote pia”

Mtume Paulo ni mtu aliyetambua kuwa kustawi kwa huduma yake kunategemea sana sapoti ya watendazi wenzake wengine wenye ni moja na yeye. Hivyo tunasoma wakati akiwa Rumi kama mfungwa, alimwandikia waraka mwanawe Timotheo, aiharakishe huduma yake, ili amfuate kule Rumi wasaidiane katika huduma kabla ya wakati wa bariki kuanza.

“Jitahidi kuja kabla ya wakati wa baridi”.

Paulo alijua mazingira yanaweza kukawiisha kusudi la Mungu. Hivyo alitambua kuwa mtu akiongeza jitihada anaweza kukamilisha mambo yake mapema kabla mazingira Fulani hayajamuathiri kutenda kusudi lingine la Mungu.

Kwa ukanda waliokuwa, ilikuwa ni ngumu sana, meli kusafiri nyakati za baridi kwasababu ya barafu baharini, hivyo safari zote za majini zilisitishwa kwa miezi kadhaa mpaka baridi itakapoisha ndipo safari zianze tena, Paulo aliliona hilo akatambua ni jambo la asili haliwezi kuepukika kwa kufunga na kuomba, isipokuwa kwa kupangilia tu ratiba vizuri.

Hii ni kutufundisha sisi, tufahamu kuwa mazingira Fulani, au nyakati Fulani zisizo rafiki sana huwa zinapita, au zitakuja mbele yetu ambazo zinaweza zikawa ni kikwazo cha utumishi kwa sehemu Fulani.

Kwamfano wakati wa baridi kwako, unaweza kuwa ni wakati wa ndoa. Kama wewe ni kijana hujaoa/ hujaolewa, unanafasi sasa ya kumtumikia Mungu kwa uhuru wote. Titahidi sana kufanya hivyo sasa, kwasababu nafasi hiyo inaweza ikapungua kwa sehemu uingiapo katika majukumu ya kindoa. Usipojitahidi sasa kujiwekea msingi mzuri kwa Mungu wako, utataabika sana kuujenga huo uwapo kwenye ndoa.

Wakati wa baridi unaweza ukawa ni kipindi cha kazini au masomoni. Ikiwa bado hujapata kazi, au upo likizo kazini au shuleni, embu tumia vema wakati wako, kuongeza kitu kikubwa katika ufalme wa Mungu, kwasababu shughuli zitakapokulemea, kuujenga tena huo msingi itakuwia ngumu sana, na kama ikiwezekana yaweza kukuchukua wakati mrefu. Uwapo ‘free’ usilale, bali tumia sasa kuongeza mikesha, maombi ya masafa marefu, kusoma biblia yote.

Wakati wa baridi waweza kuwa uzee. Kwa jinsi umri unavyokwenda ndivyo uwezo wa mwili wako unavyopungua, Hivyo utengenezapo mambo yako mapema na Bwana, basi wakati huo ukikukuta hautakuathiri sana, kwasababu tayari yale ya msingi uliyopaswa uyafanye umeshayafanya mapema, uzeeni ni kumalizia tu.

Zipo nyakati nyingi za baridi. Chunguza tu maisha yako ujue wakati wako wa baridi unafika lini na ni upi, kisha jitahidi sana, kuwekeza kwa Mungu sasa, kimaombi, kiusomaji Neno, na kiuinjilisti.

Bwana akubariki

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

MCHE MWORORO.(Opens in a new browser tab)

Nini maana ya kikombe cha maji ya baridi(Mathayo 10:42)?

Je ni wakina nani ambao hawataonja mauti mpaka siku ya kuja Bwana?

(Opens in a new browser tab)Fahamu maana ya Mithali 25:13 Kama baridi ya theluji wakati wa mavuno;(Opens in a new browser tab)

(Opens in a new browser tab)Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Devis Julius administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments